
Shirika la afya dunia WHO linashauri unyonyeshaji wa watoto kwa miezi
sita baada ya kuzaliwa bila kumpa vyakula vingine. Baada ya miezi sita
mtoto aanze kupewa vyakula vingine kama ziada ya maziwa ya mama, na
inashauriwa umuanzishie mtoto matunda na mboga mboga zilizopondwa.
Inashauriwa pia unyonyeshaji wa mtoto uwe usiku na mchana kwa kadiri
mtoto atakavyohitaji na matumizi ya chupa za kunyonyeshea yaepukwe.
0 comments:
Post a Comment