Vifo vya gafla kwa watoto wachanga imekuwa ni ngumu kwa wazazi
kujua nini ni chanzo chake.Kwenye jamii zetu za kiafrika watu wengi
huusisha vifo vya watoto na mambo ya ushirikina pale mtoto anapofariki
bila kuumwa haswa akiwa usingizini ,sababu wengi hawana elimu ya kutosha
juu ya vifo vya gafla. Takwimu inaonyesha watoto wakiume ndio
wanaadhiriwa sana kuliko watoto wa kike.
Kifo cha gafla kiitalamu huitwa Suddenly Infant Death syndrome (
SIDS) au (Crib death) kinatokea kwa watoto wenye umri 0 mpaka mwaka 1
hutokea pindi wakiwa wamelala .Vifo vingi huwapata sana watoto wenye
umri wa 0 mpaka miezi sita na kiasi kidogo kwa wamiezi 6-12.Chanzo chake
haijajulikana moja kwa moja ila kunavitu vinavyochochoea kwa kiasi
kikubwa,
:Kulamza kwa tumbo- ni hatari sababu upumuaji wake unakuwa watabu
ukiangalia hizo picha 2 tofauti anaweza pata hera vizuri akilalia
mgongo ni rahisi kwa Trachae kupitisha hewa kwa urahisi tofauti na
akilalia tumbo .
:Sigara -uvutaji wa sigara ndani ya nyumba au eneo alilopo mtoto ni
hatari mapafu yake hayaja komaa kupokea moshi mkali wenye sumu(NICOTINE)
na kumuadhiri kwa haraka.
:Watoto wanaozaliwa chini ya wiki 38( njiti) wapo kwenye hatari ya kupata vifo cha gafla
:Mama kama alitumia sigara,pombe au bangi kipindi cha ujauzito anauwezo mkubwa wa kumsababishia mtoto kifo cha gafla
:Watoto wenye infection kwenye mfumo wa hewa.
NJIA ZA KUEPUKA KIFO CHA GAFLA
:Mlaze mtoto kwa mgongo-usimlaze ubavu au tumbo sababu position ya
kumlazia tumbo inamfanya apate hewa ya oxygen kwa kiasi kidogo
inasababisha hewa ishindwe kusafirishwa kwenye ubongo ndio hapo inakuwa
rahisi kufariki kwa mtoto.
:Mama anaenyonyesha mtoto kwa kipindi cha mwaka na kuendelea
anapunguza hatari ya kifo cha gafla kwa mtoto kwa asilimia 50,kuliko
mtoto anaepewa maziwa ya kopo.
:Epuka matumizi ya sigara ndani ya nyumba au sehemu aliopo mtoto
:Mnunulie Pacifier zile chuchu za kunyonya mdomoni zinazuia kifo cha gafla.
:Utakapo mlaza kitanda cha watu wazima hakikisha asijigonge ukutani
au kusiwe na mpenyo kati ya kindani na ukuta anaweza ingia kati na
kukosa hewa na kubanwa.
:Hakikisha kitandani hakuna nguo ,mashuka ,toys,au mto vikamziba
pua akakosa hewa wakati wa kujigeuza,na kumbuka mtoto mchanga hana uwezo
wa kujitoa shuka iwapo litamfunika uso
:Mtoto kulala kitandani kwake anakuwa safe ,kumwepusha kujigonga kwenye ukuta au angle za kitanda na kuanguka,
:Epuka kumfunika na shuka kubwa au zito ,mtoto anahitaji shuka
jepesi ,na iwapo utalala nae hakikisha humfuniki na nguo zako ,au shuka
puani akakosa hewa au mwili ukachemka sana.
Nimuhimu kumwangalia mtoto mara kwa mara pindi akiwa amelala unaweza
ukamnunulia baby monitor inasaidia kumsikia akiwa anapumua,analia
,anacheka n.k inakuwa rahisi kujua kama kuna lolote lineal endelea
chumbani.
0 comments:
Post a Comment