Showing posts with label makala. Show all posts
Showing posts with label makala. Show all posts

Tuesday, September 5, 2017

Image result for madhara ya fangasi kwa mjamzito
Maambukizi  ya fangasi kwa mama mjamzito hutokea kutokana na kubadilika
kwa homoni mwilini ikiambatana na upungufu wa kinga mwilini huku
ikielezwa kuwa si kila mjamzito ana uwezekano wa kupata maambukizi.

Matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi vimetajwa kuwa kisababishi kimoja
wapo kinachoweza kumfanya mama mjamzito apate fangasi hasa wa aina ya
Candida albicans.

Wakinamama wajawazito wanaoweza kupata maambukizi ya fangasi ni wale
wenye tabia ya kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri
kama nguo za kuogelea (swim wear), nguo za ndani zilizotengenezwa kwa
kitambaa aina ya nailon au zinazobana sana.

Akizungumza na mwandishi wa Hivisasa Afisa matibabu katika zahanati ya
Kigogo Dokta Ambakisye Mwalusamba ameeleza kuwa licha ya matumizi ya
nguo au mavazi yanayoleta joto lakini pia mtindo wa kujamiiana kwa
kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi vyenye
glycerin wakati wa tendo la ndoa kuna uwezekano mkubwa wa kupata
maambukizi ya maradhi haya.

Aidha ametaja namna muathirika wa maradhi hayo anavyotakiwa kupata
vipimo ni pamoja na kumueleza daktari kumfahamisha mgonjwa aina ya
kipimo, lengo lake na jinsi kitakavyofanyika ili kumuandaa kisaikolojia
huku kabla ya kumfanyia vipimo vya uchunguzi wa uke ambavyo kitaalamu
huitwa Per Vaginal Examination (PV exam) kuona kama kuna uvimbe wowote
ndani ya uke au kama ana maumivu wakati wa kujamiiana hali
Itakayoashiria wazi kuwako kwa aina fulani ya fangasi katika sehemu hizo.

Hata hivyo Daktari anaweza kuchukua kipimo na kuotesha kwenye mahabala
ili kuangalia aina ya uoto huo kama ni wa fangasi aina ya Candida
albicans, au atafanya kipimo cha mkojo (Urinalysis) na cha ugonjwa wa
kisukari, HIV/AIDS, ugonjwa wa  kuvimba tezi la koo (goiter) na kadhalika.

Amefafanua kuwa Dokta ataangalia kama kuna uchafu wowote unaotoka, wingi
wake, rangi yake, harufu yake, uzito wake na aina ya uchafu unaotoka
kama ni sahihi kutokana huku akilinganisha na  maelezo ya mgonjwa.

Jinsi ya kujikinga na Fangasi

– kutovaa nguo za kubana ambazo zitapelekea kusababisha joto ukeni   na
kuacha majimaji  yatakayosababisha fangasi,

– Mama huyo anashauriwa kujifuta na kujikausha vizuri katika sehemu za
siri pindi anapotoaka      kuoga au kujisaidia kutoka kwamba pindi
atakapokuwa katika kipindi cha ujauzito hutoka na jasho mara kwa mara na
kubanwa na haja ndogo.

– Kuacha tabia ya kuvaliana nguo au kuazima nguo za mtu mwingine  huenda
 ikawa ana ugonjwa wa fangasi.

Wednesday, August 2, 2017

Usafi Ni afya, imezoeleka Mara kwa Mara kutolewa mafunzo ya namna ya kuswafi uke lakini pasipo kusisitiza kuwa uume nao unapaswa kusafishwa ili kuweka hali ya usafi Na kuepusha mambo mengi ikiwapo magonjwa.

Kwako mwanaume Fanya hivi kusafisha uume wako.

Mgegedo ni tafsida nimeitumia kama kiwakilishi cha maumbile ya mwanaume yaani uume. Mgegedo ni eneo muhimu sana kwawanaume ambalo wanalitukuza kuliko kitu chochote hapa duniani, hivyo leo hiinimeona ni vyema kutoa darasa kwa wanaume ili wajue namna nzuri ya kutunza migegedoyao ili iwe misafi na yenye afya kwa ustawa wa mahusiano yao na wenzi wao.

Ni vyema wanaume wakajengautaratibu wa kuweka migegedo yao katika hali ya usafi unaostahili kwa ajili yakujenga mahusiano mazuri na wenzi wao inashauriwa kuosha mgegedo kwamakini kwa kutumia maji ya uvuguvugu kila siku mwanaume anapooga, kama mwanaumeatakuwa hajatahiriwa, basi anatakiwa kuigeuza ile ngozi inayofunika sehemu yambele ya mgegedo wake na kuisafisha kwa makini ili kuondoa ukando kando unaokuwaumeganda ndani unaofanana na jibini ambapo ukando kando huo hufahamikakitaalamu kama smegma.

Huu ukando kando unaopatikanandani ya migegedo ya wanaume wasiotahiriwa ni kilainishi maalum kinachoufanyamgegedo usiwe mkavu,kilainishi hiki ni cha kimaumbile.

Kama kilainishi hiki kikiachwabila kusafishwa kwa muda mrefu kitaanza kutoa harufu mbaya na baadayekitazalisha vijidudu (bacteria) ambavyo vitasababisha mgegedo kuvimba na kuwamwekundu sehemu ya mbele ambapo tatizo hilo hufahamika kitaamu kama balanitis.

Mwanaume asiyetahiriwa asiyesafishamgegedo wake vizuri licha ya kupatamatatizo niliyoyaeleza hapo juu lakini pia huweza kuharibu mahusiano yake namwenzi wake. Hakuna mwanamke ambaye atapenda kujinafasi kwa kulamba koni yamgegedo usio msafi, kwani ni kujitafutia fangasi za kinywa.

Hata hivyo ningependa kuwaonya kina mama kamwe wasijaribu kuigeuza ngozi ya migegedo ya watoto wao wadogo ambao hawajatahiriwa, kwani hiyo inaweza kuwaumiza na kuwasababishia maumivu makali. Kwa kawaida ngozi ya mbele ya migegegdo ya watoto wadogo inakuwaimeshikana na kichwa cha mgegedo hivyo haiwezi kuvutika yote na ukilazimisha unaweza kumjeruhi. Kwa watoto wadogo katika makuzi yao hawahitaji kusafishwa migegedo yao kwa namna hiyo. 

Lakini pia pamoja nakwamba usafi ni muhimu lakini haishauriwi kusafisha migegedo kwa kiwangokilichopitiliza kwa kutumia sabuni ya kipande au ya maji kunaweza kusababisha muwasho na uvimbe kwenye mgegedo hususani kwa wanaume wasiotahiriwa.Kwa kusafisha mgegedo mara mojakwa siku kwa maji ya uvuguvugu inasaidia kuiweka migegedo katika hali ya usafi kiafya. Na kama unataka kutumia sabuni, ni nyema kutumia sabuni zisizo za manukato yaani wengine huita sabuni mbuni au sabuni ya kipande. Kwa kutumia sabuni za manukato unaweza kusababisha muwasho na uvimbe wa ngozi wa mgegedo wako.

Usafi wa eneo la korodani za mgegedo

Kuzungumzia usafi wa mgegedo sikwamba nimesahau kuzungumzia usafi wasehemu ya chini ya mgegedo yaani korodani. Eneo la korodani lisipofanyiwa usafi makini lile jasho na nywele za chini husababisha harufu Fulani yenye kukera. Eeneo la korodani linatakiwa kufanyiwa usafi makini hasa kwa wale wanaovaa nguo za ndani muda wote kwa siku nzima. Ni vyema kuhakikisha eneo lachini la korodani karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa inakuwa safi wakatiwote ili isiwe na harufu isiyovutia.

Friday, July 28, 2017

Image result for tendo la ndoa baada ya kujifungua

kufurahia tendo baada ya kujifungua inategemea zaidi na wewe mwenyewe (uponaji wako)na lini unadhani uko tayari vilevile ushirikiano wa kutosha kutoka kwa mume/mpenzi wako wakati unaendelea na uponaji baada ya kutoa kiumbe kipya duniani.

Ni hali ya kawaida kabisa kwa mwanamke kutokujiskia (kutonyegeka) au kutaka ngono kwa wiki chache tangu ujifungue na hii inatokana na kusubiri dam ya uzazi kuisha bila kusahau yale maumivu kule ukeni (sore) kupungua au kupona kabisa.

Ili kufanikisha uponaji wa haraka inategemea na wewe mwenyewe utakavojisaidia na kufuata ushauri wa Wakunga na Daktari wako bila kusahau njia unayotumia "kusababisha" uponaji wa haraka.

Njia ambayo wanawake wengi wa kiafrika wanaitumia ni maji ya moto na utumiaji huu wa maji unatofautiana na hii inategemea na Asili yako (kule utokako) kwanikuna baadhi huongezea aina ya majani (kama dawa) ili kusaidia uponaji wa mama mzazi, wenginehuchanganya maji hayo ya moto na unga unaotokana na aina fulani ya mizizi nakadhalika......Afrika tuna madawa mengi asilia ambayo yanafanya kazi nzuri kabisa.

Katika kipindi hiki mwanamke hupaswi kuharakisha mambo, nikiwa na maana kuhisi “msukumo” wa kupona haraka ili ungonoke na mumeo kwa kuhofia kuwa atachepuka, pamoja na kusema hivyo ni vema kujitahidi na kuwa karibu zaidi na mumeo/mpenzi kimapenzi na kushirikiana nae.

Sio “kudeka” kwa vile tu umezaa (kuzaa ni sehemu ya uanamke hivyo usimfanye mumeo/mpenzi wako kujihisi “mkosaji kana kwamba  kukupa mimba ilikuwa kosa wakati mlielewana.).

Siku ya mwanzo kungonoka baada ya kupona kuna uwezekano mkubwa wa wewe kutopata raha au utamu na badala yake ikawa maumivu fulani hivi ambayo sio makubwa sana yaani kama yale upatayo unapokaa muda mrefu bila kufanya tendo la ndoa”.

Vilevile unaweza ukahitaji kilainisho cha kutosha na hapa sizungumzii mate bali K-Y Jelly ili kukabiliana na ukavu wa uke ambao unaweza kujitokeza ktk ya “game”.

Kwa kawaida uke hujirudi kama awali ndani ya siku Arobaini au Miezi mitatu yote inategemea na uponaji wako na njia uliyotumia ilikusababisha uponaji wako.

Licha ya kuwa “sore” na damu ya uzazi kukupotezea hamau ya kungonoka au kufanya mpenzi na mume/mpenzi wako pia kuna sababu nyingine zinazoweza kupelekea wewe mwanamke mzazi kushindwa au kupoteza hamu ya kungonoka na hivyo kumkwepa Jamaa kila atakapo mambo fulani.

Baadhi ya sababu hizo ni:-
- Uchovu wa mwili na akili kutokana na kutokupata usingizi wa kutosha mishughuliko yako kama mwanamke na vilevile mama
.
- Maumivu ya mshono kama ulijifungua kwa njia ya upasuaji, uliongezewa njia au ulichanika kutokana na ukubwa wa mtoto inategemea na pia atakavyokuwa akitoka.

- Kutokupata muda wa kuwa karibu na mpenzi/mume kutokana na mapenzi yako mazitokwa mtoto wako, yaani unahisi kuwa mtoto anakuhitaji zaidi kuliko baba’ke.

- Kupoteza hali ya kujiamini kwa vile unadhani kuwa mwili wako hauko kama ilivyokuwa baada ya kujifungua
Image result for maumivu wakati wa tendo la ndoa
HII ni hali ambayo mwanamke anakuwa na hamu ya kufanya tendo  la ndoa lakini anapata ugumu kutokana na maumivu makali anayopata.

Hali hii inatokana na kubana au kukaza kwa misuli ya uke lakini pia  inaweza kusababishwa na matatizo ukeni.

Mfano endapo kuna michubuko au vidonda au kasoro yoyote ya uke,  aidha uke ni mdogo au maumbile ya uke hayana uwiano na uume. Tatizo hili huwapata wanawake wa rika zote ilimradi tayari yupo katika  umri wa kuzaa.

TATIZO LINAVYOGAWANYIKA

Tatizo hili la maumivu wakati wa tendo la ndoa limegawanyika katika maeneo makuu mawili. Kwanza ni Primary Dyspareunia .

Hapa  mwanamke anakuwa hana historia ya maumivu wala  hana historia ya kuwahi kufanya tendo hilo ndiyo, kwanza anaanza. Kitaalamu hali hii ya maumivu huitwa Honey moon Dypareunia au maumivu ya fungate na hutokea mara tu anapoanza kujamiiana kwa mara ya kwanza. Katika hali hii misuli ya uke inaweza kubana kutokana na michubuko au kuchanika ubikira au hata kuchanika upande wa chini wa uke na wakati mwingine  michubuko hutokea katika tundu ya mkojo.Hali ya michubuko inaweza kuwa mbaya na ikajitokeza hata kwa kugusa tu upande wa nje wa uke.

Maumivu yakiendelea au yakizidi husababisha mgonjwa apate matatizo ya kisaikolojia kiasi kwamba huanza kuogopa tendo lenyewe na kuhisi endapo atalifanya ataumia. Tatizo hili likileta michubuko kwenye njia ya mkojo husababisha maambukizi sugu ya kibofu cha mkojo kutokana na michubuko ya mara kwa mara ya tundu ya mkojo.

Maumivu ukeni hutokana pia na maandalizi mabovu kabla ya tendo ambapo uke unakuwa haujalainika kwa kutofanya romance ya kutosha,  kutofanya tendo hilo kwa ustaarabu, yaani kutumia nguvu au endapo mwanamke atakuwa na maambukizi ukeni mfano fangasi ambayo huambatana na kutokwa na uchafu ukeni na muwasho, magonjwa ya uke kama kuvimba kwa tezi za uke, kuvimba kwa mashavu ya uke au hali yoyote inayomwondolea amani mwanamke pale ukeni inaweza kumfanya kisaikolojia aathirike na kuhisi maumivu wakati wa tendo.

Michubuko ukeni au kuhisi moto ukeni wakati wa tendo la ndoa kunaweza kusababishwa na matumizi ya vilainishi visivyofaa  au kuumwa kutokana na uwepo wa vinyweleo virefu ukeni na endapo havikupunguzwa vitaingia ukeni wakati wa tendo na kukuchubua.  Kasoro katika ubikira pia husababisha mwanamke ahisi maumivu wakati wa tendo.

Maumivu haya huwa hayahusiani na yale ya awali ya fungate na wakati mwingine huanza baada ya kipindi kirefu cha miaka

mingi tangu uanze tendo la ndoa na wengine huwa na tatizo hili tayari wana watoto. Chanzo cha tatizo hili ni ukavu ukeni, umri mkubwa wa mwanamke na kusinyaa kwa misuli ya uke.

Matatizo haya isipokuwa la umri mkubwa  hutokea katika umri wa kati na tayari mwanamke  anayo historia ya kuwa katika mahusiano na hata tayari ana watoto. Umri mkubwa tunaouzungumzia ni zaidi ya miaka hamsini. Kubana misuli ya ukeni hutokana na makovu baada ya kushonwa msamba au kuongezewa njia wakati wa kujifungua au upasuaji wa kurekebisha fistula pia husababisha tatizo hili.

Vyanzo vingine vya maumivu haya ya tendo la ndoa ni kushuka kwa kizazi ambapo mwanamke atahisi kitu kama gololi ukeni wakati  akijisafi sha au kuhisi kizazi kinasukumwa wakati wa tendo, kugeuka kwa kizazi, matatizo katika tabaka la ndani la kizazi, maambukizi sugu ukeni ambapo uchafu na muwasho ukeni hujirudiarudia, matatizo katika njia ya mkojo na maambukizi katika viungo vya uzazi ’PID’  husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Matitizo ya kisaikolojia husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa pale ambapo misuli ya ukeni itakaza na mwanamke anapochunguzwa huwa hana tatizo au kasoro yoyote ukeni. Matatizo katika mishipa ya fahamu ya ukeni, kuogopa tendo lenyewe kuhisi utapata maumivu au kama kuna historia ya kuingiliwa kwa nguvu na ukaumia, kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu tendo la kujamiiana, yote haya na mengine mengi humharibu mwanamke kisaikolojia na kujikuta anaanza kuhisi maumivu hata kabla ya tendo lenyewe kwa kuingiwa na hofu.

 Image result for maumivu wakati wa tendo la ndoa

Hali nyingine inayoweza kumfanya mwanamke aathirike kisaikolojia na asiwe tayari kwa tendo na hata akilifanya apate maumivu ni kuogopa kupata ujauzito wakati hayupo tayari kwa hilo, kuogopa kupata maambukizi, kulazimishwa penzi endapo haupo tayari na mwanaume uliye naye na kuhisi kuna tofauti ya maumbile na mume uliyenaye.

Endapo mwanaume anakukwaza kutokana na kutokwa na jasho jingi sana wakati wa tendo, kutoa harufu mbaya ya pua, kinywani, makwapani au sehemu zake za siri, huwa na magonjwa ya ngozi au hata mwilini mwake, matatizo haya huweza kumwathiri mwanamke kisaikolojia na asifurahie tendo na kutotoa ushirikiano wakati wa tendo na kupata maumivu.

UCHUNGUZI Tatizo hili ni pana sana, unaweza kuhisi una kasoro au maambukizi kumbe tofauti. Kwa hiyo basi ni vizuri uchunguzwe kwa umakini katika kliniki za madaktari wa akina mama katika hospitali za mikoa ili kujua chanzo halisi cha tatizo.
 Image result for ugumba

SABABU ZIPI ZINAZOLETA TATIZO LA UGUMBA (INFERTILITY)
Kwa wanawake - Tatizo la ugumba linaweza kutokea wakati wa Yai au kiumbe kilichomo ndani ya mfuko (uterus) wa uzazi kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto.

- Mayai yaliyo ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining)

- Matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa uzazi (uterus).

- Matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai (eggs).

 Image result for ugumba

TATIZO LA UGUMBA KWA WANAWAKE HUSABABISHWA NA

- Matatizo ya autoimmune disorders kama antiphospholipid syndrome (APS)
Kuwepo kwa cervical anti-gens ambazo huua mbegu za mwanamume ambazo husababisha mwanamke kutopata ujauzito.

- Matatizo katika uterus na shingo ya kizazi (cervix) kama vile uvimbe (fibroids or myomas) na birth defects

- Matatizo ya kuziba kwa mirija ya uzazi

- Mazoezi kupita kiasi (excessive exercise),
Afya iliyodhoofika (poor nutrition),
Matatizo ya kula (eating disoder).

- Baadhi ya madawa au sumu.

- Msongo wa mawazo (emotional stress)

- Tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal inbalance)

- Uzito uliopitiliza (obesity)

- Unywaji pombe kupindukia (heavy alcohol intake) –
Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari (diabetes)

- Magonjwa ya akina mama (Pelvic inflammatory disease PID) - Ovarian cysts and polycytic ovarian syndrome

- Magonjwa ya zinaa (sexually transmitted disease, STD) au endometriosis

-Saratani

- Uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk.

- Matatizo ya hedhi – wanawake wanaopata hedhi bila kutoa mayai (anovulatory menstrual cycle)
Hizo ni baadhi tu ya mambo yanayoweza kusababisha ugumba kwa akina mama.
Image result for ugumba

Thursday, July 27, 2017

Watafiti wanaochunguza matokeo yao tafiti 200 wanasema kuwa upungufu wa kiwango cha mbegu za kiume miongoni mwa Wanaume kutoka Marekani kaskazini, Ulaya, Australia na New Zealand ufikia nusu yake.

Baadhi ya wataalam wanashaka kuhusu matokeo hayo.

Lakini mtafiti bingwa anayeongoza utafiti huo Dkt Hagi Levine anasema kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kile kitakachofanyika katika siku za usoni.

Dkt. Levine ambaye ni mtaalamu wa magonjwa aliambia BBC kwamba iwapo mwenendo huo utaendelea basi huenda binadamu wakatoweka.

Utafiti huo ambao ni miongoni mwa tafiti kubwa ulileta matokeo ya tafiti 185 kati ya 1973 na 2011.

''Iwapo hatutabadili mienendo yetu ya kuishi mbali na kemikali na mazingira yetu ,nina wasiwasi mkubwa kuhusu kile kitakachofanyika siku za usoni''.

Hatimaye tutakuwa na tatizo hususan na uzazi kwa jumla na huenda ikawa kutoweka kwa binaadamu.

Wanasayansi ambao hawakushirikishwa katika utafiti huo wameusifu ubora wake lakini wanasema kuwa huenda ni mapema mno kutoa tangazo hilo.

Dkt. Levina kutoka chuo kikuu cha Hebrew mjini Jerusalem alibaini kupungua kwa asilimia 52.4 ya manii huku asilimia 59.3 ya mbegu za kiume kutoka kwa wanaume kutoka maeneo ya Marekani kaskazini, Ulaya, Australia na New Zealand yakishuka zaidi.

Monday, July 24, 2017


Furaha kubwa ya mama mja mzito ni kumzaa mtoto aliye na afya njema na asiye na shida yoyote. Lakini kwa akina mama wengi, furaha hii hukatizwa na unene wa tumbo unaokuja baada ya kujifungua.
Shida kubwa huwa ni tumbo ambalo ni nene kuuliko mwili. Sababu hii huwafanya akina mama wengine kutoupenda mwili wao.

jinsi ya kupunguza tumbo baada ya kujifungua. Iwapo watayafuatilia maagizo haya vikamlilifu, basi unene wa tumbo baada ya kujifungua utaisha.

1- Kuwa na motisha

Ni muhimu kwa mama kuwa na motisha anapoamua kulipunguza tumbo baada ya kujifungua. Tena, anafaa kuwa na uvumilivu. Kupunguza tumbo hilo huchukua muda sawia na ule wa kubeba mimba. Kwa ufupi, inawezekana kwamba kama tu ilivyochukua miezi tiza kwa tumo kunenepa, itachukua miezi sawia kupungua.
Hivyo basi, mama hafai kufa moyo au kuwa na haraka. Kuna uwezekano kwamba mama anaweza kufanya vitu ambavyo hakuzoea pale awali kama kufanya mazoezi, kuacha vyakula fulani na kuanza kuvila vingine. Hii ni safari inayohitaji motisha.

2- Kunyonyesha mtoto

Njia ya pili ya kupunguza tumbo ni kumnyonyesha mtoto. Ni asili kwa mwili wa mwanamke kurudia hali ya mbeleni pole pole baada ya kumzaa mtoto.
Kwa mfano, mfuko wa uzazi hurudia hali yake ya kawaida. Vile vile, iwapo watakua na subira na kuwanyonyesha wanao, basi tumbo hurudia ukubwa ule wa awali.

3- Kuepukana na pombe

Iwapo mama anakunywa pombe kwa wingi baada ya kujifungua, ni ngumu kwa tumbo kurudi ukubwa ule wa kawaida. Pombe, pamoja na vinywaji vyenye sukari nyingi, huadhiri njia ya ini ya kufanya kazi. Adhari mojawapo ni kutotengeneza misuli ifaavyo mwilini.
Ini linapolemewa kuunda misuli, mwili hujaa mafuta na kusababisha mtu kunenepa. Hivyo basi, mama anapokunywa pombe, sio tumbo tu linalonenepa; mwili wote huadhirika. Hivyo basi, unywaji wa pombe haufai baada ya kujifungua.

4- Kufanya mazoezi ya tumbo

Huenda ikawa vigumu kuanza mazoezi mara tu mama anapojifungua. Hivyo basi, ni vyema kusubiri mpaka mwili utakaporudia hali ya kawaida na kupata nguvu. Hata hivyo, mama hafai kufanya mazoezi mazito au mengi sana.
Kwahivyo, anza kwa mazoezi madogomadogo yanayolenga tumbo. Kwa mfano, unaweza kulala kwa mgongo na kuyakunja magoti. Baada ya hapo, unauinua mwili wa juu polepole kisha kulala tena. Rudia zoezi hili mara kadhaa kwa siku. Kuna mazoezi mengi ambayo utaelezwa na daktari.

5- Kutembea

Kutembea ni aina ya mazoezi ambayo husaidia kupunguza tumbo. Inawezekana kutembea kukaonekana kama mazoezi duni, lakini, husaidia sana kwa kulainisha tumbo.
Mtu anapotembea, misuli mingi mwilini hutumika, ikiwemo ile ya tumbo. Hivyo basi, mafuta yaliyokusanyika sehemu ya tumboni huisha na tumbo kupungua. Zoezi hili linaweza kukufaa sana iwapo utambeba mtoto wako mgongoni (kuongeza uzito).

6- Kufanyisha misuli mikubwa mazoezi

Hata ingawa lengo ni kupunguza tumbo, mama anafaa kuifanyisha misuli yote mazoezi. Unapofanya mazoezi yalengayo tumbo pekee, mafuta huchomeka polepole mwilini.
Iwapo unataka kulipunguza tumbo haraka, basi unaarifiwa kufanya mazoezi yalengayo misuli mikubwa mwilini. Hii ni kama miguu, mikono na mgongo. Hii itazuia kulipunguza tumbo na kubakia na mafuta (unene) kwingine mwilini.

7- Kupumua kwa undani

Zoezi hili ni rahisi sana na mama anaweza kulianza saa moja tu baada ya kujifungua. Mama anafaa kuketi kitako na kuvuta hewa kwa ndani.
Anapoivuta kwa ndani, anafaa kuukunjua mgongo na kasha kuifungia hewa ile kidogo tu. Kasha, anaitoa pumzi ile na kutulia kidogo, kasha kurudia. Zoezi hili husaidia misuli ya tumbo kulegeza na kumfanya kupona kwa haraka.

8- Kufunga kitambaa cha kupunguza tumbo

Hii ni njia mojawapo ya zile zinazotumika sana na ambayo imewkuwepo kwa muda mrefu. Muda mfupi baada ya kujifungua, kitambaa spesheli kilichotengenezwa kwa pamba hufungwa tumboni.
Lengo la kitambaa hicho ni kupunguza kufura na kuirudisha misuli kuwa na ukubwa wa kawaida. Kwa kawaida, kitambaa hicho hufungwa kwa muda wa wiki moja kasha mama anapumzika kiasi na kurudia tena. Kitambaa cha kawaida kilichoundwa kwa pamba kinaweza kutumika pia.

9- Kula chakula cha kutosha

Kadri na maelezo fulani kuwa mama akila kiasi atapunguza tumbo, ni bora kuzuia njaa kabisa. Kando na kutopunguza tumbo, njaa inaweza kuzuia kupona kwa haraka.
Mama anapokaa njaa kwa muda, kuna uwezekano kuwa atakula chakula kingi baadaye. Kula chakula kingi kutachangia kunenepa kwa tumbo.

10- Kula vyakula vidogo mara nyingi kwa siku

Badala ya kukaa njaa kwa muda kasha kula chakula kingi baadaye, ni heri kula vyakula vidogovidogo mara kadhaa kwa siku. Hii inawezesha mwili kusiaga chakula chote bila kuhifadhi cha ziada kama mafuta mwilini. Nguvu itokanayo na kula vyakula vidogovidogo hutumika kikamilifu na kuzuia kunenepa tumbo na mwili kwa jumla.

11- Punguza vyakula vya ‘kujituliza’

Kwa kawaida, mama anapojifungua, yeye hudaisha vitu kadhaa anavyohisi kwamba mwili unahitaji ili kuwa imara. Baadhi ya vitu hivyo ni chakula.
Shida ni kuwa, vingi vya vyakula hivyo huwa na sukari, mafuta na bidhaa zingine ambazo huongeza mafuta mwilini. Kwa mfano soda, keki, viazi, peremende na bidhaa zilizotengenezwa kwa ngano. Ni sawa kuvila vyakula hivi, lakini, vinafaa kupunguzwa muda uendavyo.

12- Kula vyakula vya mimea

Utafiti unaonyesha kuwa vyakula vya mimea (sio nyama) vina mafuta kidogo na madini mengi ya protini ya mboga. Hivyo basi, vinapunguza kuongezeka kwa mafuta mwilini na kuzuia kunenepa.
Akina mama wanahimizwa kujiepusha na kula nyama wakati huu na kula vyakula vitokanavyo na mimea.
Baadhi ya vyakula hivyo ni:
  • Mboga kama mchicha (spinach), sukuma wiki na kabichi.
  • Matunda kama machungwa, maembe, mapapai, tikitiki maji, parachichi, mapera na mengineyo.

13- Kupunguza kiasi cha chakula

Mama anakubalika kula chakula zaidi ya kawaida anapokuwa na mimba. Hii ni kwasababu ana binadamu mwingine ndani yake mwenye mahitaji mengi. Hata hivyo, baada ya kujifungua, anafaa kupunguza kiasi cha chakula alacho.
Kula chakula ziada kinalifanya tumbo kuwa nzito na kukusanya mafuta. Hii huchangia kwa tumbo kukaa likiwa nene au kuzidi kunenepa.

14- Kula kiamsha kinywa

Kiamsha kinywa ni mojawapo wa mlo muhimu sana kwa mama aliyejifungua. Anapokula kiamsha kinywa, mwili huchangamka na kusiaga chakula chote kikamilifu. Mwili pia hukaa tayari kuvipokea vyakula vingine wakati wa mchana na kuvisiaga vizuri.
Mwisho kabisa, hakuna uwezekano wa mama kuhisi njaa kupita kiasi na kuchangia kwake kula kupita kiasi. Kwa njia hii, tumbo la baada ya kujifungua hupungua.

15- Kunywa maji baridi ya kutosha

Maji husaidia mwili wa mama aliyejifungua kupona kwa haraka. Pili, maji hujaza tumbo na kuzuia mama kula chakula kingi kupita kiasi. Hivyo basi, anaweza kurejelea hali yake ya kawaida bila kuhisi njaa.
Kunywa maji baridi kutasaidia kuchoma mafuta mwilini wakat mwili unapojikakamua kuyapa joto. Hivyo basi, mafuta yanatolewa mwilini na tumbo kupungua.

Saturday, July 22, 2017

KUNA magonjwa mengi yanayosababisha mtu kukojoa udenda (usaha), uume kuuma au kuwasha wakati wa kukojoa.

Magonjwa yanayosababisha hali hiyo kwa sana ni pamoja na klamidia (chlamydia), kisonono (gonorrhea), trichomoniasis na magonjwa mengine yanayoathiri njia ya mkojo (nongonococcal urethritis)

Klamidia (Chlamydia)

Klamidia (Chlamydia) ni moja ya magonjwa ya zinaa. Ugonjwa huu unasababishwa na viini vya bakteria vwanaojulikana kitalaamu kama Chlamydia trachomatis na waweza kuathiri uke, mrija wa kupitisha mkojo, uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.

Klamidia (Chlamydia) ndio ugonjwa wa zinaa unaotokana na bakteria unaoongoza kwa maambukizi mengi zaidi duniani ukifuatiwa na ugonjwa wa kisonono (gonorrhea).

Ugonjwa wa klamidia (chlamydia) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiana. Ugonjwa huu ni wa hatari kwa sababu mama mjamzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.

Pia, kuchangia vifaa vya kuogea kama taulo vya mtu mwenye maambukizi, kuchangia vyoo vya kukaa na mtu mwenye maambukizi na kukumbatiana na mtu mwenye maaambukizi.

Vile vile ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kupitia mbawa, kupitia vinyesi vya ndege kama kuku, bata na kasuku walioambukizwa klamidia (chlamydia) inayopatikana kwa wanyama ijulikanayo kitaalamu kama Chlamydophila psittaci na kusababisha aina ya homa ya mapafu au homa ya kasuku (psittacosis).

Klamidia huathiri sehemu tofauti za mwili wa binadamu kama macho, mfumo wa upumuaji, sehemu za siri kama makalio, viungo vya uzazi na tezi (lymph nodes).

Huchukua siku 1-14 tangu maambukizi hadi kuonekana kwa dalili. Asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume wanaopata maambukizi ya ugonjwa huu huwa hawaonyeshi dalili za moja kwa moja.

Kwa wanaume, ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitishia mkojo, dalili kama vile uume kuwasha, kutokwa na ute na kusikia maumivu wakati wa kukojoa, sehemu ya tundu kwenye uume kuwa nyekundu, kuvimba na kuwasha pia kuhisi maumivu kwenye korodani na tezi zilizopo sehemu za siri ambazo huvimba na kuambatana na maumivu.

Dalili za ugonjwa huu kama umeathiri makalio (puru) kwa wanawake na wanaume ni kama kuwashwa na kutokwa na damu kwenye puru, maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa na kutokwa na uchafu kama kamasi kutoka kwenye puru.

Iwapo vimelea vya klamidia vitaathiri macho, wanawake na wanaume huwa na dalili kama kuvimba macho, macho kuwa mekundu, kuwasha na hata kutokwa na majimaji machoni.

Klamidia inayoambukiza kwenye macho hujulikana kitaalamu kama Chlamydia conjunctivitis au Trakoma (trachoma) na ndiyo inayoongoza kwa kusababisha upofu duniani.

Dalili za klamidia kwa watoto wachanga hutokea katika kipindi cha wiki mbili kwenye macho, na iwapo ni homa ya mapafu dalili zake hujitokeza katika kipindi cha wiki mbili hadi miezi 3 baada ya kuzaliwa.

Madhara ya ugonjwa huu kwa wanaume ni kuathiri korodani na kusababisha mwanamume kukosa uwezo wa kutengeneza mbegu za uzazi (manii/shahawa) au kuwa tasa na pia husababisha maambukizi kwenye tezi dume (prostatitis).

Kwa wanawake, husababisha maambukizi kwenye mirija ya uzazi, mfuko wa uzazi, na mayai ya uzazi, kwa hivyo kusababisha ugonjwa wa uvimbe katika fupanyonga (PID).

Pia huongeza uwezekano wa wanawake kupata mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancies).

Mwanamke hupata maumivu sugu kwenye nyonga na ugonjwa wa mifupa (arthritis) aina ya Reiters syndrome. Vilevile, klamidia huweza kusababisha ugumba kwa mwanamke kama hatapata tiba na kwa wanawake wajawazito, klamidia husababisha wajifungue kabla ya wakati wao.

Aidha, mtoto anaweza kuzaliwa na maambukizi kwenye masikio, sehemu za siri, macho na kwenye mapafu, yaani homa ya mapafu, na kama mtoto hatapatiwa tiba ya haraka ya macho baada ya kuzaliwa basi anaweza kuwa kipofu.

Kisonono (Gonorrhea)

Ugonjwa wa Kisonono (gonorrhea) husababishwa pia na bakteria waitwao kitalaamu Neisseria gonorrhoeae unapofanya mapenzi na mtu mwenye kisonono.

Ugonjwa huu unaweza kuaathiri viungo kama vile uke, uume, sehemu ya haja kubwa na ya haja ndogo, na hata koo au mdomo kama ukifanya mapenzi ya kunyonyana.

Wanaume huwa na dalili kama uume kutoa ute wa njano au kijani, na kupata maumivu wakati wa kukojoa (mkojo kuchoma).

Pia kuna uwezekano wa kuwashwa ama kutokwa na maji maji katika sehemu ya kupitishia haja kubwa. Ingawa hivyo baadhi ya watu hawaoni dalili zozote kabisa lakini bado wanaweza kuwaambukiza wanaofanya mapenzi nao.

Trichomoniasis

Ugonjwa wa Trichomoniasis unasababishwa na vimelea vya jamii ya protozoa vinavyojulikana kitalaamu kama Trichomonas vaginalis.

Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitisha mkojo (urethra) na tupu ya mwanamke (vagina). Huathiri sana wanawake kuliko wanaume na wanawake wenye umri mkubwa wako katika hatari zaidi kuliko mabinti wadogo.

Ugonjwa huu hupatikana kwa njia ya kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathirika na Trichomoniasis.

Dalili za Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4 mpaka ya 28 baada ya mtu kupata maambukizi. Wanaume huwa hawaonyeshi dalili zozote lakini baadhi wanaonyesha dalili kama kuwasha ndani ya uume, kutokwa na uchafu au majimaji kutoka kwenye uume, kuwasha au mkojo kuchoma wakati wa kukojoa au baada ya kutoa shahawa.

Mwanaume asipopata matibabu mapema huongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI na huongeza hatari ya kupata saratani ya tezi dume.

Magonjwa mengine ya njia ya mkojo

Magonjwa mengine yanayoathiri njia ya mkojo husababishwa na bakteria na huathiri mfereji wa kupitisha mkojo (urethra). Magonjwa hayo husambazwa kwa kujamiiana. Dalili kwa wanaume ni kutokwa na ute kwenye tundu la uume na huenda akahisi maumivu wakati wa kukojoa au akahisi maumivu na kuwashwa-washwa kwa pamoja.

Ikiwa unapata dalili isiyo ya kawaida ni busara kutafuta msaada wa kitabibu na siyo kusubiri mpaka hali inakuwa mbaya au kujinywea tu dawa bila ushauri wa daktari.

Njia sahihi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa ni kuacha, kuepuka kujamiiana au kufanya ngono zembe na sizizo salama.

Kwa wanawake wajawazito, ni vizuri kuhudhuria kliniki mapema wakati wa ujauzito na kupimwa vipimo mbalimbali ili kubaini ikiwa mama mjamzito ameambukizwa na ugonjwa wowote wa zinaa na kupatiwa matibabu mapema.

Kwa wale wenye maambukizi wanashauriwa kuchukua tahadhari ya kutowaambukiza wapenzi wao kwa kufanya ngono salama.

Thursday, July 20, 2017

AINA ZA UZIBAJI WA MIRIJA

Katika makala iliyopita Tuliona sababu kuu tatu zinazomfanya mwanamke asipate mimba. Kuziba kwa mirija ya uzazi huchukua asilimia ishirini ya tatizo la ugumba kwa mwanamke au mwanamke kupoteza uwezo wa kuzaa, pamoja na hizo sababu tatu, pia zipo sababu nyingine ndogo nyingine.

Aina za uzibaji; ni mirija kuziba upande wa mwishoni karibu na vifuko vya mayai Distal Tubal Occlusions.

Hali hii inahusiana kabisa na tatizo la mirija kuvimba au kujaa maji hali iitwayo kitaalam Hydrosalpinx ambapo pamoja na mwanamke kushindwa kupata mimba, pia husumbuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara yanayosambaa kulia na kushoto.

Hali ya kuvimba kwa mirija au mirija ya uzazi kujaa maji husababishwa na maambukizi ya vimelea vya Chlamydia Trachomatics.

Katika hali hii pia huweza kutokea hali ya kizazi na viungo jirani kushikamana hivyo mirija pia hushikwa na kuziba.

Hali hii ya kuziba mirija mwishoni husababisha sehemu ya mirija iliyo kama vidole iitwayo Fimbriae kugandamana na kusababisha kushindwa kuchukua yai lililopevuka na kuliingiza katika mirija tayari kwa kutungisha mimba.

Tatizo hili linapotokea, sehemu nyingine ya mirija inakuwa wazi au nzima. Mrija unaweza kuziba katikati Midsegment ambapo sababu kubwa inaweza kuwa mrija kufungwa au kukatwa kama njia ya kufunga uzazi.

Mrija unaweza kuziba mwanzoni na sababu kubwa ni maambukizi kwenye kizazi kutokana na utoaji au kuharibika mimba na maambukizi mengine sugu ya kizazi.

Toa maoni yako kuhusu ulichoelewa.

Wednesday, July 19, 2017

Kutokwa Na uchafu ukeni Ni sababu tosha itakayomfanya mwanamke asijisikie huru wakati wote!
Kuna sababu nyingi zinazopelekea tatizo hili kutokea;

Maambukizi katika uke ni tatizo la kawaida kwa wanawake na wanawake wengi wameshapata tatizo la maambukizi angalau mara moja katika maisha yao.

Ukiona yafuatayo, ujue unaweza kuwa na tatizo la maambukizi ya vijijidudu vya maradhi katika uke wako:

Kutokwa a uchafu ukeni kunakoambatana na kuwashwa au vijipele, kutokwa na uchafu ukeni ambako ni endelevu na kwa kiwango kinachozidi kila siku, kusikia maumivu wakati wa kutoa haja ndogo, kutokwa na uchafu mweupe, mzito kama jibini, uchafu wa kijivu/mweupe au njano/kijani unaotoa harufu mbaya.

 AINA YA UCHAFU USIO WA KAWAIDA

Kitu chochote kitakachoharibu uwiano wa bacteria wa kawaida waishio katika uke kinaweza

kuleta mabadiliko katika rangi, harufu au muundo wa uchafu utakaotoka katika uke.

Hapa chini naonyesha aina ya uchafu unaotoka, maana yake au chazo chake na dalili ambazo zitatokea kwenye mwili wa mwanamke husika:

 Uchafu wenye damu na rangi ya kahawia ni dalili ya mzungumko wa mwezi wa mwanamke uliovurugika na mara chache ni dalili ya kansa ya Cervix au aina nyingine ya kansa iitwayo Endometrial Cancer.

 Mwanamke mwenye tatizo hili atatoa damu nyingi ukeni na kuumwa nyonga.

 Mwanamke akitokwa na uchafu wenye rangi ya mawingu au njano hiyo ni dalili ya ugonjwa wa kisonono (Gonorrhea). Mwanamke atatokwa na damu katikati ya siku zake, atatokwa na mkojo bila kukusudia na kupata maumivu ya nyonga.

Mwanamke akitokwa na uchafu wa rangi ya kijani ikiambatana na harufu mbaya na ikiwa uchafu utatoka kama mapovu, wenye rangi ya kijani au njano ukiambatana na harufu mbaya, hii ni dalili ya Trichomoniasis, maambukizi (parasitic) yanayotokana na ngono zembe.

 Dalili nyigine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.

 Ukitoka uchafu mweupe mzito kama maziwa mtindi hiyo ni dalili ya maambukizi ya aina ya fungus (Yeast Infection) na dalili nyingine atakazozisikia mwanamke huyu ni kuvimba na maumivu kwenye sehemu za nje za siri (vulva) na kuwashwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Lakini uchafu ukiwa mweupe au kijivu wenye harufu kama ya samaki hiyo ni dalili za maambukizi ya Bacterial Vaginosis.

 Mwanamke mwenye tatizo hili atasikia miwasho au maumivu, kuvimba kwa uke au sehemu ya nje ya uke (vulva).

 Maambukizi ya Bacterial Vaginosis, Trichomoniasis na Monilia (Yeast) Infection nitachambua kwa ufupi kila moja na kueleza tiba yake.

 Bacterial Vaginosis: Kinachosababisha tatizo hili kitabibu hakifahamiki.

 Kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafl a kwa idadi ya bakteria hawa ambao ni kawaida kupatikana kwenye uke na kubadilisha uwiano wao kwenye mazingira ya uke.

 Wanawake wenye wapenzi wengi ambao hujamiiana nao au wanaofanya mapenzi kupitia midomo (oral sex) wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya Bacterial Vaginosis.
Dalili za Bacterial Vaginosis ni kuongezeka kwa uchafu unaotoka ukeni kama tulivyosema, kutokwa na uchafu wa kijivu/mweupe, mwepesi au wa majimaji, harufu kama ya samaki ikiambatana na uchafu na harufu inayozidi au uchafu unaozidi mara baada ya kufanya tendo la ndoa.

 TIBA YAKE

Tiba kwa tatizo la bacterial vaginosis zipo za aina mbili.

 Tiba ya aina ya kwanza ni kutumia dawa iitwayo metronidazole (Flagyl) na tiba ya pili ni kutumia dawa ya kuua bakteria (antibiotic) ya vidonge au ya cream.

 Trichomoniasis: Maambukizi haya hutokana na aina ya protozoa wa seli moja. Trichomoniasis mara nyingi huambukizwa kwa kufanya ngono. Protozoa huyu huweza kukaa kwenye mazingira ya unyevunyevu kwa muda wa saa 24 bila kufa hivyo kufanya taulo na nguo nyingine za kuogea kuwa chanzo kingine kikuu cha maambukizi.

Ukijiona Na tatizo Kama hili Ni vyema kwanza kumuona daktari kwa ushauri Na tiba zaidi.

Tuesday, July 18, 2017

Mimba kuharibika ni tukio linalopatikana mara nyingi katika wanawake na mamalia wa kike kutokana na shida mbalimbali katika ukuaji wa mimba tumboni mwa mama.

Ni tukio tofauti na utoaji mimba ambalo linasababishwa na binaadamu kwa makusudi.

Matukio yote mawili kwa kawaida yanaleta matatizo mbalimbali kwa mama.

Kuharibika kwa kijusi au kiinitete pengine kunatokana na mfadhaiko wa kiajali au sababu za kimaumbile. Mimba nyingi huharibika kutokana na kutonakiliwa kisahihi kwa kromosomu; pia huweza kuharibika kutokana na mazingira.

Mimba inayotamatika kabla ya wiki ya 37 katika kipindi cha ujauzito husababisha uzaaji wa mtoto na hujulikana kama kuzaliwa mapema

Kati ya 10% na 50% ya mimba hutamatishwa kwa njia zinazoweza kubainishwa kimatibabu, kutegemea umri na afya ya mwanamke mjamzito.

Mimba nyingi huharibika katika hatua za mapema sana za ujauzito, kiasi kwamba mwanamke hafahamu kwamba alikuwa mjamzito. Utafiti mmoja uliofanywa kupima homoni za kutoa yai na ujauzito uligundua kuwa 61.9% ya uhamili ulipotezwa kabla ya wiki 12, na 91.7% ya kuhabirika huko kulitokea bila ya dalili, na bila ya fahamu ya mwanamke aliyekuwa mjamzito. 

Hatari ya kutoka mimba ghafla hupungua kwa kiasi kikubwa baada ya wiki 10 kutoka kipindi cha mwisho cha hedhi. 

Kisababishi kikuu cha mimba kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza huwa matatizo ya kromosomu ya kiinitete / kijusi, hali ambayo husababisha angalau 50% ya kutoka kwa mimba mapema. 

Sababu nyingine ni pamoja na magonjwa ya mishipa kisukari, matatizo mengine ya homoni, maambukizi, na matatizo ya chupa ya uzazi. 

Umri mkubwa na historia ya mimba zilizotangulia kuharibika ni sababu mbili kuu zinazohusishwa kwa pakubwa na mimba kuharibika ghafla. 

Hiyo inaweza pia kusababishwa na kiwewe kinachotokana na ajali.

Monday, July 17, 2017

Dalili

Mjamzito mwenye upungufu wa damu wa kawaida mara nyingi anaweza asioneshe dalili zozote.

Hata hivyo iwapo upungufu ni mkubwa, dalili za awali ni pamoja na uchovu wa mara kwa mara na kupumua kwa shida, kukosa hamu ya kula, mapigo ya moyo kwenda kasi, na kuchafuka kwa tumbo

Wakati wa uchunguzi mjamzito anaweza kuonekana mweupe kuliko kawaida hasa sehemu za viganjani, kucha za vidoleni, ulimi, au macho.

Anaweza pia kuwa na dalili za kuvimba miguu.

Vipimo na uchunguzi

Uchunguzi wa upungufu Wa damu hufanywa kwa kupima kiasi chahaemoglobin pamoja kufanya kipimo kingine cha damu kijulikanacho kama peripheral smear

Vipimo vingine vya maabara ni pamoja na kipimo cha kufahamu uwezo wa kuhifadhi madini ya chuma yaani total iron binding capacity (TIBC), kiasi chaferitinkatika damu, kiasi cha folic acid.

Katika mazingira mengine kipimo cha kuchukua sehemu ya supu ya mifupa na kuichunguza maabara yaani bone marrow biopsykinaweza kufanywa.

Hata hivyo hivi si vipimo vinavyofanywa mara kwa mara.

Matibabu

Mama mjamzito huitaji miligramu 2 mpaka 4.8 za madini ya chuma kila siku.
Ili aweze kupata kiasi hiki, inampasa kula kati ya miligramu 20 mpaka 48 za madini ya chuma.

Kwa jamii ambayo upatikanaji wa vyakula vyenye madini hayo ni wa shida, suala hili linaweza kuwa gumu sana kutekelezeka, ndiyo maana Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweka mpango maalum wa kuwapa wajawazito wanaohudhuria kliniki madini ya chuma na folic acid ili kufidia pengo hilo

Vidonge vya madini ya chuma ni salama, nafuu na njia makini ya kuongeza na kurekebisha upungufu wa damu mwilini.

Kwa wajawazito ambao hawawezi kunywa, kwa sababu yeyote ile, njia ya sindano inaweza pia kutumika

Wajawazito wanashauriwa kutumia miligramu 60 za madini ya chuma(ferrous sulphate) na 500mg za folic acid kila siku, ambapo utaratibu huu huendelea kwa miezi mitatu mpaka sita ili kuongeza hifadhi ya madini ya chuma mwilini, hata kama kiwango kinachotakiwa kitakuwa kimefikiwa.

Utumiaji wa vidonge vya madini ya chuma na baadhi ya vyakula: 

Kuna baadhi ya vyakula kama vile chai ya rangi ambavyo vikiliwa wakati mjamzito amekunywa vidonge vya madini ya chuma vinaweza kupunguza unyonyaji wake katika utumbo.

Kwa upande mwingine baadhi ya vyakula vyenye vitamini C kama vile matunda ya jamii ya machungwa huongeza uwezo wa utumbo kunyonya madini ya chuma mwilini

Vyakula vya kuongeza damu:

Pamoja na mkakati huo, wajawazito hushauriwa pia kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kama vile nyama, maini, mayai, samaki, mimea jamii ya kunde, maharage makavu, mboga za majani, matembele, na mikate iliyoongezwa madini ya chuma.

Matibabu ya upungufu wa damu mkali kwa wajawazito walio katika wiki za mwisho (baada ya wiki ya 32): 

Wagonjwa wa kundi hili hutibiwa hospitali. Wengi wanaweza pia kuwa na dalili za matatizo ya moyo, hivyo wanapaswa kulazwa na kupumzika kitandani, na wakati fulani kuongezewa hewa ya oksijeni.

Pamoja na kutibiwa matatizo ya moyo, huongezewa pia damu (packed red cells) kwa vile vidonge vya madini ya chuma havitafaa kurekebisha tatizo hili kwa haraka kabla ya muda wa kujifungua kufika

Matibabu ya maradhi mengine: 

kwa mazingira yetu, magonjwa kama malaria na minyoo huchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa upungufu wa damu kwa wajawazito, hivyo basi magonjwa haya hayana budi kutibiwa kikamilifu ili yasilete madhara kwa mjamzito.

Wajawazito wanaoishi maeneo yenye malaria kwa wingi hupewa dawa za SP kwa ajili ya kuwalinda wasipatwe na ugonjwa huu.

Pia dawa za minyoo za Albendazole au mebendazole hutolewa kwa wajawazito baada ya miezi mitatu ya mwanzo ili kuua minyoo.
Ili kuzuia kujiridia kwa minyoo, wajawazito pia hushauriwa kuvaa viatu/kandambili kila wakati, na kuhakikisha miili na mazingira yao yapo safi.

Ni muhimu kwa mama mjamzito kuhudhuria clinic Mara tu baada ya kujigundua ni mjamzito ili aweze kupewa ushauri Na msaada Wa kuweza kulea mimba vyema.

Saturday, July 15, 2017


baadhi ya watoto kwenye jamii zetu huzaliwa na mtindio wa ubongo yaani utakuta wazazi wanagundua kama mtoto hana akili nzuri au hawezi kufanya vitu fulani kama wenzake akishakua mtu mzima kabisa. mfano kushindwa kuongea, kutokwa mate mdomoni muda wote, kushindwa kutembea na kadhalika...kuna mambo mengi yanachangia kuzaliwa kwa watoto wa aina hii ikiwemo kuzaa umri mkubwa kwa wanawake,pombe na sigara kipindi cha ujauzito, magonjwa ya akili ya kurithi, matatizo yanayotokea katika ukuaji tumboni na kadhalika. leo tutaangalia njia kuu tano za kugundua kama mtoto wako ana akili nzuri na hana shida ya mtindio wa ubongo baada ya kuzaliwa.yani jinsi ya kumgundua kwa njia za kitaalamu kama ifuatavyo.

kushika kitu; hii huwepo mtoto anapozaliwa mpaka kufikisha miezi sita au saba, mtoto kipindi hiki ukimpa kitu chochote mfano kalamu lazima atakamata kwa nguvu bila kuachia lakini mtoto mwenye tatizo ukimpa kitu hataweza kushika na atabaki anakushangaa tu.

kujaribu kutembea; dalili hii huonekana utotoni wakati wa kuzaliwa lakini lakini hua haina nguvu sana mpaka mtoto afikishe miezi sita mpaka mwaka mmoja. kipindi hiki ukimshika mtoto kama unataka kumtembeza atapiga hatua mwenyewe, hii ni dalili njema.

kunyonya; wakati wa kuzaliwa mtoto akipewa ziwa la mama ananyonya mwenyewe bila kufundishwa kabisa, ikitokea mtoto anashindwa kunyonya siku ya kuzaliwa basi inawezekana anaumwa au ana mtindio wa ubongo na anashindwa kugundua vitu hivyo.

parachute; hii hutokea hasa kwa watoto wenye angalau miezi sita mpaka mwaka mmoja, ukimbeba moto huyu afu ukamgeuza kichwa chini miguu juu kama unataka kumuangusha atanyoosha mikono kama anataka kuzuia ule muanguko.hii inaonyesha kwamba mtoto ni mzima.

rooting; hii hutokea mtoto anapozaliwa mpaka miezi sita yaani kipindi hiki mtoto ukimgusa na kitu chochote kwenye shavu atageuka kufuata kitu hicho na mdomo akidhani labda ni ziwa la mama ili anyonye.dalili hii ni dalili nzuri na huonyesha kwamba mtoto ni mzima.
                                                        Mara uonapo dalili hizi mapema ni vyema ukajaribu kuwaona wataalamu Wa afya ili kuweza kubaini tatizo.                   

Uwezo wa kufikiri wa kizazi fulani, unaweza kuathiriwa na hali na changamoto wanazopitia wanawake wajawazito katika hatua za kushiriki uumbaji wa mwana aliye ndani ya tumbo lao kwa muda wa miezi tisa.

Mwanamke mjamzito anayekabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo kutokana na sababu zozote, huweza kuleta athari ya moja kwa moja kwenye mfumo wa ukuaji wa ubongo wa mwanae.

Hayo yamedhihirika kupitia utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Clinical Endocrinology, ambao ulionesha kuwa athari hizo zinaweza kupatikana kwa ujauzito wenye umri wa kuanzia wiki 17.

Utafiti huo ulikuja kama muendelezo wa tafiti za awali kwa binadamu na wanyama ambazo zilionesha kuwa endapo mama mjamzito atakabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo, anaweza kusababisha mwanae akawa na uwezo mdogo wa kufikiri (IQ).

Hata hivyo, watafiti hao walieleza kuwa lengo lao sio kuwapa hofu wanawake bali ni kuwatahadharisha kuhakikisha wanakuwa na afya nzuri na kuepuka mambo yanayoweza kusababisha msongo wa mawazo.

Timu ya watafiti ikiongozwa na Professa Vivette Glover wa Chuo cha Imperial cha London (Imperial College London) na wasaidizi wake ambao ni wataalam wabobezi wa afya ya mama na mtoto waliwafanyia utafiti wanawake wajawazito 267 kwa kutumia dawa maalum zinazompa mtu hali sawa na ile ya aliye na msongo wa mawazo.

Profesa Glover alisema kuwa walitoa dawa hizo kwa kuzingatia hali inayoweza kumpata mtu mwenye msongo wa mawazo wa muda mrefu ambayo ni kuchoka sana na kujisikia mgonjwa.

Hivyo, ni vyema kwa jamii kuhakikisha kuwa ili kuendela kuwa na kizazi chenye uwezo mkubwa wa kufikiria na kuamua mambo, ni vyema tukaanza na kuwajali na kuwapa furaha wanawake wajawazito.

Changamoto wanazozipitia katika ngazi za familia zinaweza kuwa chanzo cha kukosa mwana mwenye uwezo wa kuliinua Taifa.

Tuesday, July 11, 2017

Ulaji wa mara kwa mara wa viazi, bila kujali kama ni vya kuchemshwa au vya kukaangwa ama chips, unaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito, wameeleza watafiti wa Marekani.

Hii labda ni kwa sababu wanga uliomo katika viazi unaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya sukari zaidi, wanasema.
Utafiti wao ulihusisha wanawake wajawazito zaidi ya 21,000.

Lakini watafiti wa Uingereza wanasema ushahidi huo una mapungufu na kuongeza kuwa watu wengi wanahitaji kula zaidi vya wanga ili kupata nyuzi nyuzi, pamoja na matunda na mboga

Utafiti huo wa BMJ unahusu ulaji wa viazi hadi kiwango cha kuwa na uwezekano wa hatari ya kuugua kisukari

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR