Showing posts with label dondoo. Show all posts
Showing posts with label dondoo. Show all posts

Friday, September 29, 2017

 Image result for KUZOROTA AFYA YA MTOTO

Kuna imani imekuwa ikijitokeza kwamba kufanya mapenzi kipindi wakati mtoto angali ananyonya ndio hupelekea hali ya mtoto kuwa mbaya huku ikifahamika kama KUBEMENDA lakini katika hali halisi hii si kweli kabisa kwani kuzorota kwa afaya ya mtoto husababishwa na mambo yafuatayo.

  • Kukosa maziwa ya mama ya kutosha

  • Mtoto kushindwa kunyonya vizuri

  • Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.

  • Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.

  • Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.

  • Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).

    KAMA MZAZI IANAKUPASA KUMJUA NA KUMCHUNGUZA MTOTO WAKO KILA WAKATI ILI KUWEZA KUBAINI TATIZO LIKO SEHEMU IPI NA UWEZE KUMTIBIA MAPEMA.

Tuesday, September 5, 2017

Utamaduni wa Tanzania unapendekeza wanawake kuvaa nguo kubwa, zilizopwaya wakati wa ujauzito. Kama vile hawana haja ya kupendeza wakiwa wajawazito. Bahati nzuri, kuna maduka mengi zenye mavazi mazuri za wakati wa ujauzito.
Image result for mavazi ya mama mjamzito
Ila bado kuna wanawake wengi wanaoamua kutojali muonekano wao wakiwa wajawazito. Sasa, kwa wao, vidokezo vifuatayo vitakusaidia kuvaa ukiwa mjauzito.

1. Kubali umbo lako
Hamna haja ya kuficha ujauzito wako. Ila hatusema kwamba uvae blauzi inayobana na kimini (ila, unaweza kuvaa hivyo ukipenda). Tunachopendekeza hapa ni kuvaa nguo zinazotosha umbo lako.Tumbo lako likianza kujitokeza, nunua nguo kama gauni, jinzi na topu zinazo ruhusu hewa kupita; hizi zitakuwezesha kuonyesha figure yako kwa kistaarabu.

2. Usibadilishe mtindo wako wa kawaida
Kwa kuwa we ni mjazmzito haimaanisha kwamba inabidi ubadilishe mtindo wako wa kipekee.
Kwa hiyo, kama ulikuwa unapenda gauni, endelea kuvaa gauni. Hakikisha inatosha umbo lako tu.

3. Tumia vifaa vya mitindo
Scafu, bangili, ereni n.k zitasaidia kuboresha vazi lako kwa ujumla na zitakusaidia kujiamini pia. Kwa mfano, kama unawasiwasi na tumbo lako lilivyojitokeza, vaa mkufu au ereni safi zitakazo fanya watu waangalie sura badala ya tumbo yako.

4. Nunua Jinzi safi kwa ajili ya ujauzito
Nunua jinzi zenye uwezo wa kupanuka ndio zitakazokufaa. Zinaweza zikawa za kubana au zenye nafasi zaidi, cha muhimu nikwambai unajisikia vizuri ukizivaa.

5. Nunua gauni ya kufunga (Wrap Dress)
Wrap Dress zinafaa kwa umbo yoyote ile na zinapendeza sana! Pia ni rahisi kuzivaa na kutembea ndani yao ukiwa umezivaa.
 
6. Nunua nguo zenye rangi kali
Rangi kali kama njano na rangi ya machungwa (orange) zinaonyesha ile mwanga asili ambao wajawazito huwa wanao. Kwa hiyo, kuvaa gauni yenye rangi kali inaweza ikampa mjamzito mng’ao wa kirembo.

Onekana vizuri zaidi ya unavyojisikia
Kuwa mjamzito ni wakati muhimu katika maisha ya mwanamke na kwa kuwa hutajisikia vizuri kila siku ya ujazito wako, unaweza kuendelea kupendeza na kutafuta nguo zitakazoipendza mwili wako.
Image result for mavazi ya mama mjamzito

Saturday, August 5, 2017

Hivi ni baadi ya vyakula ambavyo mama mjamzito au mwanamke anaejiandaa kubeba ujauzito HARUHUSIWI kuvitumia katika kipindi cha ujauzito.

*Nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri, nyama za aina hii husemekana kuwa na bacteria ambao huwezakusababisha ujauzito kutoka au kuzaa mtoto mwenye ulemavu wa kuzaliwa

*Maziwa ya mgando au maziwa ambayo hayajachemshwa, maziwa ya aina hii husemekana kuwa na bacteria ambao wanaweza hatarisha maendeleo ya ujauzito

*Vinywaji vyenye caffeine kama vile kahawa, chai, coca cola na vingine vya asili hiyoMayai mabichi, husemekana kuwa na bacteria wanaoweza kuhatarisha maendeleo ya ujauzito.

*Samaki wabichi wa maji chumvi au samaki waliovuliwa kwa kutumia sumu.

*Vyakula laini na vyenye sukari nyingi kama soft cheeses, cake, chocolate n.k.

*Unywaji wa pombe

*Kula mboga za majani au matunda bila kuyaosha

*Ulaji wa maini
Katika kipindi cha ujauzito au katika maandalizi ya kubeba ujauzito mwanamke anatakiwa kula vyakula vya aina mbalimbali vilivyoandaliwa vizuri na kupikwa vikaiva inavyotakiwa, ulaji wa vyakula mbalimbali katika makundi ya vyakula kabla ya ujauzito au katika kipindi cha ujauzito husaidia kuupa mwili na mtoto virutubisho mbalimbali vilivyo na umuhimu katika kujenga na kulinda mwili.

Zingatia upate mafanikio bora.

Thursday, August 3, 2017

fahamu kuhusu fistula

Fistula ni nini
Fistula ni shimo ambalo hutokea kati kati ya kibofu cha mkojo na uke au kati kati ya njia ya haja kubwa na uke wa mwanamke ambaye amejifungua kwa shida. Shimo hutokea pale ambapo kichwa cha mtoto ni kikubwa kuliko njia ya uzazi.

Ina sababishwa na nini?
Inasababishwa na  kusukuma mtoto wakati wa kujifungua kwa mda mrefu bila usaidizi au matibabu yeyote, na ana chanika  katika njia ya uzazi na kusababisha shimo, hivyo husababisha uvujaji wa kinyesi na mkojo bila kujizuia. 
Kuzaa mapema kabla ya umri kumekuwa chanzo kikubwa cha kutokea fistula, hilo linatokana na kutopevuka kwa njia za uzazi pamoja na nyonga.

 Kwenda Kliniki
Wataalamu wa afya wanabaini fistula mara nyingi hutokea kwa wanawake wanaojifunglia majumbani baada ya kukosa matibabu. Ni Sahihi mara kwa mara kwa wajawazito kujifungua katika kituo cha matibabu ambapo unaweza kufuatiliwa na kupata huduma za matibabu kwa wakati ni muhimu

.Nifanye nini ikiwa nina fistula?

Kama unahisi kutokwa na mkojo bila kujizuia, harufu mbaya, maumivu makali sahemu za uzazi unashauliwa kuwahi hospitali au kituo cha afya kilipo karibu ili upate ushauri na matibabu zaidi,

Matibabu

Matibabu ya fistula ni bure katika hospitali zote nchini.

Wednesday, July 19, 2017

HILI ni tatizo linalosababisha ugumba kwa wanawake kwa kiasi kikubwa. Wanawake wanaoshindwa kupata ujauzito hukabiliwa na matatizo matatu;

* kwanza kabisa ni kuziba kwa mirija ya mayai kama tutakavyoona leo

* matatizo katika mfumo wa homoni ambapo kuna sababu zake tutakuja kuziona katika matoleo yajayo.

* dalili kuu ni kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi, kutopata hedhi na kupata damu kwa muda mrefu au muda mfupi sana ambazo ni siku moja au mbili.

* Dalili nyingine ambazo siyo nzuri katika mfumo wa homoni ambazo zinaweza kufanya mwanamke asipate mimba ni matiti kutoa maziwa wakati siyo mjamzito na wala hana mtoto anayenyonya.

* Tatizo la tatu ni kwa upande wa mwanaume kutokuwa na mbegu zenye ubora.

Yaani hana nguvu za kutosha au anawahi kumaliza tendo la ndoa Premature Ejaculation.

* Kuziba mirija ya uzazi huzuia mbegu na mayai kukutana na kutungisha mimba. Mirija ya uzazi pia huitwa Oviducts, Uterine Tubes au Salpinges

Wakati ujao tutatazamia aina za uzibaji Wa mirija ya uzazi.

Monday, July 17, 2017

Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu.
Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mama na mtoto ikiwemo kifo.

Madhara haya ni pamoja na Madhara kwa mama kipindi cha ujauzito:

kukonda au kuongezeka uzito kwa kiasi kidogo sana,

kuhisi uchungu kabla ya muda,

kondo la nyuma kutunga pasipostahili,

shinikizo la damu wakati wa ujauzito, na chupa kupasuka kabla ya wakati.

Madhara kwa mama wakati wa kujifungua:

kupatwa na uchungu usioeleweka na usio wa kawaida,

mtoto kuvuja damu ndani kwa ndani,

kupatwa na shock, hatari ya ganzi (anesthesia risk) kwa anayefanyiwa upasuaji,

moyo kushindwa kufanya kazi.

Madhara kwa mama baada ya kujifungua:

maambukizi baada ya kujifungua,

kizazi kushindwa kurudi katika hali ya kawaida au damu kuganda kwenye mishipa.

Madhara kwa mimba na mtoto atakayezaliwa:

Madhara ni pamoja na mtoto kuzaliwa njiti,

mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,

mtoto kuwa na score ndogo (poor Apgar score), 

mtoto kuzaliwa akiwa amechoka (fetal distress),

Upungufu wa damu kwa mtoto, Watoto wanaozaliwa wakiwa na upungufu wa damu hukua kwa tabu, huwa na maendeleo duni ya kiakili na kimatendo (poorer intellectual developmental milestones),

uwezekano mkubwa wa kuwa na kasoro mwilini na hata kifo.

Kasoro hizo ni pamoja na matatizo ya magonjwa ya moyo yakuzaliwa nayo.

Kila mama mjamzito anapaswa kuwa makini katika kipindi cha ujauzito ili kuepusha madhara haya.

Sunday, July 16, 2017

Historia ya ugumu wa kula, au mtoto hawezi kula kwa sasa.

Historia ya mitukutiko, au mtoto anatukutika kwa sasa.

Mtoto mchanga anaonekana mlegevu au amepoteza fahamu.

Mtoto anasonga tu iwapo amesisimuliwa.

Kupumua kwa haraka.

Kifua kubonyea ndani sana.

Homa.

Hipothemia (ukimguza, unahisi kuwa mtoto ana baridi).

Mtoto amekuwa na rangi ya manjano kabla ya kufikisha umri wa saa 24.

Umanjano unaoonekana kwenye viganja vya mikono na nyayo za miguu.

Macho yamefura au yanatoa mchozo.

Usaha unatoka kitovuni.

Zaidi ya pustuli (madoa) 10 zinaonekana ngozini.

Hizi ni dalili za hatari kwa mtoto yeyote mchanga, mama ukiona dalili hizi muone daktari mapema.

Wakina mama wengi wenye watoto wachanga hawana kawaida ya kunawa mikono Mara kwa Mara watakapo kumuhudumia mtoto.

Yakupasa kunawa mikono kila Mara kwa kufuata utaratibu huu;

*Kabla ya kunyonyesha

*Kabla ya kumvisha au kumvua mtoto nguo.

*Kabla ya kumsafisha au kumwosha mtoto.

*Baada ya kumbadilisha mtoto nepi na kutupa kinyesi.

*Baada ya mama kubadilisha padi zake mwenyewe zinazotumika kufyonzea mchozo wa damu kutoka ukeni.

*Baada ya kutumia choo.

*Kabla au baada ya kuandaa chakula.

Kwa kufanya hivi itakuhakikishia hali ya usalama Wa afya ya mtoto wako.

Monday, July 10, 2017

Lishe wakati wa ujauzito ni muhimu kwa ajili ya afya yako na maendeleo mazuri ya mtoto anayekua tumboni.

FUATA MLOLONGO HUU KUWA NA LISHE BORA;

1.Jitahidi upate mlo kamili kila siku kwa kupata vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji ya kutosha.Fanya nusu ya mlo wako uwe ni mchanganyiko wa matunda na mboga za majani.

2.Tumia nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona au mtama, mchele usiokobolewa, mikate ya brown au whole grain cereals.

3.Tumia maziwa yenye fafi kidogo( skimmed milk) au maziwa na vinywaji vya soya.

4.Chagua vyanzo vyako vya protini zaidi katika samaki, kuku, mayai, jamii ya maharage, soya na karanga.

5.Tumia zaidi mafuta ya mimea katika mapishi yako kama mafuta ya alizeti, pamba au mizeituni (Olive oil).

6.Punguza vyakula vyenye sukari za kuongeza (hasa artificial sugars) na mafuta kama biskuti, pipi, soft drinks, soda, pipi, ice creams, vyakula vya kukaanga na hot dogs.Kunywa maji mengi, zisipungue lita 2.5 kwa siku.

7.Mazoezi mepesi kama kutembea kwa dakika 30 kwa siku.Epuka matumizi ya pombe kwani yataathiri afya ya mtoto wako.

8.Tumia virutubisho ziada (supplements) utakazopata kliniki.

WAWEZA ACHA MAONI YAKO HAPA.

Monday, July 3, 2017

Uvimbe kwenye mfuko wa kizazi na sehemu nyingine mwilini imekuwa ni janga kubwa hususani kwa wanawake.Hasara za uvimbe kwenye mfuko wa kizazi.

1.Seli hasi za kwenye uvimbe zinakua haraka kuliko mtoto kwani huchukua virutubisho vyote muhimu zaidi ya mtoto hivyo husababisha mtoto kufa akiwa tumboni au kutoka kwa mimba.

2.Kwa wanaofanikiwa kukaa hadi mwishoni mwa mimba hulazimika kufanyiwa upasuaji ili kuokoa mtoto.

3.Kutokushika ujauzito kabisa.

4.Maumivu makali wakati wa hedhi,

5.maumivu makali wakati Wa tendo la ndoa.

Endelea kutembelea blog hii kwa taarifa zaidi.

Friday, June 30, 2017

Monday, June 26, 2017



1..kupata mda wa kucheza na wazazi
2.lishe boraa
3.kupewa maamuzi zaidi
4.marafiki wa lika la lengo moja
5. wazazi kutompa mda wa kuwa na huzuni  na..........................

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR