Thursday, June 29, 2017

Wanawake wanaokula udongo wakiwa wajiwazito wamo katika hatari ya kuwafanya watoto watakowajifungua kutofanya vizuri shuleni.

Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa watoto ambao kina mama wao walikuwa wakitumia udongo hawakomakiniki darasani.

Kwa kawaida wanawake wengi hutumia udongo huo baadhi wakidai kuwa wana upungufu wa madini ila wengi wao huzidisha matumizi yake.

Zaidi ya wazazi 4000 walihusishwa katika utafiti huo lakini ni 1000 tu ambao maoni yao yalitumika kuandaa ripoti ya utafiti huo.

Taasisi hiyo ilikuwa ikifuatilia matokeo ya watoto hao wakiwa shuleni kwa muda wa miaka minne na wakatambua kuwa wale ambao hawakuwa imara darasani mama zao walikuwa na historia ya kutumia udongo wakiwa wamebeba mimba zao.

Watafiti hao wanasema kuwa kutokana na hayo ubongo wa watoto waliozaliwa huchelewa kushika mambo.

Kadhalika utafiti huo unaonyesha kuwa wanawake katika miaka ya ishirini huwa na hamu kubwa kutumia udongo.

Nini maoni yako juu ya matumizi ya udongo kwa wajawazito!?

Related Posts:

  • ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MTOTO MCHANGAHistoria ya ugumu wa kula, au mtoto hawezi kula kwa sasa. Historia ya mitukutiko, au mtoto anatukutika kwa sasa. Mtoto mchanga anaonekana mlegevu au amepoteza fahamu. Mtoto anasonga tu iwapo amesisimuliwa. Kupumua kwa haraka… Read More
  • KUNAWA MIKONO NI AFYA.Wakina mama wengi wenye watoto wachanga hawana kawaida ya kunawa mikono Mara kwa Mara watakapo kumuhudumia mtoto. Yakupasa kunawa mikono kila Mara kwa kufuata utaratibu huu; *Kabla ya kunyonyesha *Kabla ya kumvisha au kumvua … Read More
  • MADHARA YA UPUNGUFU WA DAMU KWA MJAMZITOSehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mama na mtoto iki… Read More
  • MSONGO WA MAWAZO KWA MJAMZITO HUPELEKEA UPUNGUFU WA AKILI KWA MTOTO ATAKAYEZALIWA.Uwezo wa kufikiri wa kizazi fulani, unaweza kuathiriwa na hali na changamoto wanazopitia wanawake wajawazito katika hatua za kushiriki uumbaji wa mwana aliye ndani ya tumbo lao kwa muda wa miezi tisa. Mwanamke mjamzito anayek… Read More
  • ZIFAHAMU DALILI ZA MTOTO MWENYE MTINDIO WA UBONGO. baadhi ya watoto kwenye jamii zetu huzaliwa na mtindio wa ubongo yaani utakuta wazazi wanagundua kama mtoto hana akili nzuri au hawezi kufanya vitu fulani kama wenzake akishakua mtu mzima kabisa. mfano kushindwa kuongea, kut… Read More

0 comments:

Post a Comment

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR