Saturday, July 15, 2017

Uwezo wa kufikiri wa kizazi fulani, unaweza kuathiriwa na hali na changamoto wanazopitia wanawake wajawazito katika hatua za kushiriki uumbaji wa mwana aliye ndani ya tumbo lao kwa muda wa miezi tisa.

Mwanamke mjamzito anayekabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo kutokana na sababu zozote, huweza kuleta athari ya moja kwa moja kwenye mfumo wa ukuaji wa ubongo wa mwanae.

Hayo yamedhihirika kupitia utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Clinical Endocrinology, ambao ulionesha kuwa athari hizo zinaweza kupatikana kwa ujauzito wenye umri wa kuanzia wiki 17.

Utafiti huo ulikuja kama muendelezo wa tafiti za awali kwa binadamu na wanyama ambazo zilionesha kuwa endapo mama mjamzito atakabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo, anaweza kusababisha mwanae akawa na uwezo mdogo wa kufikiri (IQ).

Hata hivyo, watafiti hao walieleza kuwa lengo lao sio kuwapa hofu wanawake bali ni kuwatahadharisha kuhakikisha wanakuwa na afya nzuri na kuepuka mambo yanayoweza kusababisha msongo wa mawazo.

Timu ya watafiti ikiongozwa na Professa Vivette Glover wa Chuo cha Imperial cha London (Imperial College London) na wasaidizi wake ambao ni wataalam wabobezi wa afya ya mama na mtoto waliwafanyia utafiti wanawake wajawazito 267 kwa kutumia dawa maalum zinazompa mtu hali sawa na ile ya aliye na msongo wa mawazo.

Profesa Glover alisema kuwa walitoa dawa hizo kwa kuzingatia hali inayoweza kumpata mtu mwenye msongo wa mawazo wa muda mrefu ambayo ni kuchoka sana na kujisikia mgonjwa.

Hivyo, ni vyema kwa jamii kuhakikisha kuwa ili kuendela kuwa na kizazi chenye uwezo mkubwa wa kufikiria na kuamua mambo, ni vyema tukaanza na kuwajali na kuwapa furaha wanawake wajawazito.

Changamoto wanazozipitia katika ngazi za familia zinaweza kuwa chanzo cha kukosa mwana mwenye uwezo wa kuliinua Taifa.

Related Posts:

  • AINA ZA UZIBAJI WA MIRIJA YA UZAZIAINA ZA UZIBAJI WA MIRIJA Katika makala iliyopita Tuliona sababu kuu tatu zinazomfanya mwanamke asipate mimba. Kuziba kwa mirija ya uzazi huchukua asilimia ishirini ya tatizo la ugumba kwa mwanamke au mwanamke kupoteza uwezo … Read More
  • DALILI NA TIBA ZA UPUNGUFU WA DAMU KWA MJAMZITODalili Mjamzito mwenye upungufu wa damu wa kawaida mara nyingi anaweza asioneshe dalili zozote. Hata hivyo iwapo upungufu ni mkubwa, dalili za awali ni pamoja na uchovu wa mara kwa mara na kupumua kwa shida, kukosa hamu ya k… Read More
  • ZIFAHAMU DALILI ZA MTOTO MWENYE MTINDIO WA UBONGO. baadhi ya watoto kwenye jamii zetu huzaliwa na mtindio wa ubongo yaani utakuta wazazi wanagundua kama mtoto hana akili nzuri au hawezi kufanya vitu fulani kama wenzake akishakua mtu mzima kabisa. mfano kushindwa kuongea, kut… Read More
  • MIMBA KUHARIBIKA NA SABABU ZAKEMimba kuharibika ni tukio linalopatikana mara nyingi katika wanawake na mamalia wa kike kutokana na shida mbalimbali katika ukuaji wa mimba tumboni mwa mama. Ni tukio tofauti na utoaji … Read More
  • KUTOKWA UCHAFU UKENI NA TIBA YAKE.Kutokwa Na uchafu ukeni Ni sababu tosha itakayomfanya mwanamke asijisikie huru wakati wote! Kuna sababu nyingi zinazopelekea tatizo hili kutokea; Maambukizi katika uke ni tatizo la kawaida kwa wanawake na wanawake wengi wames… Read More

0 comments:

Post a Comment

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR