Saturday, December 23, 2017

Homoni zina mchango mkubwa katika afya kwa ujumla katika mwili wa mwanamke hasa linapokuja suala la uzazi. Mara nyingi usawa usio sawa wa homoni husababishwa na mabadiliko katika homoni ya ‘estrogen’.

Mabadiliko haya mara nyingi hutokea wakati wa kuvunja ungo, wakati wa hedhi, wakati wa ujauzito na wakati wa ukomo wa hedhi (menopause).

Vitu vingine vinavyopelekea mabadiliko ya homoni ni pamoja na kuongezeka umri, lishe duni, kutokujishughulisha na mazoezi, kupungua kwa ogani ya adreno, mfadhaiko au stress, kukosa usingizi, dawa za uzazi wa mpango, sumu na kemikali mbalimbali nk.
Wanawake wengi hukata tamaa ya kupata mtoto kwa kudhani Ni wagumba kumbe wakati mwingine  huwa Ni tatizo LA homoni imbalance .
sasa utajuaje unahomoni imbalance!? Na je, ufanyeje!?

Dalili zitakazokuonyesha homoni zako hazipo sawa ni pamoja na:

1. Kuwa na tabia ya hamaki (kukosa utulivu)
2. Uchovu sugu
3. Kuongezeka uzito
4. Kupungua kwa nywele
5. Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara
6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa
7. Chunusi
8. Kuwa na hamu na vyakula au vinywaji vya viwandani kila mara
9. Kushindwa kushika ujauzito
10. Kutokujisikia vizuri kila mara bila sababu maalumu
11. Kukosa usingizi
12. Hasira zisizo na sababu maalumu nk

Zipo dawa za asili zinazoweza kukusaidia kurekebisha na hatimaye kuweka sawa usawa wa homoni mwilini mwako.

Ni mhimu uonane na daktari kabla kwa uchunguzi, vipimo na ushauri zaidi kabla ya kuamua kutumia hivi vinavyopendekezwa kwenye makala hii hasa kama una matatizo kama ya uvimbe katika kizazi, saratani ya matiti, saratani ya kizazi au una saratani katika mirija ya uzazi.

Njia mbadala 6 za kurekebisha homoni zako na hatimaye upate ujauzito:

1. TUMIA OMEGA 3 KILA SIKU

Asidi mafuta yenye Omega-3 yana umhimu mkubwa katika kuweka sawa homoni zako.

Kwa wanawake yana umhimu mkubwa kwani husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi usiosawa na kupunguza dalili za kukoma kwa hedhi (menopausal symptoms). Omega-3 husaidia kuondoa sumu mwilini na vivimbe sehemu mbalimbali za mwili.

• Vitu vyenye omega 3 kwa wingi ni pamoja na mafuta ya samaki (yasiyo na mercury), walnuts, maharage ya soya, mafuta ya nazi, mafuta ya zeituni, mafuta ya mawese na mbegu za maboga. Tumia hivi vitu kila siku katika kuishi kwako ili kuweka sawa homoni zako.

2. VITAMINI D

Vitamini D ni mhimu kwa ajili ya tezi ya pituitari (pituitary gland) iweze kufanya kazi zake vizuri na ni tezi inayotengeneza homoni zingine nyingi mhimu.

Vitamini D pia husaidia kuondoa dalili zinazohusiana na usawa mdogo wa homoni ya ‘estrogen’. Vitamini D pia ina uhusiano na kiwango cha njaa ulichonacho na uzito pia.

Upungufu wa vitamini D unaweza pia kupelekea utolewaji usiosawa wa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘parathyroid’.

• Tembea juani wakati wa jua kali dakika 20 hadi 30 kila siku huku ukiwa wazi sehemu kubwa ya mwili wako.

• Kula vyakula kama mafuta ya samaki, maziwa na mayai ya kuku wa kienyeji kila siku.

3. JISHUGHULISHE NA MAZOEZI YA VIUNGO

Kujishughulisha na mazoezi ya viungo ndiyo njia rahisi ya kurekebisha homoni zako kwani mazoezi yanahusika katika uzalishaji wa hizo homoni. Mazoezi huipunguza nguvu homoni inayohusika na mfadhaiko (stresss) ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘cortisol’.

Hii homoni ya Cortisol huidhibiti homoni nyingine mhimu ijulikanayo kama ‘estrogen’ ambayo kama itazidi basi inaweza kuleta madhara kwa afya yako yote kwa ujumla.

Mazoezi ya mara kwa mara huusaidia ubongo kutoa kemikali ambazo huongeza hali ya kujisikia vizuri (improves your mood). Jambo hili la kupelekea ujisikie vizuri husaidia kuweka sawa homoni zako.

Siyo hilo tu mazoezi yatakusaidia pia kuwa na uzito sahihi kwani uzito uliozidi ni sababu mojawapo inayopelekea homoni zako kutokuwa sawa.

Nusu saa ya mazoezi kwa siku inatosha. Tatizo wanawake wengi hawana habari na kitu kinaitwa mazoezi!

• Nenda kaogelee, katembee kwa miguu lisaa limoja, au kimbia taratibu (jogging) mara 3 mpaka 4 kwa wiki.

4. TUMIA MAFUTA YA NAZI

Mafuta ya nazi yale ya asili yaliyotengenezwa nyumbani bila kupita kiwandani ni dawa nyingine nzuri ya asili ya kurekebisha na kuweka sawa homoni zako. Mafuta haya huiwezesha tezi ya koromeo (thyroid) kufanya kazi zake vizuri.

Mafuta ya nazi pia husaidia kuweka sawa sukari katika damu, huongeza kinga ya mwili, huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kusaidia pia kupunguza uzito. Mafuta haya ni mazuri kwa afya ya moyo wako na hayana kolesto yoyote mbaya.

Kunywa vijiko vikubwa viwili kila siku kwa mwezi mmoja hata miwili au hata mitatu kwa uhakika wa matokeo mazuri zaidi. Unaweza pia kuyaweka kwenye kachumbali. Pia nakushauri kila upikapo wali tumia tui zito la nazi na siyo wali tu hata katika mapishi mengine unaweza kutumia tui la nazi, kazi ni kwako.

5. UWATU PIA HUREKEBISHA HOMONI

Madaktari wengi wa tiba asili duniani hushauri kutumia uwatu (kwa Kiingereza huitwa ‘fenugreeek’) kwa ajili ya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha. Uwatu hutumika pia kama dawa ya asili ya kuongeza ukubwa wa matiti (natural breast enlargement).

Uwatu husaidia umeng’enywaji wa sukari mwilini na hivyo kuwa msaada mkubwa kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na uzito kupita kiasi (obesity).

• Chukua kijiko kikubwa kimoja cha unga wa mbegu za uwatu na uweke ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu, koroga vizuri na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja mpaka miwili.

Unaweza kuongeza asali kidogo kupata radha. Unaweza kutumia pia ndani ya maziwa ya moto hasa kama huna vidonda vya tumbo au kisukari.

6. TUMIA MREHANI (Basil)

Mrehani hutumika pia kama dawa ya asili ya kurekebisha homoni. Huiweka sawa homoni ya ‘cortisol’ ambayo kama itazidi kuwa nyingi inaweza kuleta shida kwenye homoni koromeo (thyroid gland), Mirija ya uzazi na Kongosho. Wakati huo huo mrehani husaidia kuweka sawa akili yako na hivyo huleta hali ya kujisikia vizuri (good mood).

Unaweza kupata Mrehani ukiwa Dar kwenye soko la kisutu au hata kariakoo pia Zanzibar. Ni kiungo mhimu katika mahoteli mengi ya kitalii.

• Tengeneza chai ukitumia majani fresh ya mmea huu na unywe kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa miezi miwili hadi mitatu.

MAMBO YA MHIMU KUZINGATIA:

Pamoja na dawa, zingatia haya yafuatayo kwa matokeo mazuri zaidi:

• Kula parachichi 1 kila siku
• Tumia vyakula asili zaidi kuliko vya kwenye makopo na migahawani (fast foods)
• Tumia vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber) nyingi kwenye chakula chako
• Epuka kahawa, chai ya rangi, soda nyeusi na vinywaji vingine vyote vyenye kafeina ndani yake
• Achana na msongo wa mawazo (stress) na upate usingizi wa kutosha kila siku
• Usitumie dawa za uzazi wa mpango kama unahitaji kuweka sawa homoni zako
• Epuka vilevi vyote
• Kunywa maji mengi kila siku lita 2 hadi 3
• Usitumie vyakula vya moto kwenye vyombo vya plastiki

0 comments:

Post a Comment

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR