Historia ya ugumu wa kula, au mtoto hawezi kula kwa sasa.
Historia ya mitukutiko, au mtoto anatukutika kwa sasa.
Mtoto mchanga anaonekana mlegevu au amepoteza fahamu.
Mtoto anasonga tu iwapo amesisimuliwa.
Kupumua kwa haraka.
Kifua kubonyea ndani sana.
Homa.
Hipothemia (ukimguza, unahisi kuwa mtoto ana baridi).
Mtoto amekuwa na rangi ya manjano kabla ya kufikisha umri wa saa 24.
Umanjano unaoonekana kwenye viganja vya mikono na nyayo za miguu.
Macho yamefura au yanatoa mchozo.
Usaha unatoka kitovuni.
Zaidi ya pustuli (madoa) 10 zinaonekana ngozini.
Hizi ni dalili za hatari kwa mtoto yeyote mchanga, mama ukiona dalili hizi muone daktari mapema.
0 comments:
Post a Comment