Tuesday, September 5, 2017

Image result for madhara ya fangasi kwa mjamzito
Maambukizi  ya fangasi kwa mama mjamzito hutokea kutokana na kubadilika
kwa homoni mwilini ikiambatana na upungufu wa kinga mwilini huku
ikielezwa kuwa si kila mjamzito ana uwezekano wa kupata maambukizi.

Matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi vimetajwa kuwa kisababishi kimoja
wapo kinachoweza kumfanya mama mjamzito apate fangasi hasa wa aina ya
Candida albicans.

Wakinamama wajawazito wanaoweza kupata maambukizi ya fangasi ni wale
wenye tabia ya kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri
kama nguo za kuogelea (swim wear), nguo za ndani zilizotengenezwa kwa
kitambaa aina ya nailon au zinazobana sana.

Akizungumza na mwandishi wa Hivisasa Afisa matibabu katika zahanati ya
Kigogo Dokta Ambakisye Mwalusamba ameeleza kuwa licha ya matumizi ya
nguo au mavazi yanayoleta joto lakini pia mtindo wa kujamiiana kwa
kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi vyenye
glycerin wakati wa tendo la ndoa kuna uwezekano mkubwa wa kupata
maambukizi ya maradhi haya.

Aidha ametaja namna muathirika wa maradhi hayo anavyotakiwa kupata
vipimo ni pamoja na kumueleza daktari kumfahamisha mgonjwa aina ya
kipimo, lengo lake na jinsi kitakavyofanyika ili kumuandaa kisaikolojia
huku kabla ya kumfanyia vipimo vya uchunguzi wa uke ambavyo kitaalamu
huitwa Per Vaginal Examination (PV exam) kuona kama kuna uvimbe wowote
ndani ya uke au kama ana maumivu wakati wa kujamiiana hali
Itakayoashiria wazi kuwako kwa aina fulani ya fangasi katika sehemu hizo.

Hata hivyo Daktari anaweza kuchukua kipimo na kuotesha kwenye mahabala
ili kuangalia aina ya uoto huo kama ni wa fangasi aina ya Candida
albicans, au atafanya kipimo cha mkojo (Urinalysis) na cha ugonjwa wa
kisukari, HIV/AIDS, ugonjwa wa  kuvimba tezi la koo (goiter) na kadhalika.

Amefafanua kuwa Dokta ataangalia kama kuna uchafu wowote unaotoka, wingi
wake, rangi yake, harufu yake, uzito wake na aina ya uchafu unaotoka
kama ni sahihi kutokana huku akilinganisha na  maelezo ya mgonjwa.

Jinsi ya kujikinga na Fangasi

– kutovaa nguo za kubana ambazo zitapelekea kusababisha joto ukeni   na
kuacha majimaji  yatakayosababisha fangasi,

– Mama huyo anashauriwa kujifuta na kujikausha vizuri katika sehemu za
siri pindi anapotoaka      kuoga au kujisaidia kutoka kwamba pindi
atakapokuwa katika kipindi cha ujauzito hutoka na jasho mara kwa mara na
kubanwa na haja ndogo.

– Kuacha tabia ya kuvaliana nguo au kuazima nguo za mtu mwingine  huenda
 ikawa ana ugonjwa wa fangasi.

0 comments:

Post a Comment

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR