Monday, July 17, 2017

Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu.
Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mama na mtoto ikiwemo kifo.

Madhara haya ni pamoja na Madhara kwa mama kipindi cha ujauzito:

kukonda au kuongezeka uzito kwa kiasi kidogo sana,

kuhisi uchungu kabla ya muda,

kondo la nyuma kutunga pasipostahili,

shinikizo la damu wakati wa ujauzito, na chupa kupasuka kabla ya wakati.

Madhara kwa mama wakati wa kujifungua:

kupatwa na uchungu usioeleweka na usio wa kawaida,

mtoto kuvuja damu ndani kwa ndani,

kupatwa na shock, hatari ya ganzi (anesthesia risk) kwa anayefanyiwa upasuaji,

moyo kushindwa kufanya kazi.

Madhara kwa mama baada ya kujifungua:

maambukizi baada ya kujifungua,

kizazi kushindwa kurudi katika hali ya kawaida au damu kuganda kwenye mishipa.

Madhara kwa mimba na mtoto atakayezaliwa:

Madhara ni pamoja na mtoto kuzaliwa njiti,

mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,

mtoto kuwa na score ndogo (poor Apgar score), 

mtoto kuzaliwa akiwa amechoka (fetal distress),

Upungufu wa damu kwa mtoto, Watoto wanaozaliwa wakiwa na upungufu wa damu hukua kwa tabu, huwa na maendeleo duni ya kiakili na kimatendo (poorer intellectual developmental milestones),

uwezekano mkubwa wa kuwa na kasoro mwilini na hata kifo.

Kasoro hizo ni pamoja na matatizo ya magonjwa ya moyo yakuzaliwa nayo.

Kila mama mjamzito anapaswa kuwa makini katika kipindi cha ujauzito ili kuepusha madhara haya.

0 comments:

Post a Comment

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR