WASICHANA wengi hasa walio na uwezo wa kushika mimba ambao
wanasoma au hawajaolewa wamekuwa wakijihusisha na matukio ya kutoa mimba
mara kwa mara bila kufikiria athari za kutoa mimba kwa uzito.
Athari hizo ni pamoja na kuweka maisha hatarini, kuharibu
kizazi, kujiweka katika hatari zaidi ya kupata maradhi kama Saratani ya
Shingo ya Kizazi, kushitakiwa na nchi kwa kosa la kuua pamoja na
kuharibu uhusiano wao na Mungu.Machaguo ya Kuzuia Mimba kwa Vijana walio
Masomoni :-
Kusubiri wakati unaofaa
Vijana wanatiwa moyo kusubiri na dini zao na walezi wao,
ingawa hata serikali ina sheria zinazopendekeza umri sahihi kujihusisha
na ngono. Kijana anaweza kuamua kibinafsi kusubiri muda muafaka na kuwa
na mtu sahihi.
Kusubiri kutakuweka salama na bila wasiwasi wowote wa
kuambukizwa magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya ngono. Kuwa salama
kutakufanya kukazia malengo yako ya maisha.
Maamuzi ya kusubiri wakati unaofaa hakutakufanya mihemko ya
ngono kupotea bali itakubidi kukazia fikra mambo ya msingi katika
maisha yako badala ya kuwaza ngono.
Ngono salama
Waopendwa wasomaji wa Gazeti hili mtandao la FikraPevu hapa
ninamaana ya kutumia njia ambazo zinazopunguza uwezekano wa kupata
mimba au magonjwa ya ngono ukitia ndani Virusi vya UKIMWI (VVU). Mihemko
ikikuzidi na ukashindwa kusubiri wakati unaofaa kuanza ngono ni bora
kujilinda wewe na mwenzi wako kwa kutumia kinga.
Mipira (Kondom) ndio njia pekee itakayokukinga usipatwe na
ujauzito na magonjwa ya ngono ikiwemo VVU, wakati huo huo hutumika kama
njia ya uzazi wa mpango.
Vidonge vya dharura vya Uzazi wa Mpango
Ikitokea umefanya ngono bila kinga ya kondom hasa kwa mtoto
wa kike ambaye hakuwa anatumia njia za uzazi wa mpango inashauriwa
kutumia vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango ili kuzuia mimba
isiyotarajiwa ingawa vidonge hivyo havitasaidia kupunguza hatari ya
kuambukizwa na magonjwa ya ngono ikiwemo VVU.
Vidonge
vya dharura vya uzazi wa mpango ni vidonge vya vya uzazi wa mpango
ambavyo ni vya aina kuu mbili, vidonge vyenye vichocheo viwili vitwavyo
Estrojeni na Projesteroni na vidonge vyenye kichocheo kimoja tu cha
Projesteroni.
Vidonge
vya dharura vya uzazi wa mpango vipo vya aina tofauti na zina nguvu
tofauti, kuna zinazopaswa kutumika ndani ya masaa 72 (Siku 3) baada ya
ngono isiyo salama na kuna zinazopaswa kutumika ndani ya masaa 120 (Siku
5) baada ya ngono isiyo salama.
Aina
zote za vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango hufanya kazi ya kuzuia
mimba kwa kuzuia Ouvuleshaji ambapo huzuia au kuchelewesha yai kutoka
kwenye kokwa (Foliko za Graaf) zilizomo katika Ovari.
Katika
hali zisizotarajiwa, mabinti hubakwa na watu wasiowafahamu hali zao za
afya. Ikiwa umetokewa na hali hiyo tafuta ushauri wa kitiba haraka sana.
Katika hali hiyo unaweza kumeza vidonge vya dhalula ndani ya saa 72
hadi 120 tangu ulipofanya ngono ili kuzuia mimba. Pia daktari anaweza
kukupima VVU na kukupa vidonge vitakavyo kukinga na VVU ikiwa
haijulikani hali ya VVU ya mbakaji.
Vidonge
vya dhalula vya uzazi wa mpango vinaweza kutumika kabla ya ngono isiyo
salama kama una hofu na njia ya uzazi wa mpango unayotumia sasa, kama
unaenda likizo na hutoweza kupata vidonge vya dhalula vya uzazi wa
mpango. Muulize daktari au muuguzi ili upate taarifa kamili kuhusu
kutumia vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango kabla ya ngono isiyo
salama.
Baada
ya kutumia vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango ikiwa hedhi yako
itachelewa zaidi ya siku 7 au ni nyepesi au ya muda mfupi sana wasiliana
na mtaalamu wa afya ili kupima mimba kwanza.
Athari
zinazojitokeza mara kwa mara baada ya kutumia vidonge vya dhalula vya
uzazi wa mpango ni pamoja na maumivu ya tumbo, kuumwa kichwa, hedhi
kubadilika badilika inaweza kuwa matone tu au nyingi zaidi, kujihisi
uchovu na kuumwa.
Athari
zinazojitokeza kwa uchache ni pamoja na matiti kujaa na kuuma,
kizunguzungu na kutapika. Ni busara kuwasiliana na mhudumu wa afya ya
uzazi ikiwa utapatwa na dalili zisizo za kawaida.
Vidonge
vya dhalula vya uzazi wa mpango vinaathiriwa na dawa zingine kama za
kutibu Kifafa, VVU, Kifua Kikuu na Vidonda vya Tumbo. Hivyo wasiliana na
mtaalamu wa huduma za uzazi wa mpango kabla ya hujatumia vidonge vya
dharura vya uzazi wa mpango.
Kitanzi (Intrauterine Device)
Kitanzi
kinaweza kuwekwa kwenye uterasi ogani ambamo utungo wa mimba hupokolewa
na kustawishwa ndani ya masaa 120 (Siku 5) baada ya ngono isiyo salama
au siku 5 kabla ya Ouvuleshaji. Kitanzi kinaweza zuia yai kurutubishwa
na mbegu ya kiume. Wanawake chini ya asilimia 1 wanaotumia kitanzi ndio
wanaweza kupata mimba.
Kitanzi
ni kifaa kidogo chenye umbo la T kilichotengenezwa kwa plastiki na kopa
(Copper). Kifaa hiki huingizwa kwenye uterasi/kizazi (ogani ambamo
utungo wa mimba hupokelewa na kustawishwa) na mtaalamu wa afya mwenye
utaalamu huo. Kifaa hiki kinafanya kazi kwa kuzuia yai kurutubishwa na
mbegu ya kiume (manii).
Kuna
aina nyingi za Vitanzi. Aina mpya zina kopa zaidi na zina ufanisi zaidi
ya asilimia 99. Wanawake chini ya wawili kati ya wanawake 100
wanaotumia aina mpya kwa zaidi ya miaka 5 ndio wanaoweza kupata mimba.
Vitanzi vyenye kopa kidogo vina nguvu kidogo ukilinganisha na vyenye
kopa nyingi ila bado vinaweza kuzuia mimba.
Ikiwa
umefanya ngono isiyo salama, kitanzi kinaweza kuwekwa ndani ya siku 5
baada ya ngono isiyo salama na kuweza kuzuia mimba. Ni njia madhubuti ya
kuzuia mimba kuliko vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango na pia
hakiingiliani na dawa zingine. Unaweza pia kuamua kukiacha kama njia
yako ya uzazi wa mpango.
Mara
nyingi wanawake wengi wanaweza kutumia kitanzi kwa kukiingiza ndani ya
uke na wale ambao hawakuwahi kushika mimba, wanaonyonyesha na wale wenye
VVU. Mtaalamu wa afya ya uzazi atakuuliza juu ya historia yako ya
matibabu ili kufahamu kama kitanzi kitakufaa.
Hupaswi
kutumia kitanzi kama una ugonjwa wa zinaa au maambukizi kwenye via vya
uzazi, ukiwa na kasoro ya maumbile kwenye mlango wa uzazi au unatokwa na
damu ukeni hasa baada ya tendo la ndoa au baada ya hedhi. Wanawake
waliopata mimba nje ya fuko la kizazi au walio haribu mimba hivi
karibuni au wanaotumia vifaa bandia vya moyo wanapaswa kuwasiliana na
daktari kabla ya kuwekewa kitanzi.
Athari
za kutumia kitanzi ni chache ila mtu anaweza kupata maumivu, maambukizi
ya njia ya mkojo na kizazi. Kama utatumia kitanzi kama njia yako ya
uzazi wa mpango, kitafanya siku zako za hedhi kuwa nyingi zaidi pamoja
na kutokwa na hedhi nyingi na maumivu zaidi. Kama unahisi vibaya au
maumivu baada ya kuweka kitanzi, kutumia dawa za kutuliza maumivu
zinaweza kutumika kupunguza tatizo.
imeandikwa na TAZAMA LINE
0 comments:
Post a Comment