Mimi ni mama, ninafurahi sana kuitwa mama huku nikitimiza majukumu yangu kama mama.
Zipo sababu nyingi zinazonifanya nifurahie kuitwa mama...
Mimi ni mama bora, je, nimewezaje kuwa mama bora!?
Kwa kuzingatia haya;
1.ninahakikisha mtoto wangu anafuraha kila wakati.
2.natambua wajibu wangu kama mama na kumpa mtoto kile anachohitaji na kinachofaa.
3.namkanya mwanangu kila akoseapo, kunawakati nakuwa mkali kiasi na wakati mwingine hutumia adhabu ndogondogo zinazoendana na umri Wa mwanangu.
4.sio MTU Wa kutetea uovu Wa mwanangu Bali huruhusu kuadhibiwa inapobidi.
5.nimejiweka karibu na mtoto wangu Ili kuweza kubaini jambo lolote LA tofauti kwake.
6.nimempa kila sababu ya kuwa muwazi kwangu hata kwa vitu ambavyo kwake ni vigumu najitahidi kuviweka sawa.
7.Mimi ni mshauri mzuri Wa mwanangu.
******
Sifa zangu ni nyingi sana, kupitia hizo chache unaweza jitathimini je, wewe ni MAMA BORA au BORA MAMA!?
#uzazisalama
#afyanauzazi
0 comments:
Post a Comment