Saturday, October 7, 2017

UMUHIMU WA KUNYONYESHA MAZIWA YA MAMA Kunyonyesha maziwa ya mama kunampa Mama Pamoja na Mtoto faida nyingi.

Faida kwa mtoto:

• Humpatia virutubisho (viini lishe) vyote anavyohitaji kwa uwiano ulio sahihi
kwa ukuaji na maendeleo yake;

• Humpatia kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kama kuharisha, magonjwa ya
njia ya hewa na masikio;

• Humwezesha mtoto kukua kimwili na kiakili kikamilifu;

• Huleta uhusiano mzuri na wa karibu kati ya mama na mtoto;

• Watoto walionyonya maziwa ya mama huwa na mwenendo mzuri pamoja na
akili ukilinganisha na wale wasionyonya maziwa ya mama.

• Maziwa ya mama humeng’enywa (huyeyushwa) kwa urahisi tumboni mwa
mtoto na hivyo kutumiwa na mwili kwa ufanisi.

Kunyonyesha kunasaidia kumkinga

mtoto na magonjwa mbalimbali

Faida kwa mama:

Huchangia katika kulinda afya ya mama kwa njia mbalimbali kama zifuatazo:

• Mama anaponyonyesha mara baada ya kujifungua husaidia tumbo la uzazi
kurudi katika hali ya kawaida mapema. Na pia husaidia kupunguza damu kutoka
hivyo kuzuia upungufu wa wekundu wa damu (upungufu wa damu);

• Hupunguza uwezekano wa kupata ujauzito katika miezi sita ya mwanzo kama
mama atamnyonyesha mtoto maziwa yake tu mara nyingi kwa siku na pia
kama hajapata hedhi;

• Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya mfuko wa uzazi, na matiti;

• Hujenga uhusiano wa karibu kati ya mama na mtoto; na

Unyonyeshaji bora wa Maziwa ya Mama 5

Kunyonyesha kunasaidia kumkinga

mtoto na magonjwa mbalimbali

• Iwapo mama aliongeza uzito mwingi wakati wa mimba, kunyonyesha husaidia
kumrudishia mama umbile lake la kawaida.
Faida nyingine za maziwa ya mama:
• Ni safi na salama, hupatikana muda wote katika joto sahihi kwa mtoto na
hayahitaji matayarisho;

• Hayaharibiki ndani ya titi na hata yakikamuliwa huweza kukaa saa 8 katika
joto la kawaida bila kuharibika, na saa 72 kwenye jokofu;

• Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na maziwa mbadala;

• Huokoa fedha za kigeni ambazo zingenunulia maziwa mbadala na madawa;

• Huokoa muda wa mama na fedha za familia ambazo zingenunua maziwa
mbadala au kulipia matibabu;

• Hayaleti matatizo ya mzio (“allergies”) kama pumu (asthma ) na magonjwa ya
ngozi;
• Maziwa ya mama hutunza mazingira, kwani hayaachi mabaki kama makopo na
chupa ambavyo hutumika kwa maziwa mbadala.

Mtoto aanze kunyonyeshwa maziwa ya mama yake mara tu
anapozaliwa

0 comments:

Post a Comment

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR