Ulaji wa mara kwa mara wa viazi, bila kujali kama ni vya kuchemshwa au vya kukaangwa ama chips, unaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maradhi ya kisukari wakati wa ujauzito, wameeleza watafiti wa Marekani.
Hii labda ni kwa sababu wanga uliomo katika viazi unaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya sukari zaidi, wanasema.
Utafiti wao ulihusisha wanawake wajawazito zaidi ya 21,000.
Lakini watafiti wa Uingereza wanasema ushahidi huo una mapungufu na kuongeza kuwa watu wengi wanahitaji kula zaidi vya wanga ili kupata nyuzi nyuzi, pamoja na matunda na mboga
Utafiti huo wa BMJ unahusu ulaji wa viazi hadi kiwango cha kuwa na uwezekano wa hatari ya kuugua kisukari
Jaman Sasa mim kila wakat nasikia hamu ya kula viazi tu chakula vingine nashindwa nifanyaje Sasa ? 🙄
ReplyDelete