Kuna baadhi ya wazazi wamejikuta wakiwaumiza watoto wao kwa joto au baridi kutokana tu Na kutokujua ni mavazi Gani sahihi kumvalisha kwa wakati Gani!?
Wazazi wengi wameshawapoteza watoto wao kwa nimonia au vifua vilivyozidi, hii ni kutokana Na kutojua mavazi sahihi ya kumvisha mtoto wakati Wa baridi.
Leo nitapenda ufahamu kwa namna Gani unaweza kumfanya mtoto wako afurahie hali ya hewa ya baridi.
** katika nyakati za baridi watoto wengi hupatwa Na vikohozi hii ni kutokana Na vifua vyao kuwa bado havijakomaa hivyo baridi kupenya kwa urahisi.
**hakikisha unamvalisha mtoto mavazi yatakayompa joto, sweta zito Na suruali, kofia , soksi au hata Viatu inapobidi.
**ukizingatia haya itasaidia Sana afya ya mtoto wako kuwa salama.
Toa maoni yako.
0 comments:
Post a Comment