Wanawake wanaokula udongo wakiwa wajiwazito wamo katika hatari ya kuwafanya watoto watakowajifungua kutofanya vizuri shuleni.
Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa watoto ambao kina mama wao walikuwa wakitumia udongo hawakomakiniki darasani.
Kwa kawaida wanawake wengi hutumia udongo huo baadhi wakidai kuwa wana upungufu wa madini ila wengi wao huzidisha matumizi yake.
Zaidi ya wazazi 4000 walihusishwa katika utafiti huo lakini ni 1000 tu ambao maoni yao yalitumika kuandaa ripoti ya utafiti huo.
Taasisi hiyo ilikuwa ikifuatilia matokeo ya watoto hao wakiwa shuleni kwa muda wa miaka minne na wakatambua kuwa wale ambao hawakuwa imara darasani mama zao walikuwa na historia ya kutumia udongo wakiwa wamebeba mimba zao.
Watafiti hao wanasema kuwa kutokana na hayo ubongo wa watoto waliozaliwa huchelewa kushika mambo.
Kadhalika utafiti huo unaonyesha kuwa wanawake katika miaka ya ishirini huwa na hamu kubwa kutumia udongo.
Nini maoni yako juu ya matumizi ya udongo kwa wajawazito!?
0 comments:
Post a Comment