Njia ya kawaida zaidi ya kupata maziwa ya mama ni ile ya mtoto kunyonya kutoka kwa mama yake mwenyewe lakini maziwa yanaweza kukamuliwa na kisha akanyeshwa kupitia chupa, kikombe na / au kijiko, mtindo wa nyongeza matone, na tubu ya nasogastiriki. maziwa yanaweza kutolewa na mwanamke ambaye si mama ya mtoto,aidha kupitia msaada wa maziwa yaliyokamuliwa(kwa mfano kutoka benki ya maziwa), au wakati mwanamke anapomnyonyesha mtoto ambaye si wake kwa matiti yake - hii hujulikana kama mama wa kunyonywa.
Faida hizi ni pamoja na;
1.kupunguzwa kwa dari hatari ya kifo cha ghafla kwa watoto wachanga (SIDS),
2.inaongeza akili
3. inapunguza uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa wa katikati mwa sikio, homa, na viini vinavyolete homa,
4.hupunguza uwezekanno wa kupata baadhi ya saratani kama vile sarateni ya damu kwa watoto,
5.kupunguza hatari ya mwanzo wa ugonjwa wa kisukari wa mtoto,
6.hupunguza hatari ya pumu na ezema, hupunguza matatizo ya meno,
7.Hupunguza hatari ya fetma baadaye katika maisha, na hupunguza uwezekano wa kupata matatizo ya kisaikolojia.
8.Kunyonyesha pia hutoa manufaa ya kiafya kwa mama. Husaidia uterasi katika kurejea hali yake ya kawaida kabla ujauzito na hupunguza kuvuja damu baada ya kuzaa,
9. husaidia mama kurudi kwa uzito wake kabla ya ujauzito.
10. hupunguza hatari ya saratani ya matiti baadaye katika maisha.
Hakikisha unamnyonyesha mtoto wako kwa umri usio chino ya miezi 6 kabla ya kianza kula Chakula kingine.
0 comments:
Post a Comment