Tuesday, September 5, 2017

Utamaduni wa Tanzania unapendekeza wanawake kuvaa nguo kubwa, zilizopwaya wakati wa ujauzito. Kama vile hawana haja ya kupendeza wakiwa wajawazito. Bahati nzuri, kuna maduka mengi zenye mavazi mazuri za wakati wa ujauzito.
Image result for mavazi ya mama mjamzito
Ila bado kuna wanawake wengi wanaoamua kutojali muonekano wao wakiwa wajawazito. Sasa, kwa wao, vidokezo vifuatayo vitakusaidia kuvaa ukiwa mjauzito.

1. Kubali umbo lako
Hamna haja ya kuficha ujauzito wako. Ila hatusema kwamba uvae blauzi inayobana na kimini (ila, unaweza kuvaa hivyo ukipenda). Tunachopendekeza hapa ni kuvaa nguo zinazotosha umbo lako.Tumbo lako likianza kujitokeza, nunua nguo kama gauni, jinzi na topu zinazo ruhusu hewa kupita; hizi zitakuwezesha kuonyesha figure yako kwa kistaarabu.

2. Usibadilishe mtindo wako wa kawaida
Kwa kuwa we ni mjazmzito haimaanisha kwamba inabidi ubadilishe mtindo wako wa kipekee.
Kwa hiyo, kama ulikuwa unapenda gauni, endelea kuvaa gauni. Hakikisha inatosha umbo lako tu.

3. Tumia vifaa vya mitindo
Scafu, bangili, ereni n.k zitasaidia kuboresha vazi lako kwa ujumla na zitakusaidia kujiamini pia. Kwa mfano, kama unawasiwasi na tumbo lako lilivyojitokeza, vaa mkufu au ereni safi zitakazo fanya watu waangalie sura badala ya tumbo yako.

4. Nunua Jinzi safi kwa ajili ya ujauzito
Nunua jinzi zenye uwezo wa kupanuka ndio zitakazokufaa. Zinaweza zikawa za kubana au zenye nafasi zaidi, cha muhimu nikwambai unajisikia vizuri ukizivaa.

5. Nunua gauni ya kufunga (Wrap Dress)
Wrap Dress zinafaa kwa umbo yoyote ile na zinapendeza sana! Pia ni rahisi kuzivaa na kutembea ndani yao ukiwa umezivaa.
 
6. Nunua nguo zenye rangi kali
Rangi kali kama njano na rangi ya machungwa (orange) zinaonyesha ile mwanga asili ambao wajawazito huwa wanao. Kwa hiyo, kuvaa gauni yenye rangi kali inaweza ikampa mjamzito mng’ao wa kirembo.

Onekana vizuri zaidi ya unavyojisikia
Kuwa mjamzito ni wakati muhimu katika maisha ya mwanamke na kwa kuwa hutajisikia vizuri kila siku ya ujazito wako, unaweza kuendelea kupendeza na kutafuta nguo zitakazoipendza mwili wako.
Image result for mavazi ya mama mjamzito

Related Posts:

  • SABABU ZINAZOPELEKEA KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZITO.HILI ni tatizo linalosababisha ugumba kwa wanawake kwa kiasi kikubwa. Wanawake wanaoshindwa kupata ujauzito hukabiliwa na matatizo matatu; * kwanza kabisa ni kuziba kwa mirija ya mayai kama tutakavyoona leo * matatizo katika… Read More
  • MLO KAMILI KWA MJAMZITOLishe wakati wa ujauzito ni muhimu kwa ajili ya afya yako na maendeleo mazuri ya mtoto anayekua tumboni. FUATA MLOLONGO HUU KUWA NA LISHE BORA; 1.Jitahidi upate mlo kamili kila siku kwa kupata vyakula vya wanga, protini, mafu… Read More
  • MADHARA YA UPUNGUFU WA DAMU KWA MJAMZITOSehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mama na mtoto iki… Read More
  • KUNAWA MIKONO NI AFYA.Wakina mama wengi wenye watoto wachanga hawana kawaida ya kunawa mikono Mara kwa Mara watakapo kumuhudumia mtoto. Yakupasa kunawa mikono kila Mara kwa kufuata utaratibu huu; *Kabla ya kunyonyesha *Kabla ya kumvisha au kumvua … Read More
  • ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MTOTO MCHANGAHistoria ya ugumu wa kula, au mtoto hawezi kula kwa sasa. Historia ya mitukutiko, au mtoto anatukutika kwa sasa. Mtoto mchanga anaonekana mlegevu au amepoteza fahamu. Mtoto anasonga tu iwapo amesisimuliwa. Kupumua kwa haraka… Read More

1 comment:

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR