Utamaduni wa Tanzania unapendekeza wanawake kuvaa nguo kubwa,
zilizopwaya wakati wa ujauzito. Kama vile hawana haja ya kupendeza
wakiwa wajawazito. Bahati nzuri, kuna maduka mengi zenye mavazi mazuri za wakati wa ujauzito.
Ila bado kuna wanawake wengi wanaoamua kutojali muonekano wao wakiwa
wajawazito. Sasa, kwa wao, vidokezo vifuatayo vitakusaidia kuvaa ukiwa
mjauzito.
1. Kubali umbo lako
Hamna haja ya kuficha ujauzito wako. Ila hatusema kwamba uvae blauzi
inayobana na kimini (ila, unaweza kuvaa hivyo ukipenda).
Tunachopendekeza hapa ni kuvaa nguo zinazotosha umbo lako.Tumbo lako
likianza kujitokeza, nunua nguo kama gauni, jinzi na topu zinazo ruhusu
hewa kupita; hizi zitakuwezesha kuonyesha figure yako kwa kistaarabu.
2. Usibadilishe mtindo wako wa kawaida
Kwa kuwa we ni mjazmzito haimaanisha kwamba inabidi ubadilishe mtindo wako wa kipekee.
Kwa hiyo, kama ulikuwa unapenda gauni, endelea kuvaa gauni. Hakikisha inatosha umbo lako tu.
3. Tumia vifaa vya mitindo
Scafu, bangili, ereni n.k zitasaidia kuboresha vazi lako kwa ujumla
na zitakusaidia kujiamini pia. Kwa mfano, kama unawasiwasi na tumbo lako
lilivyojitokeza, vaa mkufu au ereni safi zitakazo fanya watu waangalie
sura badala ya tumbo yako.
4. Nunua Jinzi safi kwa ajili ya ujauzito
Nunua jinzi zenye uwezo wa kupanuka ndio zitakazokufaa. Zinaweza
zikawa za kubana au zenye nafasi zaidi, cha muhimu nikwambai unajisikia
vizuri ukizivaa.
5. Nunua gauni ya kufunga (Wrap Dress)
Wrap Dress zinafaa kwa umbo yoyote ile na zinapendeza sana! Pia ni rahisi kuzivaa na kutembea ndani yao ukiwa umezivaa.
6. Nunua nguo zenye rangi kali
Rangi kali kama njano na rangi ya machungwa (orange) zinaonyesha ile
mwanga asili ambao wajawazito huwa wanao. Kwa hiyo, kuvaa gauni yenye
rangi kali inaweza ikampa mjamzito mng’ao wa kirembo.
Onekana vizuri zaidi ya unavyojisikia
Kuwa mjamzito ni wakati muhimu katika maisha ya mwanamke na kwa kuwa
hutajisikia vizuri kila siku ya ujazito wako, unaweza kuendelea
kupendeza na kutafuta nguo zitakazoipendza mwili wako.
Tuesday, September 5, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Asante kwa elimu
ReplyDelete