
Kuna imani imekuwa ikijitokeza kwamba kufanya mapenzi kipindi wakati mtoto angali ananyonya ndio hupelekea hali ya mtoto kuwa mbaya huku ikifahamika kama KUBEMENDA lakini katika hali halisi hii si kweli kabisa kwani kuzorota kwa afaya ya mtoto husababishwa na mambo yafuatayo.
Kukosa maziwa ya mama ya kutosha
Mtoto kushindwa kunyonya vizuri
Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.
Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.
Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.
Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).
KAMA MZAZI IANAKUPASA KUMJUA NA KUMCHUNGUZA MTOTO WAKO KILA WAKATI ILI KUWEZA KUBAINI TATIZO LIKO SEHEMU IPI NA UWEZE KUMTIBIA MAPEMA.
0 comments:
Post a Comment