Mtoto
huyo alipewa dawa za majaribio ya kukabiliana na virusi hivyo
alipozaliwa lakini hajapewa dawa zozote za kukabiliana na virusi hivyo
tangu afikishe mwaka mmoja.
Hii ni mara ya kwanza kwa mtu mwenye VVU kuishi bila virusi hivyo barani Afrika.
Wanasayansi
waliogundua kuhusu afya ya mtoto huyo mwenye miaka 9 na nusu kwa sasa,
wanamuangalia na kumfuatilia kwa karibu zaidi.
Wanasema kuwa matukio kama hayo ni machache na kwamba familia ya mtoto huyo ina furaha.
Watafiti
wanaamini kupotea huko kwa vurusi sio kwa sababu ya matibabu lakini
mtoto huyo ana jeni ama kinga zisizokuwa za kawaida ambazo zimemlinda
dhidi ya virusi vya Ukimwi.
0 comments:
Post a Comment