Furaha
kubwa ya mama mja mzito ni kumzaa mtoto aliye na afya njema na asiye na
shida yoyote. Lakini kwa akina mama wengi, furaha hii hukatizwa na unene
wa tumbo unaokuja baada ya kujifungua.
Shida kubwa huwa ni tumbo ambalo ni nene kuuliko mwili. Sababu hii huwafanya akina mama wengine kutoupenda mwili wao.
jinsi ya kupunguza tumbo baada ya kujifungua. Iwapo watayafuatilia maagizo haya vikamlilifu, basi unene wa tumbo baada ya kujifungua utaisha.
1- Kuwa na motisha
Ni muhimu
kwa mama kuwa na motisha anapoamua kulipunguza tumbo baada ya
kujifungua. Tena, anafaa kuwa na uvumilivu. Kupunguza tumbo hilo
huchukua muda sawia na ule wa kubeba mimba. Kwa ufupi, inawezekana
kwamba kama tu ilivyochukua miezi tiza kwa tumo kunenepa, itachukua
miezi sawia kupungua.
Hivyo
basi, mama hafai kufa moyo au kuwa na haraka. Kuna uwezekano kwamba mama
anaweza kufanya vitu ambavyo hakuzoea pale awali kama kufanya mazoezi,
kuacha vyakula fulani na kuanza kuvila vingine. Hii ni safari
inayohitaji motisha.
2- Kunyonyesha mtoto
Njia ya
pili ya kupunguza tumbo ni kumnyonyesha mtoto. Ni asili kwa mwili wa
mwanamke kurudia hali ya mbeleni pole pole baada ya kumzaa mtoto.
Kwa mfano,
mfuko wa uzazi hurudia hali yake ya kawaida. Vile vile, iwapo watakua
na subira na kuwanyonyesha wanao, basi tumbo hurudia ukubwa ule wa
awali.
3- Kuepukana na pombe
Iwapo mama
anakunywa pombe kwa wingi baada ya kujifungua, ni ngumu kwa tumbo
kurudi ukubwa ule wa kawaida. Pombe, pamoja na vinywaji vyenye sukari
nyingi, huadhiri njia ya ini ya kufanya kazi. Adhari mojawapo ni
kutotengeneza misuli ifaavyo mwilini.
Ini
linapolemewa kuunda misuli, mwili hujaa mafuta na kusababisha mtu
kunenepa. Hivyo basi, mama anapokunywa pombe, sio tumbo tu linalonenepa;
mwili wote huadhirika. Hivyo basi, unywaji wa pombe haufai baada ya
kujifungua.
4- Kufanya mazoezi ya tumbo
Huenda
ikawa vigumu kuanza mazoezi mara tu mama anapojifungua. Hivyo basi, ni
vyema kusubiri mpaka mwili utakaporudia hali ya kawaida na kupata nguvu.
Hata hivyo, mama hafai kufanya mazoezi mazito au mengi sana.
Kwahivyo,
anza kwa mazoezi madogomadogo yanayolenga tumbo. Kwa mfano, unaweza
kulala kwa mgongo na kuyakunja magoti. Baada ya hapo, unauinua mwili wa
juu polepole kisha kulala tena. Rudia zoezi hili mara kadhaa kwa siku.
Kuna mazoezi mengi ambayo utaelezwa na daktari.
5- Kutembea
Kutembea
ni aina ya mazoezi ambayo husaidia kupunguza tumbo. Inawezekana kutembea
kukaonekana kama mazoezi duni, lakini, husaidia sana kwa kulainisha
tumbo.
Mtu
anapotembea, misuli mingi mwilini hutumika, ikiwemo ile ya tumbo. Hivyo
basi, mafuta yaliyokusanyika sehemu ya tumboni huisha na tumbo kupungua.
Zoezi hili linaweza kukufaa sana iwapo utambeba mtoto wako mgongoni
(kuongeza uzito).
6- Kufanyisha misuli mikubwa mazoezi
Hata
ingawa lengo ni kupunguza tumbo, mama anafaa kuifanyisha misuli yote
mazoezi. Unapofanya mazoezi yalengayo tumbo pekee, mafuta huchomeka
polepole mwilini.
Iwapo
unataka kulipunguza tumbo haraka, basi unaarifiwa kufanya mazoezi
yalengayo misuli mikubwa mwilini. Hii ni kama miguu, mikono na mgongo.
Hii itazuia kulipunguza tumbo na kubakia na mafuta (unene) kwingine
mwilini.
7- Kupumua kwa undani
Zoezi hili
ni rahisi sana na mama anaweza kulianza saa moja tu baada ya
kujifungua. Mama anafaa kuketi kitako na kuvuta hewa kwa ndani.
Anapoivuta
kwa ndani, anafaa kuukunjua mgongo na kasha kuifungia hewa ile kidogo
tu. Kasha, anaitoa pumzi ile na kutulia kidogo, kasha kurudia. Zoezi
hili husaidia misuli ya tumbo kulegeza na kumfanya kupona kwa haraka.
8- Kufunga kitambaa cha kupunguza tumbo
Hii ni
njia mojawapo ya zile zinazotumika sana na ambayo imewkuwepo kwa muda
mrefu. Muda mfupi baada ya kujifungua, kitambaa spesheli
kilichotengenezwa kwa pamba hufungwa tumboni.
Lengo la
kitambaa hicho ni kupunguza kufura na kuirudisha misuli kuwa na ukubwa
wa kawaida. Kwa kawaida, kitambaa hicho hufungwa kwa muda wa wiki moja
kasha mama anapumzika kiasi na kurudia tena. Kitambaa cha kawaida
kilichoundwa kwa pamba kinaweza kutumika pia.
9- Kula chakula cha kutosha
Kadri na
maelezo fulani kuwa mama akila kiasi atapunguza tumbo, ni bora kuzuia
njaa kabisa. Kando na kutopunguza tumbo, njaa inaweza kuzuia kupona kwa
haraka.
Mama
anapokaa njaa kwa muda, kuna uwezekano kuwa atakula chakula kingi
baadaye. Kula chakula kingi kutachangia kunenepa kwa tumbo.
10- Kula vyakula vidogo mara nyingi kwa siku
Badala ya
kukaa njaa kwa muda kasha kula chakula kingi baadaye, ni heri kula
vyakula vidogovidogo mara kadhaa kwa siku. Hii inawezesha mwili kusiaga
chakula chote bila kuhifadhi cha ziada kama mafuta mwilini. Nguvu
itokanayo na kula vyakula vidogovidogo hutumika kikamilifu na kuzuia
kunenepa tumbo na mwili kwa jumla.
11- Punguza vyakula vya ‘kujituliza’
Kwa
kawaida, mama anapojifungua, yeye hudaisha vitu kadhaa anavyohisi kwamba
mwili unahitaji ili kuwa imara. Baadhi ya vitu hivyo ni chakula.
Shida ni
kuwa, vingi vya vyakula hivyo huwa na sukari, mafuta na bidhaa zingine
ambazo huongeza mafuta mwilini. Kwa mfano soda, keki, viazi, peremende
na bidhaa zilizotengenezwa kwa ngano. Ni sawa kuvila vyakula hivi,
lakini, vinafaa kupunguzwa muda uendavyo.
12- Kula vyakula vya mimea
Utafiti
unaonyesha kuwa vyakula vya mimea (sio nyama) vina mafuta kidogo na
madini mengi ya protini ya mboga. Hivyo basi, vinapunguza kuongezeka kwa
mafuta mwilini na kuzuia kunenepa.
Akina mama wanahimizwa kujiepusha na kula nyama wakati huu na kula vyakula vitokanavyo na mimea.
Baadhi ya vyakula hivyo ni:
- Mboga kama mchicha (spinach), sukuma wiki na kabichi.
- Matunda kama machungwa, maembe, mapapai, tikitiki maji, parachichi, mapera na mengineyo.
13- Kupunguza kiasi cha chakula
Mama
anakubalika kula chakula zaidi ya kawaida anapokuwa na mimba. Hii ni
kwasababu ana binadamu mwingine ndani yake mwenye mahitaji mengi. Hata
hivyo, baada ya kujifungua, anafaa kupunguza kiasi cha chakula alacho.
Kula
chakula ziada kinalifanya tumbo kuwa nzito na kukusanya mafuta. Hii
huchangia kwa tumbo kukaa likiwa nene au kuzidi kunenepa.
14- Kula kiamsha kinywa
Kiamsha
kinywa ni mojawapo wa mlo muhimu sana kwa mama aliyejifungua. Anapokula
kiamsha kinywa, mwili huchangamka na kusiaga chakula chote kikamilifu.
Mwili pia hukaa tayari kuvipokea vyakula vingine wakati wa mchana na
kuvisiaga vizuri.
Mwisho
kabisa, hakuna uwezekano wa mama kuhisi njaa kupita kiasi na kuchangia
kwake kula kupita kiasi. Kwa njia hii, tumbo la baada ya kujifungua
hupungua.
15- Kunywa maji baridi ya kutosha
Maji
husaidia mwili wa mama aliyejifungua kupona kwa haraka. Pili, maji
hujaza tumbo na kuzuia mama kula chakula kingi kupita kiasi. Hivyo basi,
anaweza kurejelea hali yake ya kawaida bila kuhisi njaa.
Kunywa
maji baridi kutasaidia kuchoma mafuta mwilini wakat mwili unapojikakamua
kuyapa joto. Hivyo basi, mafuta yanatolewa mwilini na tumbo kupungua.
Somo zuri sana. Kweli nimelifurahia
ReplyDelete