Monday, September 4, 2017

Hii ni hali inayoweza kujitokeza kwa mama mjamzito hasa katika kipindi cha umri wa mimba chini ya wiki ya 28. Baadhi ya sababu zinazoweza sababisha ni

i) Kutoka kwa mimba\

ii) Mimba nje ya mji wa uzazi

iii) Uvimbe ktk kondo la nyuma(placenta)

iv) Sababu za kienyeji

Leo ningependa tuiongelee kidogo maada ya utokaji wa mimba (Abortion) ikiwa ni moja ya sababu ya utokaji damu kwa mwanamke kwenye mimba changa.

Image result for kutokwa damu wakati wa ujauzito

Kutoka/kutolewa mimba (Abortion)

Hiki ni kitendo cha kutoa mimba kabla haijafikisha wiki ya 28 kutokana na sababu mbalimbali. Ikumbukwe kuwa katik anchi yetu kitendo cha kutoa mimba kwa makusudi ni kosa la jinai.

Ili kuzitambua sababu za kutoka kwa mimba ni vyema tukajua kwanza aina za utokaji wa mimba na ndipo tutajua na sababu zake.

Aina

Mimba inayotishia kutoka (Threatened abortion)

Hii ni mimba inayotihia tu kutoka ila haitatoka kama tahadhari zitachukuliwa mapema. Hii huwa na sifa zifuatazo;kutoka damu kidogo ukeeni na maumivu ya tumbo lakini njia (cervix) inakuwa haijafunguka.

Aina hii mara baada ya kuigundua inatakiwa mama huyu awe na mapumziko (bed rest) atumie dawa ya kutuliza maumivu na asifanye mapenzi.

Mimba ambayo ni lazima itoke( Inevitable abortion)

Hii ni mimba ambayo kwa namna yoyote ni lazima itatoka kwani njia ya kizazi huwa tayari imekwisha funguka na hivyo inaweza pelekea masalia ya mimba kutoka yote au kubakiza baadhi.


Mimba iliyotoka lakini imebakiza masalia yake (Incomplete abortion)

Huwa na sifa zifuatazo kwasababu ya yale masalia yaliyobakia;kutoka damu ya mabonge ukeni,maumivu ya tumbo,njia huwa imefunguka na mfuko wa uzazi huwa ni mdogo kuliko umri wa mimba

Mimba iliyotoka yote (Complete abortion)

Hii huwa imetoka yote bila kubakiza kitu
Image result for kutokwa damu wakati wa ujauzito

Mimba iliyotoka na kubaki uchafu ambayo imeshambuliwa na wadudu hususani bakteria (Septic abortion)

Hii inaweza tokana na mabaki ya mimba ambayo hajatolewa kitaalamu au kufanyika katika mazingira machafu na hivyo mama huyu atakuwa na homa, kutokwa damu kwa wingi, njia ya kizazi itakuwa wazi na atakuwa anatokwa na uchafu wenye harufu sehemu za siri.

Mimba kutoka mara kwa mara zenyewe ( Arbitual abortion)

Aina hii mara nyingi mimba zinakuwa zinatoka zenyewe na ni lazima iwe imejirudia zaidi ya mara 3 ktk historia ya mama.Ni muhimu sana kwa kila mama mjamzito kuhudhuria kliniki bila kujali hadhi yako.

Mimba ambayo imepoteza dalili zake ( missed abortion)

Inatokea kwa mama mjamzito kupoteza dalili za mimba wakati alikuwa mjamzito na tumbo lake la uzazi likawa dogo kuliko umri wa mimba.

Mimba inayotolewa kwa utaratibu wa kitiba ( therapeutic arbotion)

Hizi ni mimba ambazo zinatolewa kwa kitiba ili kunusuru maisha ya mama ama kutokana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaonekana kuhatarisha maisha ya mama. Hii inategemea sana maamuzi ya daktari na jinsi alivyoona.

Utoaji mimba usio salama/jinai/ (Unsafe/criminal abortion)

Utoji mimba hauruhusiwi katika nchi yetu na ndo maana unaitwa jinai lkini kitaalamu tunaita utoaji usio salama. Aina hii hufanyika kwa njia mbalimbali ambazo sitazitaja hapa kwasababu za kimaadili.

Makundi makubwa wanao fanya aina hii ambayo ni hatari kwa mtoaji na mtolewaji huwa ni wake za watu wasio waaminifu kwa ndoa zao, wanafunzi, wanaotumia vibaya uzazi wa mpango, waajiriwa wapya kama masharti ya kazi yamekataa, wanaotoka familia zenye misimamo mikali ya kidini lakini wao wamekiuka imani zao na wale wa mimbba zisizotarajiwa.

Hatari za utoaji mimba

zinazofahamika ikiwa ni pamoja na kupasua tumbo la uzazi, kutokwa damu nyingi na kupata maambukizi

Matibabu

Ni muhimu sana kumwona daktari hospitali au kliniki inayofahamika kisheria na utaratibu na si maduka ya madaw.

#jamiiforum

Sunday, August 27, 2017

Magonjwa ya zinaa ni magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiyana (sexually transmitted diseases),inayosababishwa na bakteria,virus au fungus wanaopenda ishi sehemu ya maji maji au unyevu unyevu katika mwili ,kama mdomoni,kooni,sehemu za siri au sehemu ya hajakubwa.

Iwapo mtu atakutana kimwili na mtu mwenye maambukizi hapo ni rahisi kuambukizwa. Magonjwa ya zinaa yanampata mwanamke na mwanaume pia kwa njia ya mdomo,uuke au uume.

Magonjwa ya zinaa yapo ya aina tofauti kuna

Kaswende

Kisonono

Gonorea

Ukimwi

Klamidia

Malenge lenge sehemu za siri

Dutu za sehemu ya siri

Magonjwa ya zinaa ni hatari kwa afya ,mama mjamzito akipata ugonjwa wa zinaa atapata dalili tofauti tofauti kama zifuatazo

Kuvimba sehemu za siri

Maumivu makali pindi ufanyapo mapenzi au wakati wa kukojoa

Kupata homa

Kutokwa vijipele ukeni vinaweza kuuma au visiume

Kupungua uzito

Maumivu ya mgongo

Kutokwa majasho kwa wingi nyakati za usiku

Kutokwa maji maji ukeni yenye harufu au isio na harufu

Kutokwa damu au usaha ukeni

Kuwashwa sana

Uke kubadili rangi

Madhara ya magonjwa ya zinaa kwa mama na mtoto

Mtoto anaweza kupata upofu

Uziwi-kushindwa mtoto kusikia

Mwanamke au mwanamme anaweza kuja kushindwa kuzaa sababu ugonjwa utaenda kuadhiri sehemu za uzazi

Kuziba mirija ya uzazi

Kifo

Ulemavu kwa mtoto

Mtu kupoteza kinga ya mwili kuwa dhoofu,kuumwa mara kwa mara.

Tiba

Magonjwa ya zinaa yanatibika iwapo  yatatibiwa mapema isipo kuwa ukimwi peke yake hauna tiba,mambukizi mengine mama mjamzito atatibiwa kwa kupewa antibiotic, mtoto  iwapo ataadhirika kipindi mama yake anamimba  baada ya kuzaliwa atawekwa dawa machoni ya kusafisha na kutibu.

 MTOTO ALIEPATA MAAMBUKIZI KUTOKWA KWA MAMA ,KAWEKEWA DAWA MACHONI

Iwapo mama amegundulika anamaambukizi na muda wa kijifungua umekaribia itabidi azalishwe kwa c-section ( operation)ili kumwepusha mtoto kupata maambukizi.

 

U.T.I / fungus ni magongwa ya infection nayo yanaweza mpata mama ila yenyewe hupati kwa njia ya kujamiiana haya yanatokana na virus na bakteria pia ambao unaweza watoa vyoo vya public au nyumbani iwapo mkiwa hamsafishi vyoo vizuri na kutumia maji safi ya kujitawazia.

 Uwapo mjamzito yakupasa kuwa makini Na kila hali.

Wednesday, August 23, 2017

 Image result for maumivu makali wakati wa hedhi
Kuumwa tumbo wakati wa hedhi

Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo. Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation.

Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili. Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.

Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
Karibu nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia 15 wanasema kuwa hupata maumivu makali. Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.
• Kuwa na umri wa chini ya miaka 20.
• Kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo.
• Kutoka na damu nyingi wakati wa hedhi. (suala hilo linaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali ya kitiba).
• Wanawake ambao hawajawahi kuzaa.
Maumivu ya Tumbo la Hedhi... Sehemu ya Pili
kukasababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:
• Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hta sehemu nyinginezo.
• Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaoota katika mfuko wa uzazi.
• PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.
• Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
• Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

Baada ya kujua baadhi ya matatizo ya wanawake yanayoweza kusabibisha hedhi inayoambatana na maumivu ya tumbo, hebu sasa na tuzijue tumbo la mwezi linaumaje?
1. Maumivu mara nyingi si makali.
2. Muumivu huja na kuondoka, na kwa kiwango tofauti (spasmodic).
3. Maumivu zaidi huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo.
4. Huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongoni ambayo husambaa mpaka mapajani.
5. Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.
6. Kupata choo kilaini au hata kuharisha.
7. Kufunga choo.
8. Tumbo kuwa kubwa au kuwa gumu.
9. Kuhisi maumivu ya kichwa.
10. Kutojihisi vizuri au kujisikia kuchoka.

Inapasa kujua kuwa, kiwango cha maumivu ya tumbo la hedhi na mchanganyiko wa dalili inategemea mtu na mtu, mtu mwingine anaweza akawa anapata karibu dalili zote nilizozitaja hapo juu na mwingine ni baadhi tu au hata dalili moja. Wanawake wengi hutambua wanapopata tumbo la hedhi bila hata msaada wa daktari. Wanawake wanashauri iwapo watapata maumivu makali sana ni bora
wakamuone daktari ili wafanye vipimo kama vile Ultrasound, CT na CT-Scan, MRI na vinginevyo ili kufahamu iwapo **** matatizo mengine ya kitiba yanayosababisha maumivu hayo kuwa makali.
Matibabu ya maumivu ya tumbo la hedhi kwa kawaida huweza kutibika kwa urahisi kwa kutumia vidonge vya kupunguza maumivu, kama vile Ibuprofen, naproxen au aina nyinginezo za vidonge visivyokuwa na steroids (NSAIDS).

Pia kuna wakati madaktari wanaweza kumshauri mgonjwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba, Vidonge hivyo huzuia mzunguko wa yai au Ovulation na kupunguza ukali wa maumivu ya tumbo la hedhi.
Kuna baadhi ya tiba za mitishamba pia ambazo husadia kupunguza muamivu ya tumbo la hedhi. Hapa namaanisha herbal, wenzetu Wachina ni watalamu wazuri katika ujuzi huo. Vilevile wanawake washauriwa kufanya baadhi ya vitendo ambavyo hupunguza maumivu
hayo, baadhi ya hivyo vimetaja kama kuoga maji moto, kutumia hot bottle na hata kuweka kitambaa chenye joto katika sehemu ya chini ya tumbo. Kuna baadhi husaidia kwa kufanya mazoezi kama yoga, meditation, kusuliwa, tiba ya sindano (Acupunture), TENS au kushituliwa
mishipa ya fahamu ( Transcitaneous Electric Nerve Stimulation na hata wengine husaidiwa kwa tendo la kujamiiana. Vilevile kutumia vidonge vya vitamin E, Thiamine na Omega 3 kumetajwa kuwa husaidia katika suala hilo. Wanawake wanaopatwa na matatizo kama hayo ni bora wapumzike vyema na kupata usingizi wa kutosha.

Tunaelezwa kuwa tunaweza kujiepusha na kupatwa na maumivu ya tumbo la mwezi kwa kufanya yafuatayo:
Kujitahidi kula matunda, mbogamboga na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi, pombe, cofeini, Sodium na sukari.
Kufanya mazoezi.
Kujiepusha na wasiwasi na mawazo.
Kuepuka kufuta sigara.
SOURCE JAMII FORUMS

Sunday, August 20, 2017

Miongoni mwa vitu vikubwa ambavyo humtisha mwanadamu, yawezekana kifo kikawa ni namba moja, Ukifuatilia kwa ukaribu hali ambazo husababisha vifo ni pamoja na ajali, jinsia, majanga mbalimbali, umri, imani pamoja na magonjwa.

Hata hivyo vifo vitokanavyo na magonjwa ndio huchukua nafasi kubwa sana, Je umeshawahi kujiuliza upo salama kiasi gani ? Kutana na orodha ya magonjwa ambayo husababisha sana vifo !
    

1.Lower respiratory diseases(magonjwa ya chini ya upumuaji)
magonjwa Haya huathiri mfumo wa upumuaji wa chini kutokea kwenye trachea,bronchi na mapafu mfano wa magonjwa haya ni pneumonia, majipu kwenye mapafu(lung abscesses) na bronchitis (uvimbe kwenye bronchi).
Mwaka 2015 kulikuwa na wagonjwa milioni 291 na ulisababisha vifo million 2.74
Magonjwa Haya husababishwa na virusi au bakteria.

2.Magonjwa ya kuhara
Ni gonjwa la kwa kuua watu katika nchi znazoendelea hasa watoto chini ya miaka mitano, kila mwaka watoto chini ya miaka mitano 525000 hufariki kutokana na magonjwa haya.
Magonjwa haya yanatibika na kuzuilika, huweza kuyazuia kwa kunywa maji safi na usafi kwa ujumla.

3.Kiharusi
Kiharusi hutokana na sehemu ya ubongo kukosa damu na oksijeni kutokana na kuziba kwa mishipa ya ateri ya damu au kupasuka kwa mishipa ya damu.
4.Ischaemic heart disease
Huu ni ugonjwa wa moyo unaotokana na mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo kuziba kutokana na rehemu(cholesterol) kugandia kwenye mishipa ya damu ya moyo.

5.Ukimwi
Kwa mwaka 2016 inakadiriwa kulikua na vifo milioni 1 vilivyosababishwa na sababu zinazoambatana na VVU,pia inakadiriwa watu milioni 36.7 walikuwa wakiishi na VVU duniani.

6.Kifua kikuu
Mwaka 2015 watu milioni 10.4 waliugua TB na watu milioni 1.8 walikufa kutokana na TB,laki 4 kati ya hao walikua na VVU
Asilimia 95 ya vifo vya TB hutokea katika nchi zinazoendelea.

7.Malaria
Shirika la afya duniani (WHO) linakadiria mwaka 2016 watu milioni 212 walikua na malaria huku watu 429,000 wakifa kwa malaria,
Malaria husababishwa na plasmodium na kuenezwa na mbu.

8.Preterm birth
Watoto ambao huzaliwa kabla ya miezi 9 ya ujauzito,inakadiriwa watoto milioni 15 huzaliwa kabla ya miezi 9 kila mwaka.
Kuzaliwa kabla ya miezi 9 ya ujauzito ni kati ya sababu zinazoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

9.Birth asphyxiation
Hii ni hali inayotokana na kukosa oxygen watoto kwa muda mrefu pindi wanazaliwa, hivyo husababisha matatizo ya kimwili hasa ubongo.
Asilimia 99 ya vifo hivi hutokea katika nchi zinazoendelea.

10.Ajali za barabarani.
Watu milioni 1.25 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za barabarani .
Ajali ndio huongozaa kwa kuua watu wenye umri wa miaka 15 hadi 29 huku asilimia 90 ya vifo hivi hutokea katika nchi zinazoendelea.

Bara la Africa ndio muhanga mkubwa wa vifo hivi na hii ni kutokana na uhaba wa wataalamu, vitendea kazi na utambuzi wa thamani ya mwili kwa binadamu mwenyewe, hata hivyo ikiwa u miongoni mwa wagonjwa wa magonjwa tajwa hapo juu, usikihofie kifo cha msingi zingatia ushauri wa wataalam au fika hospital mapema iwezekanavyo.

Zingatia ajali zinaua.

Sunday, August 6, 2017

 Image result for kalenda ya hedhi
Faida ya kutumia njia hiyo  

  
•Haina madhara yeyote ya kimwili. 
Matatizo yanayoweza kujitokeza 

•Njia ya kalenda si kinga dhidi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.
 
•Njia hii ni ngumu na inahitaji wanawake kuwa wastadi katika hisabati, na kuwa waangalifu sana kuandika au kukumbuka tarehe ya kuanza kipindi chao cha hedhi cha mwisho.
 
•Huchukua muda mrefu (miezi 3 hadi 6) kufahamu urefu wa mzunguko cha hedhi.
 
•Mzunguko wa hedhi huweza kubadilika wakati wowote kufuatana na mabadiliko katika mwili.  Hii huweza kusababisha tarehe ya yai kupevuka kuwahi au kuchelewa, kwa hiyo mwanamke huweza kujiweka katika hatari ya kupata mimba bila kufahamu. 
 
•Ili njia hii iwe na uhakika, mwanamke hawezi kufanya mapenzi katika siku zake 9 kila mwezi ambapo kuna uwezekano wa yeye kupata mimba.  Kwa hiyo njia hii inahitaji uwezo mkubwa wa kujidhibiti na hufanya kazi vizuri iwapo mwanaume namwanamke wamekubaliana kufanya hivyo kwa pamoja, na mwanaume anamsaidia mwanamke kuhesabu au kuandika urefu wa mzunguko wake wa hedhi.  
 
•Kwa sababu urefu wa mzunguko wa hedhi wa mwanamke huweza kubadilika ghafla bila kutegemea, hata kama inatumika inavyotakiwa, njia hii si nzuri kama njia nyingine zilizotajwa kuzuia mimba na kupanga uzazi.
Image result for kalenda ya hedhi
WASICHANA wengi hasa walio na uwezo wa kushika mimba ambao wanasoma au hawajaolewa wamekuwa wakijihusisha na matukio ya kutoa mimba mara kwa mara bila kufikiria athari za kutoa mimba kwa uzito.
Athari hizo ni pamoja na kuweka maisha hatarini, kuharibu kizazi, kujiweka katika hatari zaidi ya kupata maradhi kama Saratani ya Shingo ya Kizazi, kushitakiwa na nchi kwa kosa la kuua pamoja na kuharibu uhusiano wao na Mungu.Machaguo ya Kuzuia Mimba kwa Vijana walio Masomoni :-
Kusubiri wakati unaofaa
Vijana wanatiwa moyo kusubiri na dini zao na walezi wao, ingawa hata serikali ina sheria zinazopendekeza umri sahihi kujihusisha na ngono. Kijana anaweza kuamua kibinafsi kusubiri muda muafaka na kuwa na mtu sahihi.
Kusubiri kutakuweka salama na bila wasiwasi wowote wa kuambukizwa magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya ngono. Kuwa salama kutakufanya kukazia malengo yako ya maisha.
Maamuzi ya kusubiri wakati unaofaa hakutakufanya mihemko ya ngono kupotea bali itakubidi kukazia fikra mambo ya msingi katika maisha yako badala ya kuwaza ngono.
Ngono salama
Waopendwa wasomaji wa Gazeti hili mtandao la FikraPevu hapa ninamaana ya kutumia njia ambazo zinazopunguza uwezekano wa kupata mimba au magonjwa ya ngono ukitia ndani Virusi vya UKIMWI (VVU). Mihemko ikikuzidi na ukashindwa kusubiri wakati unaofaa kuanza ngono ni bora kujilinda wewe na mwenzi wako kwa kutumia kinga.
Mipira (Kondom) ndio njia pekee itakayokukinga usipatwe na ujauzito na magonjwa ya ngono ikiwemo VVU, wakati huo huo hutumika kama njia ya uzazi wa mpango.
Vidonge vya dharura vya Uzazi wa Mpango
Ikitokea umefanya ngono bila kinga ya kondom hasa kwa mtoto wa kike ambaye hakuwa anatumia njia za uzazi wa mpango inashauriwa kutumia vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango ili kuzuia mimba isiyotarajiwa ingawa vidonge hivyo havitasaidia kupunguza hatari ya kuambukizwa na magonjwa ya ngono ikiwemo VVU.
Vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango ni vidonge vya vya uzazi wa mpango ambavyo ni vya aina kuu mbili, vidonge vyenye vichocheo viwili vitwavyo Estrojeni na Projesteroni na vidonge vyenye kichocheo kimoja tu cha Projesteroni.

Vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango vipo vya aina tofauti na zina nguvu tofauti, kuna zinazopaswa kutumika ndani ya masaa 72 (Siku 3) baada ya ngono isiyo salama na kuna zinazopaswa kutumika ndani ya masaa 120 (Siku 5) baada ya ngono isiyo salama.

Aina zote za vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango hufanya kazi ya kuzuia mimba kwa kuzuia Ouvuleshaji ambapo huzuia au kuchelewesha yai kutoka kwenye kokwa (Foliko za Graaf) zilizomo katika Ovari.

Katika hali zisizotarajiwa, mabinti hubakwa na watu wasiowafahamu hali zao za afya. Ikiwa umetokewa na hali hiyo tafuta ushauri wa kitiba haraka sana. Katika hali hiyo unaweza kumeza vidonge vya dhalula ndani ya saa 72 hadi 120 tangu ulipofanya ngono ili kuzuia mimba. Pia daktari anaweza kukupima VVU na kukupa vidonge vitakavyo kukinga na VVU ikiwa haijulikani hali ya VVU ya mbakaji.

Vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango vinaweza kutumika kabla ya ngono isiyo salama kama una hofu na njia ya uzazi wa mpango unayotumia sasa, kama unaenda likizo na hutoweza kupata vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango. Muulize daktari au muuguzi ili upate taarifa kamili kuhusu kutumia vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango kabla ya ngono isiyo salama.

Baada ya kutumia vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango ikiwa hedhi yako itachelewa zaidi ya siku 7 au ni nyepesi au ya muda mfupi sana wasiliana na mtaalamu wa afya ili kupima mimba kwanza.

Athari zinazojitokeza mara kwa mara baada ya kutumia vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango ni pamoja na maumivu ya tumbo, kuumwa kichwa, hedhi kubadilika badilika inaweza kuwa matone tu au nyingi zaidi, kujihisi uchovu na kuumwa.

Athari zinazojitokeza kwa uchache ni pamoja na matiti kujaa na kuuma, kizunguzungu na kutapika. Ni busara kuwasiliana na mhudumu wa afya ya uzazi ikiwa utapatwa na dalili zisizo za kawaida.

Vidonge vya dhalula vya uzazi wa mpango vinaathiriwa na dawa zingine kama za kutibu Kifafa, VVU, Kifua Kikuu na Vidonda vya Tumbo. Hivyo wasiliana na mtaalamu wa huduma za uzazi wa mpango kabla ya hujatumia vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango.

Kitanzi (Intrauterine Device)

Kitanzi kinaweza kuwekwa kwenye uterasi ogani ambamo utungo wa mimba hupokolewa na kustawishwa ndani ya masaa 120 (Siku 5) baada ya ngono isiyo salama au siku 5 kabla ya Ouvuleshaji. Kitanzi kinaweza zuia yai kurutubishwa na mbegu ya kiume. Wanawake chini ya asilimia 1 wanaotumia kitanzi ndio wanaweza kupata mimba.

Kitanzi ni kifaa kidogo chenye umbo la T kilichotengenezwa kwa plastiki na kopa (Copper). Kifaa hiki huingizwa kwenye uterasi/kizazi (ogani ambamo utungo wa mimba hupokelewa na kustawishwa) na mtaalamu wa afya mwenye utaalamu huo. Kifaa hiki kinafanya kazi kwa kuzuia yai kurutubishwa na mbegu ya kiume (manii).

Kuna aina nyingi za Vitanzi. Aina mpya zina kopa zaidi na zina ufanisi zaidi ya asilimia 99. Wanawake chini ya wawili kati ya wanawake 100 wanaotumia aina mpya kwa zaidi ya miaka 5 ndio wanaoweza kupata mimba. Vitanzi vyenye kopa kidogo vina nguvu kidogo ukilinganisha na vyenye kopa nyingi ila bado vinaweza kuzuia mimba.

Ikiwa umefanya ngono isiyo salama, kitanzi kinaweza kuwekwa ndani ya siku 5 baada ya ngono isiyo salama na kuweza kuzuia mimba. Ni njia madhubuti ya kuzuia mimba kuliko vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango na pia hakiingiliani na dawa zingine. Unaweza pia kuamua kukiacha kama njia yako ya uzazi wa mpango.

Mara nyingi wanawake wengi wanaweza kutumia kitanzi kwa kukiingiza ndani ya uke na wale ambao hawakuwahi kushika mimba, wanaonyonyesha na wale wenye VVU. Mtaalamu wa afya ya uzazi atakuuliza juu ya historia yako ya matibabu ili kufahamu kama kitanzi kitakufaa.

Hupaswi kutumia kitanzi kama una ugonjwa wa zinaa au maambukizi kwenye via vya uzazi, ukiwa na kasoro ya maumbile kwenye mlango wa uzazi au unatokwa na damu ukeni hasa baada ya tendo la ndoa au baada ya hedhi. Wanawake waliopata mimba nje ya fuko la kizazi au walio haribu mimba hivi karibuni au wanaotumia vifaa bandia vya moyo wanapaswa kuwasiliana na daktari kabla ya kuwekewa kitanzi.

Athari za kutumia kitanzi ni chache ila mtu anaweza kupata maumivu, maambukizi ya njia ya mkojo na kizazi. Kama utatumia kitanzi kama njia yako ya uzazi wa mpango, kitafanya siku zako za hedhi kuwa nyingi zaidi pamoja na kutokwa na hedhi nyingi na maumivu zaidi. Kama unahisi vibaya au maumivu baada ya kuweka kitanzi, kutumia dawa za kutuliza maumivu zinaweza kutumika kupunguza tatizo.

imeandikwa na TAZAMA LINE

Saturday, August 5, 2017

Hivi ni baadi ya vyakula ambavyo mama mjamzito au mwanamke anaejiandaa kubeba ujauzito HARUHUSIWI kuvitumia katika kipindi cha ujauzito.

*Nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri, nyama za aina hii husemekana kuwa na bacteria ambao huwezakusababisha ujauzito kutoka au kuzaa mtoto mwenye ulemavu wa kuzaliwa

*Maziwa ya mgando au maziwa ambayo hayajachemshwa, maziwa ya aina hii husemekana kuwa na bacteria ambao wanaweza hatarisha maendeleo ya ujauzito

*Vinywaji vyenye caffeine kama vile kahawa, chai, coca cola na vingine vya asili hiyoMayai mabichi, husemekana kuwa na bacteria wanaoweza kuhatarisha maendeleo ya ujauzito.

*Samaki wabichi wa maji chumvi au samaki waliovuliwa kwa kutumia sumu.

*Vyakula laini na vyenye sukari nyingi kama soft cheeses, cake, chocolate n.k.

*Unywaji wa pombe

*Kula mboga za majani au matunda bila kuyaosha

*Ulaji wa maini
Katika kipindi cha ujauzito au katika maandalizi ya kubeba ujauzito mwanamke anatakiwa kula vyakula vya aina mbalimbali vilivyoandaliwa vizuri na kupikwa vikaiva inavyotakiwa, ulaji wa vyakula mbalimbali katika makundi ya vyakula kabla ya ujauzito au katika kipindi cha ujauzito husaidia kuupa mwili na mtoto virutubisho mbalimbali vilivyo na umuhimu katika kujenga na kulinda mwili.

Zingatia upate mafanikio bora.

Thursday, August 3, 2017

fahamu kuhusu fistula

Fistula ni nini
Fistula ni shimo ambalo hutokea kati kati ya kibofu cha mkojo na uke au kati kati ya njia ya haja kubwa na uke wa mwanamke ambaye amejifungua kwa shida. Shimo hutokea pale ambapo kichwa cha mtoto ni kikubwa kuliko njia ya uzazi.

Ina sababishwa na nini?
Inasababishwa na  kusukuma mtoto wakati wa kujifungua kwa mda mrefu bila usaidizi au matibabu yeyote, na ana chanika  katika njia ya uzazi na kusababisha shimo, hivyo husababisha uvujaji wa kinyesi na mkojo bila kujizuia. 
Kuzaa mapema kabla ya umri kumekuwa chanzo kikubwa cha kutokea fistula, hilo linatokana na kutopevuka kwa njia za uzazi pamoja na nyonga.

 Kwenda Kliniki
Wataalamu wa afya wanabaini fistula mara nyingi hutokea kwa wanawake wanaojifunglia majumbani baada ya kukosa matibabu. Ni Sahihi mara kwa mara kwa wajawazito kujifungua katika kituo cha matibabu ambapo unaweza kufuatiliwa na kupata huduma za matibabu kwa wakati ni muhimu

.Nifanye nini ikiwa nina fistula?

Kama unahisi kutokwa na mkojo bila kujizuia, harufu mbaya, maumivu makali sahemu za uzazi unashauliwa kuwahi hospitali au kituo cha afya kilipo karibu ili upate ushauri na matibabu zaidi,

Matibabu

Matibabu ya fistula ni bure katika hospitali zote nchini.

Wednesday, August 2, 2017

Usafi Ni afya, imezoeleka Mara kwa Mara kutolewa mafunzo ya namna ya kuswafi uke lakini pasipo kusisitiza kuwa uume nao unapaswa kusafishwa ili kuweka hali ya usafi Na kuepusha mambo mengi ikiwapo magonjwa.

Kwako mwanaume Fanya hivi kusafisha uume wako.

Mgegedo ni tafsida nimeitumia kama kiwakilishi cha maumbile ya mwanaume yaani uume. Mgegedo ni eneo muhimu sana kwawanaume ambalo wanalitukuza kuliko kitu chochote hapa duniani, hivyo leo hiinimeona ni vyema kutoa darasa kwa wanaume ili wajue namna nzuri ya kutunza migegedoyao ili iwe misafi na yenye afya kwa ustawa wa mahusiano yao na wenzi wao.

Ni vyema wanaume wakajengautaratibu wa kuweka migegedo yao katika hali ya usafi unaostahili kwa ajili yakujenga mahusiano mazuri na wenzi wao inashauriwa kuosha mgegedo kwamakini kwa kutumia maji ya uvuguvugu kila siku mwanaume anapooga, kama mwanaumeatakuwa hajatahiriwa, basi anatakiwa kuigeuza ile ngozi inayofunika sehemu yambele ya mgegedo wake na kuisafisha kwa makini ili kuondoa ukando kando unaokuwaumeganda ndani unaofanana na jibini ambapo ukando kando huo hufahamikakitaalamu kama smegma.

Huu ukando kando unaopatikanandani ya migegedo ya wanaume wasiotahiriwa ni kilainishi maalum kinachoufanyamgegedo usiwe mkavu,kilainishi hiki ni cha kimaumbile.

Kama kilainishi hiki kikiachwabila kusafishwa kwa muda mrefu kitaanza kutoa harufu mbaya na baadayekitazalisha vijidudu (bacteria) ambavyo vitasababisha mgegedo kuvimba na kuwamwekundu sehemu ya mbele ambapo tatizo hilo hufahamika kitaamu kama balanitis.

Mwanaume asiyetahiriwa asiyesafishamgegedo wake vizuri licha ya kupatamatatizo niliyoyaeleza hapo juu lakini pia huweza kuharibu mahusiano yake namwenzi wake. Hakuna mwanamke ambaye atapenda kujinafasi kwa kulamba koni yamgegedo usio msafi, kwani ni kujitafutia fangasi za kinywa.

Hata hivyo ningependa kuwaonya kina mama kamwe wasijaribu kuigeuza ngozi ya migegedo ya watoto wao wadogo ambao hawajatahiriwa, kwani hiyo inaweza kuwaumiza na kuwasababishia maumivu makali. Kwa kawaida ngozi ya mbele ya migegegdo ya watoto wadogo inakuwaimeshikana na kichwa cha mgegedo hivyo haiwezi kuvutika yote na ukilazimisha unaweza kumjeruhi. Kwa watoto wadogo katika makuzi yao hawahitaji kusafishwa migegedo yao kwa namna hiyo. 

Lakini pia pamoja nakwamba usafi ni muhimu lakini haishauriwi kusafisha migegedo kwa kiwangokilichopitiliza kwa kutumia sabuni ya kipande au ya maji kunaweza kusababisha muwasho na uvimbe kwenye mgegedo hususani kwa wanaume wasiotahiriwa.Kwa kusafisha mgegedo mara mojakwa siku kwa maji ya uvuguvugu inasaidia kuiweka migegedo katika hali ya usafi kiafya. Na kama unataka kutumia sabuni, ni nyema kutumia sabuni zisizo za manukato yaani wengine huita sabuni mbuni au sabuni ya kipande. Kwa kutumia sabuni za manukato unaweza kusababisha muwasho na uvimbe wa ngozi wa mgegedo wako.

Usafi wa eneo la korodani za mgegedo

Kuzungumzia usafi wa mgegedo sikwamba nimesahau kuzungumzia usafi wasehemu ya chini ya mgegedo yaani korodani. Eneo la korodani lisipofanyiwa usafi makini lile jasho na nywele za chini husababisha harufu Fulani yenye kukera. Eeneo la korodani linatakiwa kufanyiwa usafi makini hasa kwa wale wanaovaa nguo za ndani muda wote kwa siku nzima. Ni vyema kuhakikisha eneo lachini la korodani karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa inakuwa safi wakatiwote ili isiwe na harufu isiyovutia.

Saturday, July 29, 2017

Kisa hiki cha kusisimua kitakufanya ujifunze jambo, soma mpaka mwisho ujifunze.

Wakati Terry Gobanga, wakati huo akiitwa Terry Apudo alipotoweka katika harusi yake hakuna mtu aliyedhani kwamba alitekwa nyara ,kubakwa na kutuwa kandakando ya barabara akipigania uhai.

Lilikuwa janga la kwanza kati ya mawili kumkabili muhubiri huyo kijana .Lakini ni manusura.

Harusi iliopangwa ilitarajiwa kuwa harusi kubwa.

Nilikuwa muhubiri hivyobasi wanachama wote wa kanisa walitarajiwa kuhudhuria.

Mchumba wangu ,Harry na mimi tulikuwa na furaha tulikuwa tunafunga ndoa katika kanisa la All Saints Cathedral mjini Nairobi na nilikuwa nimekodisha rinda zuri sana la harusi.

Lakini usiku kabla ya ndoa yetu ,niligundua kwamba nina baadhi ya nguo za Harry .

Hakuweza kuja katika harusi bila tai kwa hivyo rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa amekubali kubaki nami usiku wa kuamkia harusi alikubali kumpelekea mapema alfajiri.
Niliamka mapema na kumpeleka hadi katika kituo cha kupanda basi.

Nilipokuwa nikirudi nyumbani ,nilipita karibu na mtu mmoja ambaye alikuwa ameketi kati boneti ya gari na akanishika kutoka nyuma na kuniingiza katika viti vya nyuma vya gari hilo na kuondoka mahali hapo.

Yote haya yalifanyika katika chini ya sekunde moja .Nilifunguliwa mdomo na kuwekwa kipande cha nguo mdomoni.

Nilikuwa nikirusha mikono na miguu nikitaka kupiga kelele.Nilipofanikiwa kutoa kitambara hicho nilipiga kelele: Ni siku yangu ya harusi! hapo ndipo nilipopigwa ngumi .

Mmoja ya wanaume hao wakaniambia nishirikiane nao ama niuwawe.Wanaume hao walinibaka kwa zamu .

Nilihisi nitafariki ,lakini bado niliendelea kupigania uhai wangu, hivyobasi mtu mmoja alipotoa kitambara kilichokuwa mdomoni mwangu nilimuuma uume wake.

Alipiga kelele kwa uchungu na mmoja wao akanidunga kisu tumboni.

Baadaye walifungua mlango na kunitupa kando ya barabara huku gari likiendelea kwenda.Nilikuwa mbali na nyumbani ,nje ya jiji la Nairobi .

Ilikuwa zaidi ya saa sita baada ya kutekwa.Mtoto mmoja aliniona nikirushwa nje ya gari na akamweleza bibiye.

Watu walikuja mbio .Wakati maafisa wa polisi walipokuja walijaribu kuangalia iwapo bado ninapumua ,lakini hawakupata.

Wakifikiri nimefariki walinitia katika blanketi na kuanza kunipeleka katika chumba cha kuhifadhi maiti .

Lakini njiani nilikohowa. Polisi mmoja alisema: Bado hajafariki ,hivyobasi wakabadilisha njia ya kuelekea katika chumba cha kuhifadhi maiti na kunipelekea katika hospitali kuu ya serikali nchini Kenya.

Niliwasili nikiwa na mshangao mkubwa, nikizungumza mambo nisioelewa.Nilikuwa nusu uchi nikivuja damu huku sura yangu ikiwa na majeraha kutokana na kipigo nilichopata.
Lakini kuna kitu kimoja kilichomshtua mwanamke aliyekuwa akisimamia matibabu ,kwa sababu aligundua mimi ni bibi harusi.

''Twendeni kanisani tuone iwapo wanamkosa bibi harusi'', aliambia wauguzi.

Kwa bahati kanisa la kwanza waliloulizia ni All Saints Cathedral jijini nairobi ambapo waliambiwa kwamba kulikuwa na harusi mwendo wa saa nne Asubuhi lakini bibi harusi hakuonekana.

Wakati nilipokuwa nikisubiriwa kuingia kanisani ,wazazi wangu walikuwa na wasiwasi.

Watu walitumwa kunitafuta .Kulikuwa na uvumi. Wengine walishangazwa. Je alibadili nia? Wengine walisema haiwezekani kwamba yeye alifanya hivyo.

Baada ya saa chache walilazimika kuondoa mapambo ili kutoa nafasi kwa sherehe ya pili.

Harry alikuwa amewekwa katika eneo moja ambapo alikuwa akisubiri.Wakati waliposikia kule nilikokuwa wazazi wangu waliwasili katika hospitali wakiwa na watu wote

.Harry alikuwa akibeba rinda langu la harusi. Vyombo vya habari vilikuwa vimeambiwa kuhusu kisanga hicho na pia viliwasili katika hoispitali.

Nilipelekwa katika hospitali nyengine ambapo nilipata haki yangu ya faragha.

Hapo ndipo madaktari waliponishona na kunipa habari mbaya. Jereha la kisu katika tumbo langu lilikuwa ndani ya kizazi changu.
Kwa hivyo hutaweza kushika mimba''.Nilipewa dawa ya kuzuia mimba pamoja na ile ya kuzuia virusi vya ukimwi.

Ubongo wangu ulikataa kukubali kile kilichotokea. Harry aliendelea kusema kuwa angependa kufunga ndoa nami.

''Nataka kumuuguza ili kuhakikisha kuwa anapata afya njema, katika nyumba yetu'',alisema.

Ukweli usemwe, sikuwa katika hali ya kuolewa ama kukataa kwa sababu akili yangu ilikuwa imejawa na nyuso za watu watatu walionibaka na kila kitu kilichotokea.

Siku chache baadaye, wakati nilipoanza kupata fahamu niliweza kumuangalia katika macho yake.

Niliendelea kusema pole. Nilihisi kana kwamba nilikuwa msaliti.

Watu wengine walisema kuwa ilikuwa tatizo langu kwa kuondoka nyumbani alfajiri. Iilkuwa uchungu mwingi sana lakini familia yangu na Harry walinisaidia.

Polisi walishindwa kuwakamata wabakaji. Nilienda katika gwaride la kuwatambua watu hao katika vituo vya polisi lakini sikufanikiwa na nilihisi uchungu kila wakati nilipoenda.
Mwishowe nilienda katika kituo cha polisi na kusema ''Wajua nini'': Sitawahi kurudi tena nataka kuachana na tatizo hilo.

Miezi mitatu baada ya shambulio hilo niliambiwa sikuwa na viini vya ukimwi na nikafurahia sana, lakini wakaniambia ni sharti nisubiri miezi mitatu baadaye nithibitishe.

Lakini mimi na Harry tayari tulikuwa tumeanza mipango ya harusi yetu ya pili.

Ijapokuwa nilikasirishwa na vyombo vya habari ,mtu mmoja alisoma habari yangu na kutaka kukutana nami.

Jina lake ni Vip Ogolla ambaye pia naye alikuwa manusura wa ubakaji.

Tulizungumza na aliniambia kwamba yeye na rafikize walitaka kunifanyia sherehe.''Jiachilie fanya chochote utakacho'',alisema.

Nilichagua keki ya aina yake .Keki ya ghali. Mbali na rinda ambalo lilikuwa nimekodisha sasa nilinunua na kuwa langu.

Mnamo mwezi Julai 2005, miezi saba baada ya mipango ya harusi yetu ya kwanza, mimi na Harry tulifanikiwa kufunga ndoa na tukaenda katika kusherehekea fungate yetu.
Siku 29 baadaye tulikuwa nyumbani wakati wa msimu wa baridi kali usiku mmoja.

Harry aliamua kuwasha jiko la makaa na kulipeleka katika chumba chetu cha kulala.

Baada ya chakula cha jioni aliliondoa kwa sababu chumba chetu kilikuwa na joto.

Nilijiingiza chini ya shiti huku yeye akifunga mlango.Wakati alipokuja kitandani aliniambia anahisi kisunzi, lakini hatukufikiria sana kuhusu hilo.

Ilikuwa baridi sana na hatukuweza kulala hivyobasi nilichukua blanketi jingine.

Lakini Harry akasema hakuliona kwa sababu hakuwa na nguvu nyingi. Mimi nami sikusimama.

Tulihisi kwamba kuna kitu kibaya.Tulilala nakumbuka nikimuita, mara nyengine aliitikia mara nyengine hakuitika.

Nilijilazimisha kushuka kitandani ambapo nilitapika na kupata nguvu .Nilitambaa hadi katika simu.

Niliwaita majirani zangu nikawaambia kwamba kuna kitu kibaya mume wangu haitiki.

Alikuja haraka, lakini ikanichukua muda mrefu kutambaa hadi katika mlango wa mbele ili kumfungulia huku nikiendelea kupoteza fahamu.

Niliwaona watu wengi wakiingia, wakipiga kelele. Na nikapoteza fahamu kwa mara nyengine.

Niliamka hospitalini na kuuliza kule ambapo mume wangu yuko.

Waliniambia kwamba wanamtibu katika chumba chengine.

Nilisema: Mimi ni muhubiri nimepitia mengi katika maisha yangu, nataka muniambie ukweli.

Daktari alianiangalia akaniambia mumeo hakufanikiwa.Sikuamini.

Kurudi kanisani kwa mazishi ya Harry lilikuwa tatizo kuu.

Mwezi mmoja uliopita nilikuwa katika kanisa hilo na rinda langu jeupe huku Harry akisimama mbele yangu akionekana mtanashati.

Sasa nimevaa mavazi meusi na Harry anaingizwa kwa jeneza.

Watu walidhani nimelaaniwa na kuwazuia watoto wao kunifikia. ''Ana bahati mbaya inayomfuata '',walisema.

Wakati mmoja karibia nikubali kwamba nina bahati mbaya.

Wengine walinituhumu kwa kumuua mume wangu.

Hilo liliniathiri sana nilikuwa na huzuni hadi kuchanganyikiwa.

Ukaguzi wa matibabu ulionyesha kile kilichotokea. Wakati moshi wa jiko ulipojaa chumbani alikosa hewa safi na kuaga dunia.

Nilihisi Mungu amenitenga. Sikuamini kwamba watu walikuwa wakicheka na kuendelea na maisha yao.

Siku moja nilikuwa nimeketi katika roshani nikiwaangalia ndege waliokuwa wakiruka na kusema: Mungu inawezekanaje unawalinda ndege hawa na sio mimi?

Wakati huo nilikumbuka kwamba kuna saa 24 kwa siku, nikiwa nimekaa ndani nikiangalia pazia , hakuna mtu anayeweza kukurejeshea saa hizo 24.

Kabla ugundue ni wiki moja , mwezi na mwaka umepotea. Huo ndio ulikuwa ukweli.

Niliambia kila mtu kwamba sitaweza kuolewa tena.

Mungu alimchukua mume wangu, na fikira za upweke zilikuwa nyingi na zenye uchungu mwingi, Kitu ambacho singependelea mtu yeyote kupitia.

''Uchungu huo ni mwingi, unahisi katika kucha zako.lakini kulikuwa na mtu mmoja Tonny Gobanga''.

Ambaye aliendelea kunitembelea. Alikuwa akinishinikiza kuzungumza kuhusu mume wangu na kufikiria kuhusu siku njema naye.

Siku moja hakunipigia simu kwa siku tatu na nilikasirika sana. Na hapo ndipo nilipogundua kwamba nimempenda.
Niliandika kitabu ''Crawling out of darkness'' kuhusu yalionipata ili kuwapa watu motisha wa kujitoa katika majanga.

Pia nilianzisha shirika kwa jina Kara Olmurani.

Tunashirikiana na manusura wa ubakaji- kama ninavyowaita na sio waathiriwa wa ubakaji.

Tunatoa ushauri na usaidizi.Tunataka kununua nyumba ambayo tunaweza kuwaweka na kuanza tena maisha kabla ya kukabili ulimwengu.

''Nimewasamehe walio nishambulia .Haikua rahisi lakini nilibaini kwamba ninajiumiza zaidi na watu ambao hawajali''.

Imani yangu pia inanitaka kuwasamehe na kutolipiza kisasi na badala yake kulipa kwa kufanya mema.

Kitu muhimu ni kuomboleza. Pitia kila hatua. Jiumize hadi pale unapohisi kufanya kitu kuhusu hali yako.

Lazima uendelee kusonga mbele, tambaa iwapo unaweza. Lakini elekea katika hatma yako kwa sababu inakusibiri na ni lazima uende kuichukua.

Friday, July 28, 2017

Image result for tendo la ndoa baada ya kujifungua

kufurahia tendo baada ya kujifungua inategemea zaidi na wewe mwenyewe (uponaji wako)na lini unadhani uko tayari vilevile ushirikiano wa kutosha kutoka kwa mume/mpenzi wako wakati unaendelea na uponaji baada ya kutoa kiumbe kipya duniani.

Ni hali ya kawaida kabisa kwa mwanamke kutokujiskia (kutonyegeka) au kutaka ngono kwa wiki chache tangu ujifungue na hii inatokana na kusubiri dam ya uzazi kuisha bila kusahau yale maumivu kule ukeni (sore) kupungua au kupona kabisa.

Ili kufanikisha uponaji wa haraka inategemea na wewe mwenyewe utakavojisaidia na kufuata ushauri wa Wakunga na Daktari wako bila kusahau njia unayotumia "kusababisha" uponaji wa haraka.

Njia ambayo wanawake wengi wa kiafrika wanaitumia ni maji ya moto na utumiaji huu wa maji unatofautiana na hii inategemea na Asili yako (kule utokako) kwanikuna baadhi huongezea aina ya majani (kama dawa) ili kusaidia uponaji wa mama mzazi, wenginehuchanganya maji hayo ya moto na unga unaotokana na aina fulani ya mizizi nakadhalika......Afrika tuna madawa mengi asilia ambayo yanafanya kazi nzuri kabisa.

Katika kipindi hiki mwanamke hupaswi kuharakisha mambo, nikiwa na maana kuhisi “msukumo” wa kupona haraka ili ungonoke na mumeo kwa kuhofia kuwa atachepuka, pamoja na kusema hivyo ni vema kujitahidi na kuwa karibu zaidi na mumeo/mpenzi kimapenzi na kushirikiana nae.

Sio “kudeka” kwa vile tu umezaa (kuzaa ni sehemu ya uanamke hivyo usimfanye mumeo/mpenzi wako kujihisi “mkosaji kana kwamba  kukupa mimba ilikuwa kosa wakati mlielewana.).

Siku ya mwanzo kungonoka baada ya kupona kuna uwezekano mkubwa wa wewe kutopata raha au utamu na badala yake ikawa maumivu fulani hivi ambayo sio makubwa sana yaani kama yale upatayo unapokaa muda mrefu bila kufanya tendo la ndoa”.

Vilevile unaweza ukahitaji kilainisho cha kutosha na hapa sizungumzii mate bali K-Y Jelly ili kukabiliana na ukavu wa uke ambao unaweza kujitokeza ktk ya “game”.

Kwa kawaida uke hujirudi kama awali ndani ya siku Arobaini au Miezi mitatu yote inategemea na uponaji wako na njia uliyotumia ilikusababisha uponaji wako.

Licha ya kuwa “sore” na damu ya uzazi kukupotezea hamau ya kungonoka au kufanya mpenzi na mume/mpenzi wako pia kuna sababu nyingine zinazoweza kupelekea wewe mwanamke mzazi kushindwa au kupoteza hamu ya kungonoka na hivyo kumkwepa Jamaa kila atakapo mambo fulani.

Baadhi ya sababu hizo ni:-
- Uchovu wa mwili na akili kutokana na kutokupata usingizi wa kutosha mishughuliko yako kama mwanamke na vilevile mama
.
- Maumivu ya mshono kama ulijifungua kwa njia ya upasuaji, uliongezewa njia au ulichanika kutokana na ukubwa wa mtoto inategemea na pia atakavyokuwa akitoka.

- Kutokupata muda wa kuwa karibu na mpenzi/mume kutokana na mapenzi yako mazitokwa mtoto wako, yaani unahisi kuwa mtoto anakuhitaji zaidi kuliko baba’ke.

- Kupoteza hali ya kujiamini kwa vile unadhani kuwa mwili wako hauko kama ilivyokuwa baada ya kujifungua
Image result for maumivu wakati wa tendo la ndoa
HII ni hali ambayo mwanamke anakuwa na hamu ya kufanya tendo  la ndoa lakini anapata ugumu kutokana na maumivu makali anayopata.

Hali hii inatokana na kubana au kukaza kwa misuli ya uke lakini pia  inaweza kusababishwa na matatizo ukeni.

Mfano endapo kuna michubuko au vidonda au kasoro yoyote ya uke,  aidha uke ni mdogo au maumbile ya uke hayana uwiano na uume. Tatizo hili huwapata wanawake wa rika zote ilimradi tayari yupo katika  umri wa kuzaa.

TATIZO LINAVYOGAWANYIKA

Tatizo hili la maumivu wakati wa tendo la ndoa limegawanyika katika maeneo makuu mawili. Kwanza ni Primary Dyspareunia .

Hapa  mwanamke anakuwa hana historia ya maumivu wala  hana historia ya kuwahi kufanya tendo hilo ndiyo, kwanza anaanza. Kitaalamu hali hii ya maumivu huitwa Honey moon Dypareunia au maumivu ya fungate na hutokea mara tu anapoanza kujamiiana kwa mara ya kwanza. Katika hali hii misuli ya uke inaweza kubana kutokana na michubuko au kuchanika ubikira au hata kuchanika upande wa chini wa uke na wakati mwingine  michubuko hutokea katika tundu ya mkojo.Hali ya michubuko inaweza kuwa mbaya na ikajitokeza hata kwa kugusa tu upande wa nje wa uke.

Maumivu yakiendelea au yakizidi husababisha mgonjwa apate matatizo ya kisaikolojia kiasi kwamba huanza kuogopa tendo lenyewe na kuhisi endapo atalifanya ataumia. Tatizo hili likileta michubuko kwenye njia ya mkojo husababisha maambukizi sugu ya kibofu cha mkojo kutokana na michubuko ya mara kwa mara ya tundu ya mkojo.

Maumivu ukeni hutokana pia na maandalizi mabovu kabla ya tendo ambapo uke unakuwa haujalainika kwa kutofanya romance ya kutosha,  kutofanya tendo hilo kwa ustaarabu, yaani kutumia nguvu au endapo mwanamke atakuwa na maambukizi ukeni mfano fangasi ambayo huambatana na kutokwa na uchafu ukeni na muwasho, magonjwa ya uke kama kuvimba kwa tezi za uke, kuvimba kwa mashavu ya uke au hali yoyote inayomwondolea amani mwanamke pale ukeni inaweza kumfanya kisaikolojia aathirike na kuhisi maumivu wakati wa tendo.

Michubuko ukeni au kuhisi moto ukeni wakati wa tendo la ndoa kunaweza kusababishwa na matumizi ya vilainishi visivyofaa  au kuumwa kutokana na uwepo wa vinyweleo virefu ukeni na endapo havikupunguzwa vitaingia ukeni wakati wa tendo na kukuchubua.  Kasoro katika ubikira pia husababisha mwanamke ahisi maumivu wakati wa tendo.

Maumivu haya huwa hayahusiani na yale ya awali ya fungate na wakati mwingine huanza baada ya kipindi kirefu cha miaka

mingi tangu uanze tendo la ndoa na wengine huwa na tatizo hili tayari wana watoto. Chanzo cha tatizo hili ni ukavu ukeni, umri mkubwa wa mwanamke na kusinyaa kwa misuli ya uke.

Matatizo haya isipokuwa la umri mkubwa  hutokea katika umri wa kati na tayari mwanamke  anayo historia ya kuwa katika mahusiano na hata tayari ana watoto. Umri mkubwa tunaouzungumzia ni zaidi ya miaka hamsini. Kubana misuli ya ukeni hutokana na makovu baada ya kushonwa msamba au kuongezewa njia wakati wa kujifungua au upasuaji wa kurekebisha fistula pia husababisha tatizo hili.

Vyanzo vingine vya maumivu haya ya tendo la ndoa ni kushuka kwa kizazi ambapo mwanamke atahisi kitu kama gololi ukeni wakati  akijisafi sha au kuhisi kizazi kinasukumwa wakati wa tendo, kugeuka kwa kizazi, matatizo katika tabaka la ndani la kizazi, maambukizi sugu ukeni ambapo uchafu na muwasho ukeni hujirudiarudia, matatizo katika njia ya mkojo na maambukizi katika viungo vya uzazi ’PID’  husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Matitizo ya kisaikolojia husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa pale ambapo misuli ya ukeni itakaza na mwanamke anapochunguzwa huwa hana tatizo au kasoro yoyote ukeni. Matatizo katika mishipa ya fahamu ya ukeni, kuogopa tendo lenyewe kuhisi utapata maumivu au kama kuna historia ya kuingiliwa kwa nguvu na ukaumia, kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu tendo la kujamiiana, yote haya na mengine mengi humharibu mwanamke kisaikolojia na kujikuta anaanza kuhisi maumivu hata kabla ya tendo lenyewe kwa kuingiwa na hofu.

 Image result for maumivu wakati wa tendo la ndoa

Hali nyingine inayoweza kumfanya mwanamke aathirike kisaikolojia na asiwe tayari kwa tendo na hata akilifanya apate maumivu ni kuogopa kupata ujauzito wakati hayupo tayari kwa hilo, kuogopa kupata maambukizi, kulazimishwa penzi endapo haupo tayari na mwanaume uliye naye na kuhisi kuna tofauti ya maumbile na mume uliyenaye.

Endapo mwanaume anakukwaza kutokana na kutokwa na jasho jingi sana wakati wa tendo, kutoa harufu mbaya ya pua, kinywani, makwapani au sehemu zake za siri, huwa na magonjwa ya ngozi au hata mwilini mwake, matatizo haya huweza kumwathiri mwanamke kisaikolojia na asifurahie tendo na kutotoa ushirikiano wakati wa tendo na kupata maumivu.

UCHUNGUZI Tatizo hili ni pana sana, unaweza kuhisi una kasoro au maambukizi kumbe tofauti. Kwa hiyo basi ni vizuri uchunguzwe kwa umakini katika kliniki za madaktari wa akina mama katika hospitali za mikoa ili kujua chanzo halisi cha tatizo.
 Image result for ugumba

SABABU ZIPI ZINAZOLETA TATIZO LA UGUMBA (INFERTILITY)
Kwa wanawake - Tatizo la ugumba linaweza kutokea wakati wa Yai au kiumbe kilichomo ndani ya mfuko (uterus) wa uzazi kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto.

- Mayai yaliyo ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining)

- Matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa uzazi (uterus).

- Matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai (eggs).

 Image result for ugumba

TATIZO LA UGUMBA KWA WANAWAKE HUSABABISHWA NA

- Matatizo ya autoimmune disorders kama antiphospholipid syndrome (APS)
Kuwepo kwa cervical anti-gens ambazo huua mbegu za mwanamume ambazo husababisha mwanamke kutopata ujauzito.

- Matatizo katika uterus na shingo ya kizazi (cervix) kama vile uvimbe (fibroids or myomas) na birth defects

- Matatizo ya kuziba kwa mirija ya uzazi

- Mazoezi kupita kiasi (excessive exercise),
Afya iliyodhoofika (poor nutrition),
Matatizo ya kula (eating disoder).

- Baadhi ya madawa au sumu.

- Msongo wa mawazo (emotional stress)

- Tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal inbalance)

- Uzito uliopitiliza (obesity)

- Unywaji pombe kupindukia (heavy alcohol intake) –
Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari (diabetes)

- Magonjwa ya akina mama (Pelvic inflammatory disease PID) - Ovarian cysts and polycytic ovarian syndrome

- Magonjwa ya zinaa (sexually transmitted disease, STD) au endometriosis

-Saratani

- Uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk.

- Matatizo ya hedhi – wanawake wanaopata hedhi bila kutoa mayai (anovulatory menstrual cycle)
Hizo ni baadhi tu ya mambo yanayoweza kusababisha ugumba kwa akina mama.
Image result for ugumba

Thursday, July 27, 2017

Watafiti wanaochunguza matokeo yao tafiti 200 wanasema kuwa upungufu wa kiwango cha mbegu za kiume miongoni mwa Wanaume kutoka Marekani kaskazini, Ulaya, Australia na New Zealand ufikia nusu yake.

Baadhi ya wataalam wanashaka kuhusu matokeo hayo.

Lakini mtafiti bingwa anayeongoza utafiti huo Dkt Hagi Levine anasema kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kile kitakachofanyika katika siku za usoni.

Dkt. Levine ambaye ni mtaalamu wa magonjwa aliambia BBC kwamba iwapo mwenendo huo utaendelea basi huenda binadamu wakatoweka.

Utafiti huo ambao ni miongoni mwa tafiti kubwa ulileta matokeo ya tafiti 185 kati ya 1973 na 2011.

''Iwapo hatutabadili mienendo yetu ya kuishi mbali na kemikali na mazingira yetu ,nina wasiwasi mkubwa kuhusu kile kitakachofanyika siku za usoni''.

Hatimaye tutakuwa na tatizo hususan na uzazi kwa jumla na huenda ikawa kutoweka kwa binaadamu.

Wanasayansi ambao hawakushirikishwa katika utafiti huo wameusifu ubora wake lakini wanasema kuwa huenda ni mapema mno kutoa tangazo hilo.

Dkt. Levina kutoka chuo kikuu cha Hebrew mjini Jerusalem alibaini kupungua kwa asilimia 52.4 ya manii huku asilimia 59.3 ya mbegu za kiume kutoka kwa wanaume kutoka maeneo ya Marekani kaskazini, Ulaya, Australia na New Zealand yakishuka zaidi.

Tuesday, July 25, 2017

Wanasayansi Afrika Kusini wamebaini kwamba mtoto aliyeambukizwa virusi vya Ukimwi, ameishi kwa miaka minane na nusu bila viini hivyo.

Mtoto huyo alipewa dawa za majaribio ya kukabiliana na virusi hivyo alipozaliwa lakini hajapewa dawa zozote za kukabiliana na  virusi hivyo tangu afikishe mwaka mmoja.
Hii ni mara ya kwanza kwa mtu mwenye VVU kuishi bila virusi hivyo barani Afrika.
Wanasayansi waliogundua kuhusu afya ya mtoto huyo mwenye miaka 9 na nusu kwa sasa, wanamuangalia na kumfuatilia kwa karibu zaidi.
 
Wanasema kuwa matukio kama hayo ni machache na kwamba familia ya mtoto huyo ina furaha.
Watafiti wanaamini kupotea huko kwa vurusi sio kwa sababu ya matibabu lakini mtoto huyo ana jeni ama kinga zisizokuwa za kawaida ambazo zimemlinda dhidi ya virusi vya Ukimwi.

Monday, July 24, 2017


Furaha kubwa ya mama mja mzito ni kumzaa mtoto aliye na afya njema na asiye na shida yoyote. Lakini kwa akina mama wengi, furaha hii hukatizwa na unene wa tumbo unaokuja baada ya kujifungua.
Shida kubwa huwa ni tumbo ambalo ni nene kuuliko mwili. Sababu hii huwafanya akina mama wengine kutoupenda mwili wao.

jinsi ya kupunguza tumbo baada ya kujifungua. Iwapo watayafuatilia maagizo haya vikamlilifu, basi unene wa tumbo baada ya kujifungua utaisha.

1- Kuwa na motisha

Ni muhimu kwa mama kuwa na motisha anapoamua kulipunguza tumbo baada ya kujifungua. Tena, anafaa kuwa na uvumilivu. Kupunguza tumbo hilo huchukua muda sawia na ule wa kubeba mimba. Kwa ufupi, inawezekana kwamba kama tu ilivyochukua miezi tiza kwa tumo kunenepa, itachukua miezi sawia kupungua.
Hivyo basi, mama hafai kufa moyo au kuwa na haraka. Kuna uwezekano kwamba mama anaweza kufanya vitu ambavyo hakuzoea pale awali kama kufanya mazoezi, kuacha vyakula fulani na kuanza kuvila vingine. Hii ni safari inayohitaji motisha.

2- Kunyonyesha mtoto

Njia ya pili ya kupunguza tumbo ni kumnyonyesha mtoto. Ni asili kwa mwili wa mwanamke kurudia hali ya mbeleni pole pole baada ya kumzaa mtoto.
Kwa mfano, mfuko wa uzazi hurudia hali yake ya kawaida. Vile vile, iwapo watakua na subira na kuwanyonyesha wanao, basi tumbo hurudia ukubwa ule wa awali.

3- Kuepukana na pombe

Iwapo mama anakunywa pombe kwa wingi baada ya kujifungua, ni ngumu kwa tumbo kurudi ukubwa ule wa kawaida. Pombe, pamoja na vinywaji vyenye sukari nyingi, huadhiri njia ya ini ya kufanya kazi. Adhari mojawapo ni kutotengeneza misuli ifaavyo mwilini.
Ini linapolemewa kuunda misuli, mwili hujaa mafuta na kusababisha mtu kunenepa. Hivyo basi, mama anapokunywa pombe, sio tumbo tu linalonenepa; mwili wote huadhirika. Hivyo basi, unywaji wa pombe haufai baada ya kujifungua.

4- Kufanya mazoezi ya tumbo

Huenda ikawa vigumu kuanza mazoezi mara tu mama anapojifungua. Hivyo basi, ni vyema kusubiri mpaka mwili utakaporudia hali ya kawaida na kupata nguvu. Hata hivyo, mama hafai kufanya mazoezi mazito au mengi sana.
Kwahivyo, anza kwa mazoezi madogomadogo yanayolenga tumbo. Kwa mfano, unaweza kulala kwa mgongo na kuyakunja magoti. Baada ya hapo, unauinua mwili wa juu polepole kisha kulala tena. Rudia zoezi hili mara kadhaa kwa siku. Kuna mazoezi mengi ambayo utaelezwa na daktari.

5- Kutembea

Kutembea ni aina ya mazoezi ambayo husaidia kupunguza tumbo. Inawezekana kutembea kukaonekana kama mazoezi duni, lakini, husaidia sana kwa kulainisha tumbo.
Mtu anapotembea, misuli mingi mwilini hutumika, ikiwemo ile ya tumbo. Hivyo basi, mafuta yaliyokusanyika sehemu ya tumboni huisha na tumbo kupungua. Zoezi hili linaweza kukufaa sana iwapo utambeba mtoto wako mgongoni (kuongeza uzito).

6- Kufanyisha misuli mikubwa mazoezi

Hata ingawa lengo ni kupunguza tumbo, mama anafaa kuifanyisha misuli yote mazoezi. Unapofanya mazoezi yalengayo tumbo pekee, mafuta huchomeka polepole mwilini.
Iwapo unataka kulipunguza tumbo haraka, basi unaarifiwa kufanya mazoezi yalengayo misuli mikubwa mwilini. Hii ni kama miguu, mikono na mgongo. Hii itazuia kulipunguza tumbo na kubakia na mafuta (unene) kwingine mwilini.

7- Kupumua kwa undani

Zoezi hili ni rahisi sana na mama anaweza kulianza saa moja tu baada ya kujifungua. Mama anafaa kuketi kitako na kuvuta hewa kwa ndani.
Anapoivuta kwa ndani, anafaa kuukunjua mgongo na kasha kuifungia hewa ile kidogo tu. Kasha, anaitoa pumzi ile na kutulia kidogo, kasha kurudia. Zoezi hili husaidia misuli ya tumbo kulegeza na kumfanya kupona kwa haraka.

8- Kufunga kitambaa cha kupunguza tumbo

Hii ni njia mojawapo ya zile zinazotumika sana na ambayo imewkuwepo kwa muda mrefu. Muda mfupi baada ya kujifungua, kitambaa spesheli kilichotengenezwa kwa pamba hufungwa tumboni.
Lengo la kitambaa hicho ni kupunguza kufura na kuirudisha misuli kuwa na ukubwa wa kawaida. Kwa kawaida, kitambaa hicho hufungwa kwa muda wa wiki moja kasha mama anapumzika kiasi na kurudia tena. Kitambaa cha kawaida kilichoundwa kwa pamba kinaweza kutumika pia.

9- Kula chakula cha kutosha

Kadri na maelezo fulani kuwa mama akila kiasi atapunguza tumbo, ni bora kuzuia njaa kabisa. Kando na kutopunguza tumbo, njaa inaweza kuzuia kupona kwa haraka.
Mama anapokaa njaa kwa muda, kuna uwezekano kuwa atakula chakula kingi baadaye. Kula chakula kingi kutachangia kunenepa kwa tumbo.

10- Kula vyakula vidogo mara nyingi kwa siku

Badala ya kukaa njaa kwa muda kasha kula chakula kingi baadaye, ni heri kula vyakula vidogovidogo mara kadhaa kwa siku. Hii inawezesha mwili kusiaga chakula chote bila kuhifadhi cha ziada kama mafuta mwilini. Nguvu itokanayo na kula vyakula vidogovidogo hutumika kikamilifu na kuzuia kunenepa tumbo na mwili kwa jumla.

11- Punguza vyakula vya ‘kujituliza’

Kwa kawaida, mama anapojifungua, yeye hudaisha vitu kadhaa anavyohisi kwamba mwili unahitaji ili kuwa imara. Baadhi ya vitu hivyo ni chakula.
Shida ni kuwa, vingi vya vyakula hivyo huwa na sukari, mafuta na bidhaa zingine ambazo huongeza mafuta mwilini. Kwa mfano soda, keki, viazi, peremende na bidhaa zilizotengenezwa kwa ngano. Ni sawa kuvila vyakula hivi, lakini, vinafaa kupunguzwa muda uendavyo.

12- Kula vyakula vya mimea

Utafiti unaonyesha kuwa vyakula vya mimea (sio nyama) vina mafuta kidogo na madini mengi ya protini ya mboga. Hivyo basi, vinapunguza kuongezeka kwa mafuta mwilini na kuzuia kunenepa.
Akina mama wanahimizwa kujiepusha na kula nyama wakati huu na kula vyakula vitokanavyo na mimea.
Baadhi ya vyakula hivyo ni:
  • Mboga kama mchicha (spinach), sukuma wiki na kabichi.
  • Matunda kama machungwa, maembe, mapapai, tikitiki maji, parachichi, mapera na mengineyo.

13- Kupunguza kiasi cha chakula

Mama anakubalika kula chakula zaidi ya kawaida anapokuwa na mimba. Hii ni kwasababu ana binadamu mwingine ndani yake mwenye mahitaji mengi. Hata hivyo, baada ya kujifungua, anafaa kupunguza kiasi cha chakula alacho.
Kula chakula ziada kinalifanya tumbo kuwa nzito na kukusanya mafuta. Hii huchangia kwa tumbo kukaa likiwa nene au kuzidi kunenepa.

14- Kula kiamsha kinywa

Kiamsha kinywa ni mojawapo wa mlo muhimu sana kwa mama aliyejifungua. Anapokula kiamsha kinywa, mwili huchangamka na kusiaga chakula chote kikamilifu. Mwili pia hukaa tayari kuvipokea vyakula vingine wakati wa mchana na kuvisiaga vizuri.
Mwisho kabisa, hakuna uwezekano wa mama kuhisi njaa kupita kiasi na kuchangia kwake kula kupita kiasi. Kwa njia hii, tumbo la baada ya kujifungua hupungua.

15- Kunywa maji baridi ya kutosha

Maji husaidia mwili wa mama aliyejifungua kupona kwa haraka. Pili, maji hujaza tumbo na kuzuia mama kula chakula kingi kupita kiasi. Hivyo basi, anaweza kurejelea hali yake ya kawaida bila kuhisi njaa.
Kunywa maji baridi kutasaidia kuchoma mafuta mwilini wakat mwili unapojikakamua kuyapa joto. Hivyo basi, mafuta yanatolewa mwilini na tumbo kupungua.

Saturday, July 22, 2017

KUNA magonjwa mengi yanayosababisha mtu kukojoa udenda (usaha), uume kuuma au kuwasha wakati wa kukojoa.

Magonjwa yanayosababisha hali hiyo kwa sana ni pamoja na klamidia (chlamydia), kisonono (gonorrhea), trichomoniasis na magonjwa mengine yanayoathiri njia ya mkojo (nongonococcal urethritis)

Klamidia (Chlamydia)

Klamidia (Chlamydia) ni moja ya magonjwa ya zinaa. Ugonjwa huu unasababishwa na viini vya bakteria vwanaojulikana kitalaamu kama Chlamydia trachomatis na waweza kuathiri uke, mrija wa kupitisha mkojo, uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.

Klamidia (Chlamydia) ndio ugonjwa wa zinaa unaotokana na bakteria unaoongoza kwa maambukizi mengi zaidi duniani ukifuatiwa na ugonjwa wa kisonono (gonorrhea).

Ugonjwa wa klamidia (chlamydia) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiana. Ugonjwa huu ni wa hatari kwa sababu mama mjamzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.

Pia, kuchangia vifaa vya kuogea kama taulo vya mtu mwenye maambukizi, kuchangia vyoo vya kukaa na mtu mwenye maambukizi na kukumbatiana na mtu mwenye maaambukizi.

Vile vile ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kupitia mbawa, kupitia vinyesi vya ndege kama kuku, bata na kasuku walioambukizwa klamidia (chlamydia) inayopatikana kwa wanyama ijulikanayo kitaalamu kama Chlamydophila psittaci na kusababisha aina ya homa ya mapafu au homa ya kasuku (psittacosis).

Klamidia huathiri sehemu tofauti za mwili wa binadamu kama macho, mfumo wa upumuaji, sehemu za siri kama makalio, viungo vya uzazi na tezi (lymph nodes).

Huchukua siku 1-14 tangu maambukizi hadi kuonekana kwa dalili. Asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume wanaopata maambukizi ya ugonjwa huu huwa hawaonyeshi dalili za moja kwa moja.

Kwa wanaume, ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitishia mkojo, dalili kama vile uume kuwasha, kutokwa na ute na kusikia maumivu wakati wa kukojoa, sehemu ya tundu kwenye uume kuwa nyekundu, kuvimba na kuwasha pia kuhisi maumivu kwenye korodani na tezi zilizopo sehemu za siri ambazo huvimba na kuambatana na maumivu.

Dalili za ugonjwa huu kama umeathiri makalio (puru) kwa wanawake na wanaume ni kama kuwashwa na kutokwa na damu kwenye puru, maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa na kutokwa na uchafu kama kamasi kutoka kwenye puru.

Iwapo vimelea vya klamidia vitaathiri macho, wanawake na wanaume huwa na dalili kama kuvimba macho, macho kuwa mekundu, kuwasha na hata kutokwa na majimaji machoni.

Klamidia inayoambukiza kwenye macho hujulikana kitaalamu kama Chlamydia conjunctivitis au Trakoma (trachoma) na ndiyo inayoongoza kwa kusababisha upofu duniani.

Dalili za klamidia kwa watoto wachanga hutokea katika kipindi cha wiki mbili kwenye macho, na iwapo ni homa ya mapafu dalili zake hujitokeza katika kipindi cha wiki mbili hadi miezi 3 baada ya kuzaliwa.

Madhara ya ugonjwa huu kwa wanaume ni kuathiri korodani na kusababisha mwanamume kukosa uwezo wa kutengeneza mbegu za uzazi (manii/shahawa) au kuwa tasa na pia husababisha maambukizi kwenye tezi dume (prostatitis).

Kwa wanawake, husababisha maambukizi kwenye mirija ya uzazi, mfuko wa uzazi, na mayai ya uzazi, kwa hivyo kusababisha ugonjwa wa uvimbe katika fupanyonga (PID).

Pia huongeza uwezekano wa wanawake kupata mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancies).

Mwanamke hupata maumivu sugu kwenye nyonga na ugonjwa wa mifupa (arthritis) aina ya Reiters syndrome. Vilevile, klamidia huweza kusababisha ugumba kwa mwanamke kama hatapata tiba na kwa wanawake wajawazito, klamidia husababisha wajifungue kabla ya wakati wao.

Aidha, mtoto anaweza kuzaliwa na maambukizi kwenye masikio, sehemu za siri, macho na kwenye mapafu, yaani homa ya mapafu, na kama mtoto hatapatiwa tiba ya haraka ya macho baada ya kuzaliwa basi anaweza kuwa kipofu.

Kisonono (Gonorrhea)

Ugonjwa wa Kisonono (gonorrhea) husababishwa pia na bakteria waitwao kitalaamu Neisseria gonorrhoeae unapofanya mapenzi na mtu mwenye kisonono.

Ugonjwa huu unaweza kuaathiri viungo kama vile uke, uume, sehemu ya haja kubwa na ya haja ndogo, na hata koo au mdomo kama ukifanya mapenzi ya kunyonyana.

Wanaume huwa na dalili kama uume kutoa ute wa njano au kijani, na kupata maumivu wakati wa kukojoa (mkojo kuchoma).

Pia kuna uwezekano wa kuwashwa ama kutokwa na maji maji katika sehemu ya kupitishia haja kubwa. Ingawa hivyo baadhi ya watu hawaoni dalili zozote kabisa lakini bado wanaweza kuwaambukiza wanaofanya mapenzi nao.

Trichomoniasis

Ugonjwa wa Trichomoniasis unasababishwa na vimelea vya jamii ya protozoa vinavyojulikana kitalaamu kama Trichomonas vaginalis.

Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitisha mkojo (urethra) na tupu ya mwanamke (vagina). Huathiri sana wanawake kuliko wanaume na wanawake wenye umri mkubwa wako katika hatari zaidi kuliko mabinti wadogo.

Ugonjwa huu hupatikana kwa njia ya kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathirika na Trichomoniasis.

Dalili za Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4 mpaka ya 28 baada ya mtu kupata maambukizi. Wanaume huwa hawaonyeshi dalili zozote lakini baadhi wanaonyesha dalili kama kuwasha ndani ya uume, kutokwa na uchafu au majimaji kutoka kwenye uume, kuwasha au mkojo kuchoma wakati wa kukojoa au baada ya kutoa shahawa.

Mwanaume asipopata matibabu mapema huongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI na huongeza hatari ya kupata saratani ya tezi dume.

Magonjwa mengine ya njia ya mkojo

Magonjwa mengine yanayoathiri njia ya mkojo husababishwa na bakteria na huathiri mfereji wa kupitisha mkojo (urethra). Magonjwa hayo husambazwa kwa kujamiiana. Dalili kwa wanaume ni kutokwa na ute kwenye tundu la uume na huenda akahisi maumivu wakati wa kukojoa au akahisi maumivu na kuwashwa-washwa kwa pamoja.

Ikiwa unapata dalili isiyo ya kawaida ni busara kutafuta msaada wa kitabibu na siyo kusubiri mpaka hali inakuwa mbaya au kujinywea tu dawa bila ushauri wa daktari.

Njia sahihi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa ni kuacha, kuepuka kujamiiana au kufanya ngono zembe na sizizo salama.

Kwa wanawake wajawazito, ni vizuri kuhudhuria kliniki mapema wakati wa ujauzito na kupimwa vipimo mbalimbali ili kubaini ikiwa mama mjamzito ameambukizwa na ugonjwa wowote wa zinaa na kupatiwa matibabu mapema.

Kwa wale wenye maambukizi wanashauriwa kuchukua tahadhari ya kutowaambukiza wapenzi wao kwa kufanya ngono salama.

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR