HILI ni tatizo linalosababisha ugumba kwa wanawake kwa kiasi kikubwa. Wanawake wanaoshindwa kupata ujauzito hukabiliwa na matatizo matatu;
* kwanza kabisa ni kuziba kwa mirija ya mayai kama tutakavyoona leo
* matatizo katika mfumo wa homoni ambapo kuna sababu zake tutakuja kuziona katika matoleo yajayo.
* dalili kuu ni kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi, kutopata hedhi na kupata damu kwa muda mrefu au muda mfupi sana ambazo ni siku moja au mbili.
* Dalili nyingine ambazo siyo nzuri katika mfumo wa homoni ambazo zinaweza kufanya mwanamke asipate mimba ni matiti kutoa maziwa wakati siyo mjamzito na wala hana mtoto anayenyonya.
* Tatizo la tatu ni kwa upande wa mwanaume kutokuwa na mbegu zenye ubora.
Yaani hana nguvu za kutosha au anawahi kumaliza tendo la ndoa Premature Ejaculation.
* Kuziba mirija ya uzazi huzuia mbegu na mayai kukutana na kutungisha mimba. Mirija ya uzazi pia huitwa Oviducts, Uterine Tubes au Salpinges
Wakati ujao tutatazamia aina za uzibaji Wa mirija ya uzazi.
0 comments:
Post a Comment