Friday, July 28, 2017
kufurahia tendo baada ya kujifungua inategemea zaidi na wewe mwenyewe (uponaji wako)na lini unadhani uko tayari vilevile ushirikiano wa kutosha kutoka kwa mume/mpenzi wako wakati unaendelea na uponaji baada ya kutoa kiumbe kipya duniani.
Ni hali ya kawaida kabisa kwa mwanamke kutokujiskia (kutonyegeka) au kutaka ngono kwa wiki chache tangu ujifungue na hii inatokana na kusubiri dam ya uzazi kuisha bila kusahau yale maumivu kule ukeni (sore) kupungua au kupona kabisa.
Ili kufanikisha uponaji wa haraka inategemea na wewe mwenyewe utakavojisaidia na kufuata ushauri wa Wakunga na Daktari wako bila kusahau njia unayotumia "kusababisha" uponaji wa haraka.
Njia ambayo wanawake wengi wa kiafrika wanaitumia ni maji ya moto na utumiaji huu wa maji unatofautiana na hii inategemea na Asili yako (kule utokako) kwanikuna baadhi huongezea aina ya majani (kama dawa) ili kusaidia uponaji wa mama mzazi, wenginehuchanganya maji hayo ya moto na unga unaotokana na aina fulani ya mizizi nakadhalika......Afrika tuna madawa mengi asilia ambayo yanafanya kazi nzuri kabisa.
Katika kipindi hiki mwanamke hupaswi kuharakisha mambo, nikiwa na maana kuhisi msukumo wa kupona haraka ili ungonoke na mumeo kwa kuhofia kuwa atachepuka, pamoja na kusema hivyo ni vema kujitahidi na kuwa karibu zaidi na mumeo/mpenzi kimapenzi na kushirikiana nae.
Sio kudeka kwa vile tu umezaa (kuzaa ni sehemu ya uanamke hivyo usimfanye mumeo/mpenzi wako kujihisi mkosaji kana kwamba kukupa mimba ilikuwa kosa wakati mlielewana.).
Siku ya mwanzo kungonoka baada ya kupona kuna uwezekano mkubwa wa wewe kutopata raha au utamu na badala yake ikawa maumivu fulani hivi ambayo sio makubwa sana yaani kama yale upatayo unapokaa muda mrefu bila kufanya tendo la ndoa.
Vilevile unaweza ukahitaji kilainisho cha kutosha na hapa sizungumzii mate bali K-Y Jelly ili kukabiliana na ukavu wa uke ambao unaweza kujitokeza ktk ya game.
Kwa kawaida uke hujirudi kama awali ndani ya siku Arobaini au Miezi mitatu yote inategemea na uponaji wako na njia uliyotumia ilikusababisha uponaji wako.
Licha ya kuwa sore na damu ya uzazi kukupotezea hamau ya kungonoka au kufanya mpenzi na mume/mpenzi wako pia kuna sababu nyingine zinazoweza kupelekea wewe mwanamke mzazi kushindwa au kupoteza hamu ya kungonoka na hivyo kumkwepa Jamaa kila atakapo mambo fulani.
Baadhi ya sababu hizo ni:-
- Uchovu wa mwili na akili kutokana na kutokupata usingizi wa kutosha mishughuliko yako kama mwanamke na vilevile mama
.
- Maumivu ya mshono kama ulijifungua kwa njia ya upasuaji, uliongezewa njia au ulichanika kutokana na ukubwa wa mtoto inategemea na pia atakavyokuwa akitoka.
- Kutokupata muda wa kuwa karibu na mpenzi/mume kutokana na mapenzi yako mazitokwa mtoto wako, yaani unahisi kuwa mtoto anakuhitaji zaidi kuliko babake.
- Kupoteza hali ya kujiamini kwa vile unadhani kuwa mwili wako hauko kama ilivyokuwa baada ya kujifungua
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
This is great
ReplyDelete