Monday, July 10, 2017

Lishe wakati wa ujauzito ni muhimu kwa ajili ya afya yako na maendeleo mazuri ya mtoto anayekua tumboni.

FUATA MLOLONGO HUU KUWA NA LISHE BORA;

1.Jitahidi upate mlo kamili kila siku kwa kupata vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji ya kutosha.Fanya nusu ya mlo wako uwe ni mchanganyiko wa matunda na mboga za majani.

2.Tumia nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona au mtama, mchele usiokobolewa, mikate ya brown au whole grain cereals.

3.Tumia maziwa yenye fafi kidogo( skimmed milk) au maziwa na vinywaji vya soya.

4.Chagua vyanzo vyako vya protini zaidi katika samaki, kuku, mayai, jamii ya maharage, soya na karanga.

5.Tumia zaidi mafuta ya mimea katika mapishi yako kama mafuta ya alizeti, pamba au mizeituni (Olive oil).

6.Punguza vyakula vyenye sukari za kuongeza (hasa artificial sugars) na mafuta kama biskuti, pipi, soft drinks, soda, pipi, ice creams, vyakula vya kukaanga na hot dogs.Kunywa maji mengi, zisipungue lita 2.5 kwa siku.

7.Mazoezi mepesi kama kutembea kwa dakika 30 kwa siku.Epuka matumizi ya pombe kwani yataathiri afya ya mtoto wako.

8.Tumia virutubisho ziada (supplements) utakazopata kliniki.

WAWEZA ACHA MAONI YAKO HAPA.

Related Posts:

  • SABABU ZINAZOPELEKEA KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZITO.HILI ni tatizo linalosababisha ugumba kwa wanawake kwa kiasi kikubwa. Wanawake wanaoshindwa kupata ujauzito hukabiliwa na matatizo matatu; * kwanza kabisa ni kuziba kwa mirija ya mayai kama tutakavyoona leo * matatizo katika… Read More
  • KUNAWA MIKONO NI AFYA.Wakina mama wengi wenye watoto wachanga hawana kawaida ya kunawa mikono Mara kwa Mara watakapo kumuhudumia mtoto. Yakupasa kunawa mikono kila Mara kwa kufuata utaratibu huu; *Kabla ya kunyonyesha *Kabla ya kumvisha au kumvua … Read More
  • FAHAMU KUHUSU FISTULA.fahamu kuhusu fistula Fistula ni nini?  Fistula ni shimo ambalo hutokea kati kati ya kibofu cha mkojo na uke au kati kati ya njia ya haja kubwa na uke wa mwanamke ambaye amejifungua kwa shida. Shimo hutokea pale amb… Read More
  • ZIFAHAMU DALILI ZA HATARI KWA MTOTO MCHANGAHistoria ya ugumu wa kula, au mtoto hawezi kula kwa sasa. Historia ya mitukutiko, au mtoto anatukutika kwa sasa. Mtoto mchanga anaonekana mlegevu au amepoteza fahamu. Mtoto anasonga tu iwapo amesisimuliwa. Kupumua kwa haraka… Read More
  • MADHARA YA UPUNGUFU WA DAMU KWA MJAMZITOSehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mama na mtoto iki… Read More

0 comments:

Post a Comment

Dondoo Zilizosomwa Sana hapa leo..!!

VIDEOS BAR